(6) Mambo ya kweli yaliyomo ndani ya
Qur’an. Ndani ya Qur’an
kuna
ukweli mbalimbali kuhusu mambo ya kale ambayo hayakuwa yakijulikana kwa watu wa
rika na zama za Muhammad (S.A.W). Katika
Aya mbalimbali tunakuta rejea ya maajabu ya kisayansi yanayohusu ulimwengu na
uhai, madawa, hisabati (mahesabu). Je
mtu asiyesoma angeweza kuhusika na utambuzi wa mambo hayo ya kielimu? Muhammad angewezaje kusema kuwa dunia ipo
katika muundo wa yai?
Angewezaje
kuijua nadharia ya upanukaji wa ulimwengu?
Angewezaje kusema kuwa element za maAda inayounda ulimwengu zote ni za
aina moja? Kwamba msongamano wa hewa huongezeka kadiri mtu aendavyo juu na
hivyo kupumua huwa tabu(1), na jinsi jua na mwezi vinavyoelea angani(2)? Qur’an imejaa mifano kama hiyo. Muhammad asiyesoma aliwezaje kujua mambo ya
kisayansi ambayo yamekuja kujulikana hivi karibuni tu kwa msaada wa maabara na
satelait za kisasa?
Rejea Surat Naazia’at 79:30, Dhariyaat 51:47na Anbiyaa
21:30)
(7) Makemeo kwa Muhammad. kuna Aya nyingi za
Qur’an,
Mtume amekemewa. Sura iitwayo “Abasa”
yaweza kuwa mfano unaojulikana vyema:-
“Alikunja
uso na akageuza mgongo. Kwa sababu
alimjia kipofu” .
Siku
moja kipofu mmoja aliyeitwa Abdullah Ibn Umm Maktum, alimkatiza Muhammad
(S.A.W) wakati akizungumza na Walid na wakubwa wengine wa Kikuraishi. Mtume akionesha kutomtambua kipofu huyo
aliinua sauti yake kwa ari na kuomba maelekezo ya kidini, lakini Muhammad
akiudhika na uingiliaji kati huo, alikunja uso na kugeuza mgongo. Aya hiyo ni lawama kwa Mtume kwa kitendo
chake kwenye tukio hilo. Udhaifu ni sifa za mwanadamu.
Vile
vile kuna idadi ya mifano mingine kama hiyo ndani ya Qur’an. Je inaingia akilini kufikiri kuwa Muhammad
ndiye aliyetunga kitabu ambacho ndani yake amekemewa?
Wala
usiseme kabisa juu ya jambo lolote.
Hakika mimi
nitalifanya
kesho, isipokuwa Mungu akipenda yeye mtunzi mwenyewe analaumiwa? Kuna matukio mengi ambapo Muhammad (S.A.W)
aliweka katika namna fulani, lakini Qur’an kwa uwazi kabisa huilaumu tabia yake
ya kuonesha kosa alilotenda. Muhammad
hakujisikia vibaya kunukuu matukio hayo kama angekuwa ndiye mtunzi wa Qur’an je
asingebadilisha rekodi hizo kwa kuzifuta au kwa kuzirekebisha ili kuakisi
mapendeleo yake mwenyewe?
(8) Kipindi cha muda baina ya tamaa ya Muhammad
ya kuongea
na
ufunuo uliokuwa ukimfikia. Wakati fulani
Muhammad (S.A.W) alihisi udharura wa kuzungumzia mambo fulani au kutoa
maelekezo kuhusu namna ya kuyatenda.
Lakini bado alisubiri usiku na mchana mpaka agizo limfikie kabla ya
kufanya vitu hivyo kujulikana kwa watu wengine.
HEBU TUJIULIZE?
Kitabu
kilichotengezwa na binadamu kiliwezaje
kutangaza
umoja wa Mungu katika mtindo na mfumo wa uadilishaji ambao haukupatikana katika
maandiko matakatifu yaliyotangulia?
Je
akili yenye busara na nguvu haitoshi kupinga moja kwa moja hoja ya kwamba
Qur’an imetungwa na Muhammad?
PIA WAPO WALIOJARIBU KUFANANISHA MANENO
HAYA NA MASHAIRI
Sasa nakwenda kwenye uwezekano kwamba
kitabu hiki sio kazi ya mtu mmoja, bali watu wengi Waarabu kama inavyofahamika
vyema, Waarabu walikuwa na mapenzi ya asili ya kupenda ushairi na
Rejea: “Ewe Nabii; mbona unaharamisha
alichokuhalalishia Mwenye-Enzi-Mungu?
Unatafuta
radhi ya wake zako, na Mwenye-Enzi-Mungu ni mwingi wa kusamehe, mwenye kurehemu”
(Tahriim 66:1)
fasihi ya ufasaha wa kuzungumza. Hafla na matamasha ya mara kwa mara
yaliyofanyika, ambapo washairi na wasemaji wao walishindana katika medani ya
vita, walitiwa ujasiri wa ajabu uliotokana na ufasaha wa tenzi na hotuba zilizosifu
makabila yao na kuwamiminia dharau maadui na kuwavunja nguvu.
Sasa, miujiza iliyofanywa na Mitume wa
Mungu ni matukio yaliyokuwa na kikomo cha muda na mahali, na yalikuwa na faida
kwa wale waliokuwa mahali hapo na kuyashuhudia.
Na miongoni mwa mambo yaliyokubalika katika miujiza aliyopewa Musa (A.S)
ilikuwa ni ya namna ya uchawi, kwa kuwa uchawi ulikuwa ukifanywa sana zama
hizo. Hivyo Musa aliweza kuwashinda
wachawi wa zama zake, na hivyo kuweza kufikisha ujumbe.
Vivyo hivyo, miujiza iliyofanywa na
Yesu ‘Masih – Issa’ ilikuwa katika mazingira ya tiba, hivyo changamoto
iliyokuwa ikimkabili ni kuwashinda matabibu wa zama hizo.
Vile vile, Qur’an ni tukio la kimiujiza
lililoteremshwa kwa watu waliokuwa na desturi ya kujivunia uwezo wao katika
medani ya fasihi, lakini ambao walitakiwa kuzidiwa katika medani waliyoichagua
wenyewe. Sasa basi, iliwezekanaje Qur’an
iwe ni kazi ya Waarabu? Hususani pale
kitabu hiki kinapowapa changamoto ya kweli walete mfano wake kwa kutunga sura
moja au hata Aya moja inayolingana nayo.
Lau kama Waarabu wangekuwa na uwezo wa kuandika Qur’an yao wenyewe,
wasingesita kufanya hivyo ili kulinda ibada ya masanamu ambayo imekanushwa na
kushutumiwa ndani ya Qur’an. Hakuna
shaka hata kidogo kuwa Qur’an haikutoka kwa Waarabu kwa sababu wao wenyewe
walistaabishwa na mtindo, ufasaha na sheria yake iliyoitangaza rasmi, kiasi ambacho walisalimu amri mbele yake na
kuingia katika dini ya Mwenye-Enzi-Mungu.
Walifanya hivyo kwa sababu wao wenyewe hawakuwa na uwezo wa kuiga mfano
wa Qur’an.
Hivyo changamoto iliyotolewa ndani ya
Qur’an ni ya milele, hali ya kushindwa kufunga Qur’an ni ushahidi tosha kuwa
Qur’an haiwezi kuwa imetungwa na Waarabu ambao ni wanadamu kama sisi.
Inafurahisha kusikia kuna wengine
wanahisi imetokana na chanzo kisichojulikana.
Ikiwa Waarabu ni wazungumzaji wa asili wa lugha hii, hawakuwa na uwezo
wa kujibu changamoto nilizozieleza, je inaingia akilini hata kidogo kudhani
kuwa Qur’an iliandikwa na watu wengine
wenye lugha tofauti na hii ambao walikuwa hawajui Kiarabu? Je itakuwa imetungwa na Wafursi (Waajemi),
Warumi, Wahabeshi? Kama haikutokea kwa
Waarabu, wala majirani zao, ingetokea wapi?
Kama Waarabu walikaa kimya bila shaka, itakuwa imetoka kwa chanzo
kilicho juu zaidi.
“Na ikiwa mnashaka kwa hayo
tuliyomteremshia Mja wetu, basi leteni sura
iliyo
mfano wa hii, na muwaite wasaidizi wenu badala ya Mwenye-Enzi-
Mungu,
ikwa mnasema kweli. Lakini kama
hamtafanya basi, uogopeni Moto ambao kuni
zake
ni watu na mawe, ulioandaliwa kwa makafiri”.
(2:23 – 24)
“Sema: Hata wakijikusanya watu wote na majini wote
ili kuleta mfano wa
hii
Qur’an hawataweza kuleta mfano wake hata kama watasaidiana wao
kwa
wao”
(17:88)
katika kitabu chake kiitwacho “The
Inimitability of the Qur’an” Al-Rafeie
anasema:-
“Wakati
huo, Waarabu hawakuweza kukabiliana na changamoto ya Qur’an
kwa
ufasaha waliokuwa wakijivunia. Kwa miaka
mingi changamoto hii imeendelea kuwaita
kwenye ushindani wasemaji wote wazuri na watu wenye ufasaha, na hivyo kutoacha
nafasi ya ukosoaji kudai kwamba ya wanadamu na kinachopita vipawa vya ubunifu
wao?”
Wewe ni
mwakilishi wa akili na fikra, hivyo wewe
ndiye
unayestahiki zaidi kuhukumu. Hoja juu ya
upekee wa kitabu hiki dondoo za kila aina, ufasaha wa matamshi, kutokuwa na
hali ya kutofautiana au makosa, wingi wa maana, utabiri na miujiza, mfumo wa
sheria uliokusanya kila kitu na uliokamilika
…. Haya yote yametoka wapi?
Harakati Zangu Katika Uchambuzi Wa Mada Kuhusu Qur an na Miujiza Yake
No comments:
Post a Comment