Thursday, May 15, 2014

MANENO YA KWELI YASIYO NA CHEMBE YA SHAKA NDANI YAKE - 4




CHANZO CHA QUR'AN

          “Je, wanasema ameitunga? Sema:          Basi leteni sura moja mfano wake
na muwaite muwezao wasaidie asiyekuwa Mwenye-Enzi-Mungu ikiwa
nyinyi mnasema kweli”.
                                                          (Yunus 10:38)

Kabla hatujaangazia Chanzo kikuu cha Qur’an ni vema tukaangalia hoja mbalimbali za makafiri na washirikina kuhusiana na chanzo cha Qur’an


MATWAGHUTI WANADAI QUR’AN IMETUNGWA NA MUHAMMAD,
HILI LINAWEZA KUKANUSHWA KWA KUTUMIA VIGEZO VINANE VIFUATAVYO:-


                   (1)     Suala la mtindo, kama kila mmoja ajuavyo kuna tofauti
kubwa sana kati ya mtindo wa maneno ya Qur’an na mtindo
wa maneno ya Muhammad (S.A.W) mwenyewe. 
Ukilinganisha maneno ya Muhammad yaliyokusanywa katika
                             Vitabu vya hadithi pamoja na Qur’an, tofauti katika hali zote
mtindo, somo huonekana dhahili. Maneno ya Muhammad ni
aina ya mazungumzo, maelezo ya kina, ya kuadilisha na
fasaha ambayo tayari yalikuwa yamezoeleka kwa Waarabu. 
Kinyume na muundo wa Qur’an ambao haukuwa ukijulikana
kwa Waarabu, ulikuwa unakosoa kila ovu na kuweka sheria
ya mambo mbali mbali.

Rejea:   The Reader’s Companion to World Literature, Hornstein, Persy, Brown,
ukurasa 298 “Mohammed au Muhammad, kiongozi wa dini na mtunzi wa Qur’an”.

                   (2)     Taathira inayotokea kwa msomaji.  Kwa kusoma vitabu vya
hadithi, mtu hujihisi kuwa yuko mbele ya mwanadamu.
Tofauti iliyoje wakati wa kusoma Qur’an, msomaji huona kuwa yupo mbele ya Mungu, muumba wa vitabu vyote, mwenye nguvu, haki, hekima na rehma ambayo haina hata chembe ya udhaifu ndani yake, hata mahali rehma inapoonekana.  Kama Qur’an ingekuwa imetungwa na Muhammad, basi muundo wake
ungeafikiana na ule wa hadithi zake.  Kwani siyo jambo la kawaida katika elimu ya uandishi kuwa mtu mmoja hawezi kuwa na mitindo miwili, ambayo yote ina tofauti sana ya asili?

                   (3)     Muhammad (S.A.W) hakuwahi kusoma wala kuandika. 
Mtume hakwenda shule au kuwa na mwalimu, kamwe hakuwahi kusoma chini ya mkufunzi wa aina yoyote.  Je inaingia akilini, kufikiria kuwa mtu kama huyo angeweza kuwa na haya maandiko ya sheria ya ajabu, yenye kukubalika sana na isiyokuwa na hitilafu yoyote, ukuu wake unatambulika sana. unatambulika kwa Waislam na wasiokuwa Waislam, aidha umepitishwa kama chanzo kikuu cha sheria za ulaya?  Mtu asiyejua kuandika angewezaje kubuni Qur’an, pamoja upekee wa mtindo wake, na sheria zake za kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini?

Rejea:   “Na hukuwa mwenye kusoma kitabu chochote kabla ya hiki, wala hakuandika kwa mkono wako wa kulia”.
                                                                             (ANKABUUT 29:48)


                   (4)     Maudhui ya kielimu yaliyo ndani ya Qur’an mtazamo juu ya
ulimwengu, maisha, fikra, shughuli za kifedha, vita, ndoa, ibada, biashara na mengine yaliyomo ndani ya Qur’an ni kamili yote yanapatikana, hayatofautiani.  Kama yote haya yangetoka kwa Muhammad, isingewezekana tena kuamiliana naye kama mwanadamu.  Kwa sababu hata kundi la kamati zote, wajumbe wake wanaounda tamaduni za kimataifa pamoja na wenye elimu kubwa, wangekabiliwa na ugumu wa hali ya juu katika kutengeneza kanuni hizo za kimaadili na kisheria, bila kujali ni kazi ngapi za rejea na uchunguzi wa kitaalamu na ugunduzi wa kitafiti ambao ungewekwa katika mamlaka yao, bila kujali urefu gani wa muda.  Hakuna mtu yeyote, mwenye kipaji cha aina gani na elimu pana kiasi gani, ambaye angeweza kutunga masuluhisho ya tatizo lolote miongoni mwa matatizo yanayomkabili mwanadamu, sasa tutasema nini tutakapofikiria utata wake, tofauti zake nyingi?  Ingewezekanaje kwa mtu asiyesoma awe ndiye mwanzilishi wa yote haya?

                   (5)     Suala la ufahari binafsi wa mtunzi sababu gani ambayo
ingemfanya Muhammad (S.A.W) aandike Qur’an kisha
akaihusisha na mtunzi mwingine?  Sifa hii ingekuwa kubwa sana kama angekuwa ametengeneza kazi yake mwenyewe ili kuushangaza ulimwengu mzima kwa kitu ambacho wao binafsi hawakuwa na uwezo hata kidogo wa kukitengeneza.  Jambo hili lingemwinua kwenye daraja ya juu zaidi ya wanadamu wengine.  Faida au manufaa gani ambayo Muhammad (S.A.W) angeyapata kwa kutunga Qur’an lakini akawapa sifa wengine?

Endelea Kufatilia mada hii adhimu itakayoendelea hapahapa…………………………………………………..

No comments:

Post a Comment