Thursday, August 30, 2012

JUKUMU LETU KWA WATOTO WETU

Jukumu letu kwa watoto wetu

Ulimwengu ni makazi makubwa mno ya mitihani iliyopambwa kwa Baraka,vifungo, matarajio na raghba mbalimbali. Rasilimali za kidunia kama vile fedha, mali na watoto ni mitihani tuliyokabidhiwa ili tuwekeze kwa ajili ya Maisha ya baadaye. Kwa hivyo, ni muhimu kuzichukulia rasilimali za kidunia kama nyenzo za ustawi kwa ajili ya maisha ya Akhera. Qur’an Tukufu inatueleza:
“Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini.” (Kahf, 18: 46)
Wakati pesa, mali na watoto ni pambo zinapotumika katika njia ya Mwenyezi Mungu, pindi zinapotumika vibaya kwa ajili ya starehe na matamanio, baraka hizi zinaweza kumpeleka mtu kwenye njia ya taabu.
Walengwa wa karibu zaidi kwa Mwislamu ni watoto wake. Urithi pekee wa kweli ambao anaweza kukiachia kizazi chake ni neema za milele. Ni jukumu letu kuwaachia watoto wetu urithi wa daima, neema isiyonyauka wala kuisha, badala ya mali na furaha ya muda mfupi. Urithi wa milele ni Qur’an Tukufu na Sunnah tulizopewa na Mtume Muhammad (s.a.w). Kuhakikisha kuwa urithi huu mtakatifu unawafikia watoto wetu ni sababu kubwa ya wazazi kuendelea kupata thawabu, na kupuuza jambo hili ni sababu kubwa mno ya wazazi kupata adhabu na mateso katika maisha ya Akhera.
Mwenyzi Mungu Mtukufu anatuamrisha akisema; “Enyi mlio amini! Zilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe.” (Tahrim, 66: 6)
Mtukufu Mtume (s.a.w) naye anatuonya akisema; “Kila mmoja wenu ni mchunga na ataulizwa kwa alivyovichunga. Mwanaume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake na ataulizwa, na mwanamke ni mchunga wa nyumba ya mume wake naye ataulizwa”. Anasisitiza kuwa malezi na makuzi ya watoto ni jukumu shirikishi.
Katika hadith nyingine, Mtukufu Mtume (s.a.w) anasema; “Watendeeni wema watoto wenu na wafundisheni tabia njema.” (Ibn Majah, Adab 3)
Katika Hadith ifuatayo, Mtukufu Mtume (s.a.w) anaonyesha kuwa jukumu la malezi ya watoto ni bora zaidi kuliko hata Jihad, ambayo ni mojawapo ya amali zinazoheshimika sana katika dini ya Kiislamu. Mtume (s.a.w) alipojua kuwa hakuna mtu ambaye angewatunza wake na watoto, au wazee wa masahaba fulani waliotaka kushiriki katika vita vya Jihad, aliwaambia, “Rejeeni mkaziangalie familia zenu, kwani kufanya hivyo ni Jihad kubwa.”
Siku moja kijana mmoja mkakamavu, jasiri na mwenye afya njema, alikuja kumtembelea Mtume (s.a.w), na maswahaba walimstaajabia sana na kuvutiwa naye. Wakiwa wameshindwa kujizuia walisema;
“Ewe Mtume wa Allah! Kama kijana huyu jasiri angeshiriki katika vita kwa ajili ya Mwenyezi Mung (Jihad) ingekuwa jambo jema.”
Mtume (s.a.w) akawajibu, “Ikiwa kijana huyu anafanya juhudi kwa ajili ya mama na baba yake, anafanya juhudi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kama anafanya juhudi ya kulinda staha na heshima yake, anafanya juhudi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kama anafanya juhudi ya kutafuta riziki kwa ajili ya familia yake, anafanya juhudi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Lakini iwapo anafanya hivyo kwa ajili ya kutaka kusifiwa, basi yuko katika njia ya Shetani.” (Haythami, VIII, 144; Al –Mutaqqi, IV, 12/9252)
Katika Hadith ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w) anazungumzia thawabu, anahamasisha malezi ya watoto akisema:
“Zawadi bora ambayo mzazi anaweza kumpa mtoto wake ni tabia njema”. (Bayhaqi, Shuabul Iman, VI, 401 – 402)
Kila mzazi anatakiwa kuwa mfano kwa watoto wake katika ibada, tabia na maadili, na anatakiwa kuwalea tangu wakiwa wadogo, kama inavyosimuliwa katika kisa kifuatacho;
Tangu akiwa mtoto Abdullah bin Abbas alimuiga Mtume (s.a.w) baada ya kumuona akiswali swala ya usiku, na anaielezea kumbukumbu hii nzuri kama ifuatavyo:
“Usiku mmoja nilikuwa kwa shangazi yangu Maymuna, mmojawapo wa wake wa Mtume (s.a.w). Mtukufu Mtume (s.a.w) naye pia alikuwepo. Aliongoza swala ya ishaa, kisha akaja nyumbani na kuswali rakaa nne zaidi. Baada ya kulala kidogo alizinduka, nikamsikia akisema ‘mtoto mpendwa amelala,’ akinikusudia mimi. Kisha aliamka. Nami pia niliamka kuswali, nikasimama upande wake wa kushoto. Mtume (s.a.w) aliniweka upande wake wa kulia, akaswali rakaa tano, kisha akaswali rakaa nne zaidi…” (Bukhari, Ilm, 41)
Katika matukio mengine, akiwa bado mtoto mdogo, Ibn Abbas alishiriki swala ya jeneza na swala za Eid sambamba na Mtume (s.a.w), akipata bahati ya kuswali sana pamoja na Mtume (s.a.w) ( Bukhari, Janazah, 60, Idayn 16)
Mtume alikuwa akila na watoto, akiwaangalia, akizichangamsha akili na nyoyo zao, na akiwasahihisha katika makosa yao kwa njia nzuri.
‘Umar bin Abu Salama alielezea maneno ya hekima ya mtume:
“Nilikuwa miongoni mwa watoto waliolelewa chini ya malezi na uangalizi wa mtume (s.a.w).Wakati nilipokuwa nikila, mkono wangu ulikuwa ukizunguka sahani yote nikichukua, hivyo siku moja mtume akaniambia:
“Kijana, taja jina la M/mungu, kula kwa kutumia mkono wako wa kulia, na kula chakula kilichokuwa upande wako.” (Bukhari, Muslim)
Kwa mujibu wa riwaya nyingine, Mtume Muhammad (s.a.w) alisema “Sogea karibu yangu ule” akimfundisha taratibu za kula kirafiki na maneno mazuri ya upendo. (Ibn Majah)
Kwa hakika, mama na baba ambao wanataka watoto wao kuwa na tabia nzuri zenye kupendeza, ni lazima kwanza wafanye kila liwezekenalo wao wenyewe wawe ni mfano mzuri zaidi wa tabia hizo. Kama mtume alivyosema, “Heshimu wanawake wa wenzako, wanawake wako watakuheshimu, Kuwa mtii na mwenye huruma kwa wazazi wako, watoto wako watakuwa watii na wenye huruma kwako. Mtu ni lazima awe tayari kusamehe ndugu zake hata kama ni wakosa, kinyume na hayo, hatokuwa pamoja nami pembezoni mwa mto wa Kawthar huko peponi.” (Hakim IV, 170/7258)
Tunawajibika siku zote kukaa na watoto wetu kwa huruma, na tusiwapelekee katika fikira zisizofaa. Mfano ufuatao ni somo tosha kwetu sote:
Mtu mmoja alikuja kwa Abdullah bin Mubarak na kumlalamikia kuhusiana na ubaya wa tabia za mwanae. Abdullah bin Mubarak akamuuliza:
“Umeshawahi kumtolea maneno makali mwanao?” hivyo yule mtu akajibu:
“Ndio nimewahi kufanya hivyo” Ndipo Abdullah bin Mubarak aliposema:
“Wewe ndio sababu ya tabia hizo za mwanao”
Nukta nyingine muhimu ni kuwa mama au baba wasijaribu kuwalaghai watoto wao, na wawafundishe kuwa wakarimu. Abdullah bin Amir alielezea:
“Siku moja mama yangu aliniita wakati mtume yupo nyumbani kwetu, alisema:
-Njoo hapa, nataka nikupe kitu, hivyo mtume alipouliza:
-Unakusudia kumpa kitu gani? Mama yangu alijibu:
-Tende. Ndipo mtume akasema:
-Ikiwa hutampa kitu, itanukuliwa katika akili yako kuwa umemdanganya.” (Abu Dawud Adab, 80; \ahmad III, 447)
Katika hadithi nyingine, mtume alisema: Waleeni watoto wenu kwa huruma. Wote wanaohisiwanaweza kuondosha utovu wa nidhamu kwa watoto wao.” (Haythami)
Kwa kuongezea katika mapambano ya wazi ya kuelimisha watoto wetu. Tunawajibika pia kuswali kila siku, kwa kuwa elimu na swala vyote ni muhimu kwa wokovu wao.Ibn Abbas amesimulia, “Mtume alinikumbatia na kusema: “Ewe Allah Mpatie huyu hekima.” Na kwa baraka ya dua ya mtume, wakati alipokuwa mkubwa, alineemeshwa na sifa ya Mwanachuoni mkubwa wa waislamu na pia ni mfasiri wa Qur’an: Mfasiri alieleta changamoto katika maana ya Qur’an.”
Maneno haya yalizungumzwa na wachamungu wakubwa waliotangulia ni mifano mizuri zaidi ya ushauri unaohusu uangalizi wa watoto:
Abu Zakhariah Al-Anbar amesema: “Pasi na kuwa na mbinu mbadala, Taaluma ni sawa na kuni bila ya moto.”
Maneno ya ushauri toka kwa Ali kwenda kwa mwanawe ni mfano mkubwa kwetu sote, pale aliposema, “Ushauri wangu wa kwanza na wa kipaumbele zaidi kwako mwanangu ni kumkhofu Allah kwa kila jambo, kuwa mja wake mtiifu, na umkumbuke katika nafsi yako kila wakati.Kwa uangalifu chunga taratibu zinazokupeleka kwake (Qur’an na Uislamu).Kuna kifungo chochote kinachoweza kuwa kikubwa na muhimu kati yako na muumba? Ichunge nafsi yako kwa umakini kabisa ukitazama wakati wa umauti wako.Pandikiza uchamungu na uharibu matamanio ya nafsi yako, sikiliza kwa makini maneno yangu ya ushauri, tambua kuwa allah, amabe anamiliki kifo cha kila nafsi katika umiliki wake, pia ana miliki maisha yako.Yeye ndie anetoa uhai kwa vilivyopo, ndie ambae anachukua uhai huo, Yeye ndie ambae anamfanya tajiri kuwa masikini, na masikini kuwa tajiri.Yeye ndie ambae huleta kila aina ya taabu, matata, majonzi na maradhi na pia ndie ambae anatoa ulinzi na matibabu.Haijalishi umejihusisha kiasi gani katika elimu, bado utabakiwa na vitu vingi ambavyo ni lazima ukavisome, kwa hiyo kuna kweli nyingi nyuma ya mipaka ya fikira na nguvu za uono.Ikiwa utajaaliwa na lolote miongoni mwa kweli hizi, na allah akakufundisha hekima na busara, usije ukafikiri kwamba umeyapata hayo kwa nguvu zako binafsi.Kinyume chake, chukua kimbilio kwa aliye mtukufu zaidi na umpende, muabudu na umtii yeye pekee inavyotakikana, Uzuri wa ulimwengu huu ni mdogo na uhai wake ni mfupi, na mabadiliko yake ni ya haraka na yenye kuleta huzuni, furaha yake ni ya bandia na neema na ukarimu ni wake ni wakupita, dhambi na dhima yake ni ya milele, siku zote kumbuka chanzo kikuu cha maovu yote ni ni matamanio ya mali na hutakiwi kuruhusu tabia hizi za shetani kuingia ndani ya moyo wako! Kuwa mchamungu utaweza kujizuilia chukua uzoefun toka katika orodha ya waliobarikiwa inawezekana na katu usitume au kutegemea furaha hizi, zitumie katika njia ya Allah”
Imam Ghazali alitoa maneno haya ya usia kwa mwanae “Mwanangu elimu pasi na vitendo ni wazimu, na vitendo pasi na ujuzi ni upuuzi, tambua kwamba elimu hii leo haitakuweka mbali na uasi wala kukupeleka katika utii, hakutakuwa na umbali kati yako na moto wa kuzimu kesho”
Khalifa wa tano kutawala akiwafuatia makhalifa waongofu, Umar bin Abdul Aziz ambae alikifia kilele cha taaluma, hekima na uchamungu, na wakati wa mwaka wake wa pili na nusu kahalifa aliangazia moja ya utendaji wa kuheshimika zaidi, alibadilisha kivitendo kuelekea watoto wake kufuatia ushindi wake kama Khalifa katika siku aliyoigia madarakani, aliwaelekeza watu wakati abdul Malik, shati la mtoto wake lilipokuwa limechanika na wamejichanganya katikati ya kundi la watu walipoona pahala palipochanika, Umar alimwambia mwanawe akalishone shati hilo, “Mwanangu nenda kashone shati lako, unaweza ukawa huna tatizo la mavazi hivi sasa ila baadae ukalihitaji.”
Umar bin Abdul Aziz angeenda chumbani kwa binti yake kila usiku na kumjulia hali yake kabla ya kwenda kulala, usiku mmoja bintiye huyo alikuwa akifumba mdomo wakati wa kuzungumza na baba yake, wakati umar alipomuuliza mtumishi wao kwanini bintiye alifanya vile, alijibu
“Hakukuwa na chochote cha kula isipokuwa vitunguu na maharagwe, walifumba midomo yao ili usihisi harufu ya vitunguu.” Alivutika sana na tabia yao ya kichamungu na hisia ambapo macho yake yalijawa na machozi na akawaambia binti zake, “binti zangu wapendwa ikiwa mtapenda vyakula vizuri na furaha za ulimwengu, baba yenu atapata tabu huko akher”
Pia wakati; Umar alipokuwa katika kitanda chake cha mauti, mmoja aliyekaribu naye akasema “hujaacha mali yoyote kwa ajili ya familia na watoto wako” Ndipo akajibu, “Ikiwa watoto wangu ni watiifu kwa Allah atakuwa radhi nao, ikiwa watoto si watiifu kwa Allah kuwaachia utajiri hakutawasaidia”
Muadh bin Jabal alimuusia mwanawe, “Mwanangu wakti unaposwali, iswali swala hiyo kana kwamba ndiyo swala yako ya mwisho na katu usitarajie kuifika swala inayofuata, muumini anatakiwa kufa akiwa katikati ya mema mawili, wakati muumini anafanya jambo jema, anatakiwa kuwa na malengo ya kufanya jema linguine baada ya hilo, na hakuna jambo ovu litalokuja kati ya mambo haya mema mawili”
Maneno haya ya usia na maonyo ni muhimu sana kwa maisha katika kujichunga kuelekea katika furaha njema kwetu sote, na watoto wetu kutoka na utawala huo tunatakiwa kuzivunja tamaa mbovu na uovu, na kujiandaa wenyewe kwa ajili ya kukutana na muumba kabla hatujauacha ulimwengu huu wenye kukoma katika hali ya kuangalia kwa umakini ni vipi tunatumia uhai wetu, wapi tunapata utajiri wetu na tunautumiaje, ni nguvu kiasi gani tunatumia kuelimisha watoto wetu, watatuletea sifa au kutupunguzia siku ya hukumu na hatimaye matendo yetu yakiwa mazuri au mabaya Qur’an inatumbia: “Na jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni Fitna (mtihani), na kwamba kwa Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa.”(Anfal 8 28)
Mtume (s.a.w) alielezea katika hadithi kuwa mtoto anaefundishwa dini yake, anaandaliwa maisha ya milele huko akhera, na matokeo yake, hufunuliwa ubora wa tabia njema ni maana ya furaha na amani katika ulimwengu huu, na akhera kwa wote yeye mtoto na wazazi wake.Kutokana na habari iliyotolewa na mtume “Baada ya umauti, mja hupandishwa, kisha mja huyo huuliza:
Ewe mola, ni kipi nilichofanya kutunukiwa malipo haya? Ndipo Allah (s.w) atapomjibu
Mtoto wako wema (uliemuacha nyuma) amekuombea na kujitolea kwa ajili ya msamaha wako” (Ibn Majah Adab I Ahmad II, 509)
Kutokana na taarifa ya Ibn Abbas mtume s.a.w, “Mtu aliekufa ndani ya kaburi ni sawa na mfa maji anayetapatapa kutafuta msaada, akitumainia kufikiwa na msaada toka kwa baba mama au rafiki yake mpendwa na hilo ni jepesi zaidi kuliko ulimwengu na vyote vilivyopo ndani yake, Mwenyezi Mungu hushusha rehma kubwa zaidi ya milima humo kaburini kwa wote walio mara nyingi duniani wakijitolea na zawadi kubwa aliyehai kumuendea aliekufa ni kumuombea msamaha” (Daylami Musnad IV; Ali Al-Muttaqi XV)
Katika hali kama hiyo, maana pekee ya wokovu huko akhera ni kuendelea kwa mambo mema tuliyoyawacha na lililo muhimu kuliko mengine yote ni mtoto mchamungu, Asik pasa mtunzi wa Garibname, kitabu cha mashairi ya kisufi alielezea nasaba ya mja huendelea katika sehemu nne
1. Sulbi hii ni nasaba ya mtu binafsi anaemiliki mtoto, na muendelea kwa kizazi hiki kunategemea majaaliwa siku moja kizazi hiki kitakuja kukoma na inatupa mashaka kama nasaba hii itasitawi au la
2. Mali Huu ni usmbazaji wa utajiri na upendo wa mtu binafsi na malipo ya sadaka hii huendelea kwa kadiri mja yule alivyotoa zakat
3. Irshad Hawa ni watoto, na wanafunzi wanaojituma, na ukawaacha baada ya umauti nasaba hii itaendelea kwa kadiri watavyoendelea kufundisha wengine.
4. ‘Ilm ma Irfan hivi ni vitabu au makala zilizoandikwa kuvutia fikira na nafsi zote katika njia ya ukweli, hii ndio njia nzuri na yenye maskahi zaidi kuliko kazi zote kwa kuwa itaendelea kuwavutia kila wasomao makala hizo katika imani kamili, hadi kufikia siku ya hukumu.
Kufuatana na hayo, somo kuu ambalo kila mama na baba anatakiwa kuliangalia kufuatilia elimu za watoto wao na ni lazima tutende hivyo, na kuzuia wivu wa aina yoyote kati ya watoto wetu wakti utapofikia, tutawaingiza watoto wetu katika ndoa ndani ya mipaka ya uwezo wetu na wakati wa kutafuta mke au mume tunawajibika kuzingatia vigezo vya dini yetu na mwenendo mwema, ikiwa ndoa itafanyioka nje ya taratibu hizi huenda ikaishia katika talaka, au itakuwa ni sababu ya mateso na taabu hadi siku ya umauti, tunawajibika kuwachunga watoto wetu katika hali ya juu ya uwezo wetu kuwaepusha na uzembe, kuchelewa kurudi nyumbani, kwenda kuzurura pasi na sababu maalum, na kuepukana na marafiki wasiofaa, tuwaelekeze watoto wetu kuwa makini na majukumu yao, kuwa na heshima kwa familia zao, wakubwa, jirani, wanyonge, yatima, masikini, na kuwaombea kila mara.Tunatakiwa kuwafundisha watoto wetu kuwatembelea wagonjwa, kuwasaidia wenzao, na kujizoesha kutoa sadaka katika kuongeza hali njema ya kiroho kwao, pia tunatakiwa kuakisi uwajibikaji ulioelezwa katika Sunnah za mtume wetu na taarifa za wanachuoni na viongozi waliotazamia upendo, kujitolea, na kusimamia haki na uadilifu katika nyoyo zao
Ewe Mwenyezi mungu waongoze watoto wetu wawe wawajibikaji katika dini yetu hapa nchini na ulimwenguni kote, na uwalinde na kizinga cha uovu na vishawishi vinavyowazunguka na uwajaalie wawe ni sadaka yenye kuendelea kwa ajili yetu huko akhera
Amin!

No comments:

Post a Comment