Saturday, April 21, 2012

Ni Lazima Mwanadamu Awe Na Mwenza Ndipo Atulie Katika Maisha

Swali–Tunalazimika kuanza kwakuuliza: 


Hivi wanadamu wanatakiwa kuishi kijamii na kuanza familia kwa ujumlal?
Hivi hawawezi kuishi peke yao?

Kuwa peke ni jambo la kweli kwa Mwenyezi Mungu pekee. Muumbaji ameweka upweke kuwa ni wakwake pekee, Kisha akaumba viumbe vyote vilivyopo katika jozi. Hivyo viumbe wote wana hitajio kubwa la kuhitajiana wenyewe kwa wenyewe kwa wakati mmoja, Tangia wao wameumbwa, wana mapungufu ya asili na madhaifu katika uhalisia wao.Ma siwa Allah, “wasiokuwa mwenyezi Mungu” -viumbe wote isipokuwa Mwenyezi mungu mtukufu-daima huhitajiana wenyewe kwa wenyewe na humuhitajia Mwenyezi Mungu mtukufu.
Ukiondoa kuumbwa, wanadamu wanahitajiana sana wenyewe kwa wenyewe. Watu wana mahitaji na vipaumbele vingi sana, ukilinganisha na viumbe wengine!Kwa kuwa watu siku zote hutaka kuishi katika vifaa na faraja ya kiroho, mahitajio yao kawaida huongezeka na katu hayawezi kufikia mwisho. Matatizo, ukata, maumivu, mateso na huzuni vyote hutukutanisha na ugumu. Katika nyakati za shida, tunaitizama roho ipumzike na mkono usubirie.
Hivyo kizazi cha Adam kimeoneshwa kwa neno la kiarabu lijulikanalo kama insan, amabalo limetoholewa toka katika neno uns au unsiyya,lenye kumaanisha urafiki. Hata Falsafa inaonesha mahitaji yetu kuwa karibu ya urafiki! Mahitajio haya ndio ubora wetu wa kwanza na mwanadamu anatofautishwa kwa ubora huu.
Ufunuo sahihi wa urafiki ni umoja ambao unaunganisha mwanaume na mwanamke. Jambo hili ni muhimu sana, hata utii, kwa uendeleaji wa kizazi cha mwanadamu.
Umuhimu wa umoja hujifunua wenyewe katika viumbe hai kupitia uwepo wa mwanaume na mwanamke na viumbe visivyo na uhai kupitia uwepo wa ncha chanya na hasi. Hali hii imeelezwa ndani ya Qur’an katika aya nyingi sana.
“Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie .”(Adhdhaariyaat 51: 49)
“Subhana, Ametakasika, aliye umba dume na jike vyote katika vinavyo mea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyo vijua.”(Yasin 36:36)
“Na tukakuumbeni kwa jozi(Annabaa 78: 8)
Kumiliki asili ya kuumbwa katika jozi humaanisha kuumbwa mwanaume na mwanamke,nyongeza,si katika miwili ya aina moja. Katika hali hiyo, uumbaji wa moja ya wawili ungepunguzwa na hilo halipo kwa Mwenyezi mungu. Kwahiyo Mwenyezi mungu ameumba viumbe katika jinsia za wanandoa.Hivyo kila kiumbe kilichoumbwa kina upekee wa chenyewe. Mwenyezi Mungu hakuumba kiumbe kinachochanganya, amacho hakitofautiani na kingine. Hata mapacha wana tofauti nyingi za kimaumbile na kiroho.
Hivyo Mwenyezi Mungu mtukufu ameumba kila kiumbe katika jozi zenye kusaidiana nawakati huo huo sheria yake ya uungu ya mvutano kati yao ili kuwafanya wawe karibu karibu mno. Kisha akaweka maendeleo ya kiumbo na kiroho ya kwa jozı zote mbili kwa muungano unaowezekana baına yao.
Ingawa mahıtajı ya mvutano mwanaume humfikiria mwanamke na mwanamke humfikiria mwanaume kimsingi hili huendeleza kizazi, Hili si lengo lao pekee. Moja ya majukumu yao muhimu ni ni kutengeneza misingi ya familia iliyo bora, ambayo hutengeneza mazingira yanayoruhusu mtu binafsi kupata usawa wa amani ya kiroho na kijamii.Kusudio hili linaweza kufikiwa tu kupitia mahabbat Allah,Moyo kupendelea kuweka upendo wa Mwenyezi mungu mtukufu.
Baadhi ya nyakati upendo kwa Mwenyezi Mungu hutokana na upendo wa duniani: Mpenzi husimama usiku akimuelekea Mawla (Bwana mlezı-kutokana na upendo wa Mungu). Lakini kuwezekana kwa safari hii, Nı kuweza kuwa Leıla kwa sehemu ya kwanza! Kisha upendo kati ya mwanaume na mwanamke unaweza kuanzisha hatua ya kwanza ya kuwa karibu na mwenyezı mungu. Ingawa mvutano huo huanza na tamaa za kibinafsi, Haiwezi kuelekea katika upendo wa kweli wa kibinadamu hadi ıwe huru kuepukana na hizo tamaa za kibinafsi. Wakati tabia za kuheshimiana zitakapojikita kwa wapenzi, ni hapo tu ndipo tunapoweza kuita mvutano, Upendo.
Moyo, Abao ndio kituo kikuu cha mvutano, umejaribiwa na kutahiniwa nguvu yake kupitia makundi tofauti ya upendo wa huyu na yule na kupata uwezo wa kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu. Uwezo wa kupata upendo wa Mwenyezi Mungu ni hatua ya juu kabisa ya mandeleo kupitia upendo kwa mtoto wa mmoja wetu, tunda la asili la familia.
Ili uwe umezungukwa na upendo kwa Mwenyezi Mungu, Ndoa ni lazima ipatikane kupitia kanuni za Muumba. Ndoa itakayofanyika kutokana na tamaa za kimwili sıku zote huwa hazıtengenezi upendo. Maendeleo ya kiroho na mafunzo ya moyo kupitia upendo ambayo yanaweza kutarajıwa kutoka katika ndoa ya kiisilamu haıwezi kukubalika katika familia za kiislamu kuanzishwa na tamaa,kwa kuwa katika aina hiyo ya ndoa wanandoa hua watumwa. Sahau maendeleo ya kiroho: wanandoa wanaweza hata kufikia kupoteza viwango vya kiroho walivyovifikia kabla hawajawa wanandoa yaani walipokuwa peke.
Ndoa inayohitajika ni ile inayotupelekea kufikia maendeleo wa kiroho. Uhusiano wa kindoa wa aina hiyo ambao unafanya kazi katika njia kama hiyo hupelekea ukamilifu wa kifikira. Ni aina hiyo ya ndoa ambayo huitwa, katıka Sunnah za Mtume (s.a.w), “nusu ya dini.”Kupata nusu ya jambo fulani haimaanishi tukate tamaa ya kuitafuta nusu ingine iliyobakia! Tunalazimika kufanya chochote tuwezacho kuhakikisha kuwa tunapata sifa bora ya ndoa.Ni hapo tu ndipo tunapoweza kupata utulivu, amani tuliyokuwa tumeitarajia.
Ingawa moja ya malengo ya uhusiano baina ya mwanaume na mwanamke ni njia ya kufikia katika kumpenda Mwenyezi Mungu, Si njia pekee. Mtu asiye na mke anaweza kufikia hatua ya kuwa na maendeleo ya kiroho.Kuna wachamungu wengi mno waliokuwa wapweke wametajwa ndani ya Qur’an, Kuanzia na Maryam na Yesu (a.s). Hali hii inaonesha kuwa si kila mmoja ameumbwa na aina hiyo moja tu ya uwezo wa kiasili. Mazingira, vilevile, yanaleta athari tofauti kwa watu. Katika mitazamo ya baadhi ya watu njia ya kuoa imefungwa;Vizuizi vinavyozuia ndoa vinaweza kupelekea majaribu ya hali ya kiroho kwao.Kwa wengine,ndoa yaweza kuwa ni chanzo cha mateso na huzuni.Mwenyezi mungu Mtukufu ameteremsha aina fulani ya uwezo maalum juu ya wale wote waliojaribiwa na kupitia majaribu hayo wanaweza kupata masilahi ya kiroho amayo yalitarajiwa kupatikana katika ndoa ya kawaida. Baadhi ya waja wa Allah wasiokuwa katika ndoa hufanya mambo makubwa ya mafanikio ya kiroho kupitia huruma na ukarimu wao kwa wanyama na mimea. Wengine wamepitia hatua za kiroho kwa kufaulu majaribu yaliyowakuta katika ndoa zao. Maswahaba wa mtume, waliowasaidia maswahaba wa Mtume walikuwa masikini kiasi cha kukosa uwezo wa kuoa,walifikia vilele vya kiroho kupitia taaluma na kusoma. Haipaswi kusahaulika, hata hivyo, haya ni mambo maalum na yakipekee. Sheria kuu ni kwamba wanadamu ni lazima waingie katika ndoa na waanzishe familia zenye furaha.
Ni hakika kwamba moyo bila upendo ni sawa na shamba lisilopandwa kitu, lililoachwa peke kwa muda mrefu. Uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke utailima ardhi hii. Bila ya shaka, ili kuwa mshindi, aina hiyo ya uhusiano haiwezi kuelemea katika matamanio binafsi. Ushindi utapatikana tu kwa kuweza kuipuka matamanio binafsi. Kama tulivyosema, Karibu sana uhusiano wa asili utabadilisha uelekeo wake katika upendo wa mungu.Kwa haraka sana upendo wa asili unalazimika kubadilisha uelekeo wako kumuelekea Mwenyezi mungu, kwa kuwa ni pale tu muungano baina ya mwanaume na mwanamke unapopata ubora huu ndipo roho zinapoweza kuhamishia upendo wake kwa allah (s.w). Kupata watoto katika hali hii huanzisha hatua ya pili katika kufikia upendo kwa ajili ya allah (s.w). Kisha unakuja upendo kwa ndugu na jamaa wa karibu, Marafiki, waalimu na wengineo.Hivyo moyo hukuwa, hatua kwa hatua huja karibu zaidi na malengo makuu, upendo wa mungu. Baada ya kuwa mmoja na upendo wa Mungu, Mja hujumuika na marafiki wa Mwenyezi mungu mtukufu. Ambapo hili ndilo lengo la kuumbwa mwanadamu.
Kwa kifupi, Mahitaji yetu kwa jili ya kuwa na familia na muungano wetu baina ya wanaume na wanawake ni uhalisia uliosimikwa katika asili yetu na muumba wetu ambae anajivunia mambo hayo, kadiri mti wa familia unavyozidi kutoa matawi yake, tunapata matunda matamu ya amani katiika jamii, utulivu na furaha.
Kwahiyo, uanzishwaji wa mazingira ya familia yenye amani huja katika kichwa cha orodha wa mambo yaliyopewa kipaumbele cha juu kabisa cha kuikuza jamii kuwa katika hatua ya juu kabisa ya usitaarabu. Mwanaume na mwanamke wanaotekeleza ahadi zao kwa kila mmoja kwa jina la Mwenyezi mungu mtukufu kwa kuwa hizo ahadi huweka malengo yao ya kufanya upendo wa kweli kulingana na makusudio ya uumbwaji wao. Bila shaka heshima kuu, uaminifu na usafi wa moyo vyote ni asili ya matendo yao!

No comments:

Post a Comment