Monday, May 21, 2012

Lengo Na Hadhi Ya Mwanadamu Hapa Ulimwenguni.

Lengo la maisha
lengo la kuumbwa binadamu ni kumuabudu Allah(s.w).
"sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu"(51:56)


Maana ya ibada kwa mnasaba wa lengo:
"ibada"ni neno la kiarabu linlotokana na neno abd,lenye maana ya mtumwa au mtumishi. km abdillah=mtumishi(mtumwa)wa Allah.

kisheria,kumuabudu Allah ni kumtii Allah kwa unyenyekevu.
kumuabudu Allah s.w kama lengo la maisha ni kumtiiallah s.w kwa unyenyekevu katika kukiendea kila kipengele cha maisha ya kila siku ya kibinfsi na kijamii.
wanaotambua lengo hili na kuishi kwalo ndio binaadam wenye akili kama inavyoainishwa katika Qur'an.

katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana ,ziko hoja(za uwepo wa mungu mmoja), kwa wenye akili.ambao humkumbuka mwenyezi mungu wakiwa wima na wakikaa na wakilala.na hufikiri umbo la mbingu na ardhi(wakasema)"mola wetu hukuviumba hivi bure.utukufu ni wako.basi tuepushe na adhabu ya moto".


Mtazamo potofu juu ya ibada
wengi wa waislamu wamelifanya lengo la kuumbwa binadamu kwenye kutenda matendo machache ya kibinfsi kama vile kuswali,kufunga,kutoa zakat na sadaqat,kuhiji na kufanya sunnah zinazoambatana na ibada hizi maalum.
inamkininika kweli Allah s.w mjuzi mwenye hekima atangaze kuwa "hakumuumba mtu ila kwa lengo la kumuabudu tu",kisha kuwe ni kwa sehemu ndogo sana ya umri wake anaoishi hapa duniani?

-Ili kudhihirisha kwa uwazi mshangao huu hebu tuone,kama mfano muda tunaochukua kutekeleza nguzo nne za uislamu,ukiacha shahada ambayo wengi kwa mtazamo huu mpotofu wanaamini inaishia kwenye matamshi tu.

(1) Swala tano;
-jaalia kila swala inagharimu dakika 20.
-dakika 20 x5=dakika 100.
-hivyo katika saa 24(dakika 60 x 24)=dk 1440)
-100/1440=0.069=0.07asilimia 7(7%)kuabudu na asilimia 93(93%)iko nje ya ibada ya swala.

(2) Zakat
-kiwango cha zakat ni asilimia 2.5 ya mali ya tajiri kwa mwaka ndiyo inayotumika katika kumuabudu Allah(s,w),na aslimia 97.5 iko nje ya ibada.

(3) Swaum
-katika miezi kumi na mbili ya mwaka tunafunga mwezi mmoja,lakini hatufungi saa 24,bali kwa urefu,hasa nyakati za kiangazi(katika nchi za joto-tropical)tunaweza kufunga saa 14 kwa siku.
-hivyo kwa mwezi tunafunga saa 14 x 30 = saa 420.
-hivyo asilimia ya muda tunaoabudu katika funga ya ramadhan katika mwaka ni (420/360 x 24 = 0.048 = 0.05)asilimia 5 na asilimia 95 iko nje ya ibada ya funga.

(4) Hija
-ibada hii inafanywa mara moja katika umri wa mtu kwa wale wenye uwezo.
-jaalia mtu aliyeishi miaka 100,anahiji mara moja,na tjaalie alitumia mwezi mmoja katika kutekeleza ibada hiyo.
-hivyo aslimia ya umri wake aliyoitumia kufanya ibada hiyo ya hija(siku 30/siku 360 x 100 = 0.0008=0) inakaribia aslimia 0 na sehemu ya umri wake aliyoitumia nje ya ibada hii ni 99.9992% =100%

.kwa mifano hii wastani wa muda amba muumini anamuabudu Allah kwa kutekeleza kwa ukamilifu nguzo tano za uislamu ni {0% +7% +2.5% + 5% + 0% / 5 =2.9% = 3%} asilimia tatu na aslimia 987 iko nje ya ibada.

Tanbihi:
nguzo ya shahada imepewa aslimia sifuri kwa kuwa kutamka shahada ni kitendo kinachokamilika kwa sekunde chache.

haiyumkiniki Allah atangaze kuwa amemleta binaadamu hapa duniani ili tu amuabudu,kuabudu kwenyewe kuwe asilimia tatu tu.

kwa mifano hii utaona kuwa lengo la kuumbwa binaadamu halitafikiwa kwa kutekeleza tu nguzo tano za uislamu na sunnah zilizoambatanishwa nazo,bali litafikiwa kwa kumuabudu Allah saa 24,kama anavyotuamrisha katika qur'an.

"enyi mlioamini! ingieni katika hukumu za uislamu zote,wala msifuate nyayo za shetani:kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri(2:208)

"Enyi mlioamini mcheni Allah kama ipasavyo kumcha wala msife isipokuwa mmekua wakamili.(3.102)

No comments:

Post a Comment