Wednesday, May 28, 2014

MANENO YA KWELI YASIYO NA CHEMBE YA SHAKA NDANI YAKE - 5




                   (6)     Mambo ya kweli yaliyomo ndani ya Qur’an.  Ndani ya Qur’an
kuna ukweli mbalimbali kuhusu mambo ya kale ambayo hayakuwa yakijulikana kwa watu wa rika na zama za Muhammad (S.A.W).  Katika Aya mbalimbali tunakuta rejea ya maajabu ya kisayansi yanayohusu ulimwengu na uhai, madawa, hisabati (mahesabu).  Je mtu asiyesoma angeweza kuhusika na utambuzi wa mambo hayo ya kielimu?  Muhammad angewezaje kusema kuwa dunia ipo katika muundo wa yai? 
Angewezaje kuijua nadharia ya upanukaji wa ulimwengu?  Angewezaje kusema kuwa element za maAda inayounda ulimwengu zote ni za aina moja? Kwamba msongamano wa hewa huongezeka kadiri mtu aendavyo juu na hivyo kupumua huwa tabu(1), na jinsi jua na mwezi vinavyoelea angani(2)?  Qur’an imejaa mifano kama hiyo.  Muhammad asiyesoma aliwezaje kujua mambo ya kisayansi ambayo yamekuja kujulikana hivi karibuni tu kwa msaada wa maabara na satelait za kisasa?
                        Rejea Surat Naazia’at 79:30, Dhariyaat 51:47na Anbiyaa 21:30)


                   (7)     Makemeo kwa Muhammad.  kuna Aya nyingi za
Qur’an, Mtume amekemewa.  Sura iitwayo “Abasa” yaweza kuwa mfano unaojulikana vyema:-

“Alikunja uso na akageuza mgongo.  Kwa sababu alimjia kipofu” .

Siku moja kipofu mmoja aliyeitwa Abdullah Ibn Umm Maktum, alimkatiza Muhammad (S.A.W) wakati akizungumza na Walid na wakubwa wengine wa Kikuraishi.  Mtume akionesha kutomtambua kipofu huyo aliinua sauti yake kwa ari na kuomba maelekezo ya kidini, lakini Muhammad akiudhika na uingiliaji kati huo, alikunja uso na kugeuza mgongo.  Aya hiyo ni lawama kwa Mtume kwa kitendo chake kwenye tukio hilo. Udhaifu ni sifa za mwanadamu.

Vile vile kuna idadi ya mifano mingine kama hiyo ndani ya Qur’an.  Je inaingia akilini kufikiri kuwa Muhammad ndiye aliyetunga kitabu ambacho ndani yake amekemewa?
                                                                       
                             Wala usiseme kabisa juu ya jambo lolote.  Hakika mimi
nitalifanya kesho, isipokuwa Mungu akipenda yeye mtunzi mwenyewe analaumiwa?  Kuna matukio mengi ambapo Muhammad (S.A.W) aliweka katika namna fulani, lakini Qur’an kwa uwazi kabisa huilaumu tabia yake ya kuonesha kosa alilotenda.  Muhammad hakujisikia vibaya kunukuu matukio hayo kama angekuwa ndiye mtunzi wa Qur’an je asingebadilisha rekodi hizo kwa kuzifuta au kwa kuzirekebisha ili kuakisi mapendeleo yake mwenyewe?

                   (8)     Kipindi cha muda baina ya tamaa ya Muhammad ya kuongea
na ufunuo uliokuwa ukimfikia.  Wakati fulani Muhammad (S.A.W) alihisi udharura wa kuzungumzia mambo fulani au kutoa maelekezo kuhusu namna ya kuyatenda.  Lakini bado alisubiri usiku na mchana mpaka agizo limfikie kabla ya kufanya vitu hivyo kujulikana kwa watu wengine.

HEBU TUJIULIZE?
          Kitabu kilichotengezwa na binadamu kiliwezaje
kutangaza umoja wa Mungu katika mtindo na mfumo wa uadilishaji ambao haukupatikana katika maandiko matakatifu yaliyotangulia?
Je akili yenye busara na nguvu haitoshi kupinga moja kwa moja hoja ya kwamba Qur’an imetungwa na Muhammad?

PIA WAPO WALIOJARIBU KUFANANISHA MANENO HAYA NA MASHAIRI
Sasa nakwenda kwenye uwezekano kwamba kitabu hiki sio kazi ya mtu mmoja, bali watu wengi Waarabu kama inavyofahamika vyema, Waarabu walikuwa na mapenzi ya asili ya kupenda ushairi na


Rejea:   “Ewe Nabii; mbona unaharamisha alichokuhalalishia Mwenye-Enzi-Mungu? 
Unatafuta radhi ya wake zako, na Mwenye-Enzi-Mungu ni mwingi wa kusamehe, mwenye kurehemu”
                                                                                    (Tahriim 66:1)

fasihi ya ufasaha wa kuzungumza.  Hafla na matamasha ya mara kwa mara yaliyofanyika, ambapo washairi na wasemaji wao walishindana katika medani ya vita, walitiwa ujasiri wa ajabu uliotokana na ufasaha wa tenzi na hotuba zilizosifu makabila yao na kuwamiminia dharau maadui na kuwavunja nguvu.

Sasa, miujiza iliyofanywa na Mitume wa Mungu ni matukio yaliyokuwa na kikomo cha muda na mahali, na yalikuwa na faida kwa wale waliokuwa mahali hapo na kuyashuhudia.  Na miongoni mwa mambo yaliyokubalika katika miujiza aliyopewa Musa (A.S) ilikuwa ni ya namna ya uchawi, kwa kuwa uchawi ulikuwa ukifanywa sana zama hizo.  Hivyo Musa aliweza kuwashinda wachawi wa zama zake, na hivyo kuweza kufikisha ujumbe.

Vivyo hivyo, miujiza iliyofanywa na Yesu ‘Masih – Issa’ ilikuwa katika mazingira ya tiba, hivyo changamoto iliyokuwa ikimkabili ni kuwashinda matabibu wa zama hizo.

Vile vile, Qur’an ni tukio la kimiujiza lililoteremshwa kwa watu waliokuwa na desturi ya kujivunia uwezo wao katika medani ya fasihi, lakini ambao walitakiwa kuzidiwa katika medani waliyoichagua wenyewe.  Sasa basi, iliwezekanaje Qur’an iwe ni kazi ya Waarabu?  Hususani pale kitabu hiki kinapowapa changamoto ya kweli walete mfano wake kwa kutunga sura moja au hata Aya moja inayolingana nayo.  Lau kama Waarabu wangekuwa na uwezo wa kuandika Qur’an yao wenyewe, wasingesita kufanya hivyo ili kulinda ibada ya masanamu ambayo imekanushwa na kushutumiwa ndani ya Qur’an.  Hakuna shaka hata kidogo kuwa Qur’an haikutoka kwa Waarabu kwa sababu wao wenyewe walistaabishwa na mtindo, ufasaha na sheria yake iliyoitangaza rasmi,  kiasi ambacho walisalimu amri mbele yake na kuingia katika dini ya Mwenye-Enzi-Mungu.  Walifanya hivyo kwa sababu wao wenyewe hawakuwa na uwezo wa kuiga mfano wa Qur’an.

Hivyo changamoto iliyotolewa ndani ya Qur’an ni ya milele, hali ya kushindwa kufunga Qur’an ni ushahidi tosha kuwa Qur’an haiwezi kuwa imetungwa na Waarabu ambao ni wanadamu kama sisi.

Inafurahisha kusikia kuna wengine wanahisi imetokana na chanzo kisichojulikana.  Ikiwa Waarabu ni wazungumzaji wa asili wa lugha hii, hawakuwa na uwezo wa kujibu changamoto nilizozieleza, je inaingia akilini hata kidogo kudhani kuwa Qur’an iliandikwa na  watu wengine wenye lugha tofauti na hii ambao walikuwa hawajui Kiarabu?  Je itakuwa imetungwa na Wafursi (Waajemi), Warumi, Wahabeshi?  Kama haikutokea kwa Waarabu, wala majirani zao, ingetokea wapi?  Kama Waarabu walikaa kimya bila shaka, itakuwa imetoka kwa chanzo kilicho juu zaidi.

            “Na ikiwa mnashaka kwa hayo tuliyomteremshia Mja wetu, basi leteni sura
iliyo mfano wa hii, na muwaite wasaidizi wenu badala ya Mwenye-Enzi-
Mungu, ikwa mnasema kweli.  Lakini kama hamtafanya basi, uogopeni Moto ambao kuni
zake ni watu na mawe, ulioandaliwa kwa makafiri”.
                                                                                                                        (2:23 – 24)

            “Sema:  Hata wakijikusanya watu wote na majini wote ili kuleta mfano wa
hii Qur’an hawataweza kuleta mfano wake hata kama watasaidiana wao
kwa wao”
                                                                                                            (17:88)

katika kitabu chake kiitwacho “The Inimitability of the Qur’an”  Al-Rafeie anasema:-



          “Wakati huo, Waarabu hawakuweza kukabiliana na changamoto ya Qur’an
kwa ufasaha waliokuwa wakijivunia.  Kwa miaka mingi changamoto hii imeendelea  kuwaita kwenye ushindani wasemaji wote wazuri na watu wenye ufasaha, na hivyo kutoacha nafasi ya ukosoaji kudai kwamba ya wanadamu na kinachopita vipawa vya ubunifu wao?”

          Wewe ni mwakilishi wa akili na fikra, hivyo wewe
ndiye unayestahiki zaidi kuhukumu.  Hoja juu ya upekee wa kitabu hiki dondoo za kila aina, ufasaha wa matamshi, kutokuwa na hali ya kutofautiana au makosa, wingi wa maana, utabiri na miujiza, mfumo wa sheria uliokusanya kila kitu na uliokamilika  …. Haya yote yametoka wapi?



                       Harakati Zangu Katika Uchambuzi Wa Mada Kuhusu Qur an na Miujiza Yake

UHURU WA MTU BINAFSI NNI JAMBO LA LAZIMA KATIKA DEMOKRASIA




Kuna mambo ni ya lazima katika demokrasia, ukiyakosa hayo demokrasia hakuna.
 La kwanza ni kwamba kila mtu lazima aweze kusema hisia zake kwa uhuru kabisa, na maneno ya kila mtu lazima yasikilizwe. Hata kama mawazo ya mtu huyu hayapendwi kiasi gani, au walio wengi wanamdhania anapotoka kiasi gani, siki tu. Kama mtu anapendwa kwa wema wake, au hapendwi kwa visa vyake, hayo yote si kitu. Kila mtanzania, kila mtu kijijini, kila mjumbe wa Halmashauri ya wilaya, kila mbunge, n.k., lazima aweze kusema kwa uhuru bila hofu ya vitisho, iwe katik amkutano iwe nje ya mkutano.
Watu wenye mawazo tofauti hata wakiwa wachache, lazima wawe na haki ya kutoa mawazo yao katika majadiliano bila hofu ya kusumbuliwa, mawazo yao yaje kushindwa katika hoja za majadiliano, siyo yashindwe kwa vitisho au mabavu.Majadiliano yenyewe yatakayoleta uamuzi lazima yawape nafasi watu kusema kwa uhuru kabisa. Na hata baada ya kuamua jambo watu wawe na uhuru kuendelea kulizungumzia jambo hilo. Maana wale wachache wenye mawazo tofauti lazima wafahamu kuwa kama wanayo mawazo yenye maana, na kama wakiyaeleza mawazo hayo vizuri, wanaweza kubadili mawazo ya wale wengine walio wengi. Kadhalika wale walio wengi lazima wawe tayari kuyashikilia mawazo yao mpaka wale wachache waridhike kuwa uamuzi uliofanywa juu ya jambo hilo ulikuwa sawa. Majadiliano lazima yaruhusiwe kuendelea, kwa uhuru kabisa. NA HIYO NI SEHEMU YA MAANA YA UHURU WA MTU BINAFSI.

Thursday, May 15, 2014

MANENO YA KWELI YASIYO NA CHEMBE YA SHAKA NDANI YAKE - 4




CHANZO CHA QUR'AN

          “Je, wanasema ameitunga? Sema:          Basi leteni sura moja mfano wake
na muwaite muwezao wasaidie asiyekuwa Mwenye-Enzi-Mungu ikiwa
nyinyi mnasema kweli”.
                                                          (Yunus 10:38)

Kabla hatujaangazia Chanzo kikuu cha Qur’an ni vema tukaangalia hoja mbalimbali za makafiri na washirikina kuhusiana na chanzo cha Qur’an


MATWAGHUTI WANADAI QUR’AN IMETUNGWA NA MUHAMMAD,
HILI LINAWEZA KUKANUSHWA KWA KUTUMIA VIGEZO VINANE VIFUATAVYO:-


                   (1)     Suala la mtindo, kama kila mmoja ajuavyo kuna tofauti
kubwa sana kati ya mtindo wa maneno ya Qur’an na mtindo
wa maneno ya Muhammad (S.A.W) mwenyewe. 
Ukilinganisha maneno ya Muhammad yaliyokusanywa katika
                             Vitabu vya hadithi pamoja na Qur’an, tofauti katika hali zote
mtindo, somo huonekana dhahili. Maneno ya Muhammad ni
aina ya mazungumzo, maelezo ya kina, ya kuadilisha na
fasaha ambayo tayari yalikuwa yamezoeleka kwa Waarabu. 
Kinyume na muundo wa Qur’an ambao haukuwa ukijulikana
kwa Waarabu, ulikuwa unakosoa kila ovu na kuweka sheria
ya mambo mbali mbali.

Rejea:   The Reader’s Companion to World Literature, Hornstein, Persy, Brown,
ukurasa 298 “Mohammed au Muhammad, kiongozi wa dini na mtunzi wa Qur’an”.

                   (2)     Taathira inayotokea kwa msomaji.  Kwa kusoma vitabu vya
hadithi, mtu hujihisi kuwa yuko mbele ya mwanadamu.
Tofauti iliyoje wakati wa kusoma Qur’an, msomaji huona kuwa yupo mbele ya Mungu, muumba wa vitabu vyote, mwenye nguvu, haki, hekima na rehma ambayo haina hata chembe ya udhaifu ndani yake, hata mahali rehma inapoonekana.  Kama Qur’an ingekuwa imetungwa na Muhammad, basi muundo wake
ungeafikiana na ule wa hadithi zake.  Kwani siyo jambo la kawaida katika elimu ya uandishi kuwa mtu mmoja hawezi kuwa na mitindo miwili, ambayo yote ina tofauti sana ya asili?

                   (3)     Muhammad (S.A.W) hakuwahi kusoma wala kuandika. 
Mtume hakwenda shule au kuwa na mwalimu, kamwe hakuwahi kusoma chini ya mkufunzi wa aina yoyote.  Je inaingia akilini, kufikiria kuwa mtu kama huyo angeweza kuwa na haya maandiko ya sheria ya ajabu, yenye kukubalika sana na isiyokuwa na hitilafu yoyote, ukuu wake unatambulika sana. unatambulika kwa Waislam na wasiokuwa Waislam, aidha umepitishwa kama chanzo kikuu cha sheria za ulaya?  Mtu asiyejua kuandika angewezaje kubuni Qur’an, pamoja upekee wa mtindo wake, na sheria zake za kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini?

Rejea:   “Na hukuwa mwenye kusoma kitabu chochote kabla ya hiki, wala hakuandika kwa mkono wako wa kulia”.
                                                                             (ANKABUUT 29:48)


                   (4)     Maudhui ya kielimu yaliyo ndani ya Qur’an mtazamo juu ya
ulimwengu, maisha, fikra, shughuli za kifedha, vita, ndoa, ibada, biashara na mengine yaliyomo ndani ya Qur’an ni kamili yote yanapatikana, hayatofautiani.  Kama yote haya yangetoka kwa Muhammad, isingewezekana tena kuamiliana naye kama mwanadamu.  Kwa sababu hata kundi la kamati zote, wajumbe wake wanaounda tamaduni za kimataifa pamoja na wenye elimu kubwa, wangekabiliwa na ugumu wa hali ya juu katika kutengeneza kanuni hizo za kimaadili na kisheria, bila kujali ni kazi ngapi za rejea na uchunguzi wa kitaalamu na ugunduzi wa kitafiti ambao ungewekwa katika mamlaka yao, bila kujali urefu gani wa muda.  Hakuna mtu yeyote, mwenye kipaji cha aina gani na elimu pana kiasi gani, ambaye angeweza kutunga masuluhisho ya tatizo lolote miongoni mwa matatizo yanayomkabili mwanadamu, sasa tutasema nini tutakapofikiria utata wake, tofauti zake nyingi?  Ingewezekanaje kwa mtu asiyesoma awe ndiye mwanzilishi wa yote haya?

                   (5)     Suala la ufahari binafsi wa mtunzi sababu gani ambayo
ingemfanya Muhammad (S.A.W) aandike Qur’an kisha
akaihusisha na mtunzi mwingine?  Sifa hii ingekuwa kubwa sana kama angekuwa ametengeneza kazi yake mwenyewe ili kuushangaza ulimwengu mzima kwa kitu ambacho wao binafsi hawakuwa na uwezo hata kidogo wa kukitengeneza.  Jambo hili lingemwinua kwenye daraja ya juu zaidi ya wanadamu wengine.  Faida au manufaa gani ambayo Muhammad (S.A.W) angeyapata kwa kutunga Qur’an lakini akawapa sifa wengine?

Endelea Kufatilia mada hii adhimu itakayoendelea hapahapa…………………………………………………..

UMUHIMU WA TENDO LA NDOA KIAFYA



đź’•Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili.
Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.

đź’•Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.Kuongeza mwendo wa damu

đź’•Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji.

đź’•Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.

đź’•Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.

đź’•Kupunguza maumivuWakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa.

đź’•Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini.

đź’•Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara.

đź’•Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.

đź’•Kupunguza mfadhaiko wa moyo

đź’•Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini.

đź’•Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

đź’•Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen).

đź’•Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi.

đź’•Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.

đź’•Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijanaWakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka.

đź’•Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular).

đź’•Hupunguza baridi na mafua

đź’•Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa.

Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.

Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa.

Ndiyo maana nikasema ni maalum kwa wanandoa tu