Wednesday, April 23, 2014

MUINGEREZA NA SHEIKH

Mwanaume wa kingereza alienda kwa sheikh na kumuuliza: Kwanini hairuhusiwi kwa mwanamke wa kiisilamu kushikana mikono na mwanaume? 

Sheikh akamuuliza: Je wewe unaweza kushikana na mkono na malikia Elizabeth?

Yule mwanaume wa kingereza akajibu: Bila shaka hilo jambo haliwezekani, wako watu maalum wenye kuweza kushikana mkono na malkia Elizabeth.

Sheikh akajibu: Wanawake zetu ni malkia na malkia hawawezi kushikana mkono na mtu yeyote wasiyemjua au kuidhinishwa.
Kisha kijana yule wa kiingereza akauliza tena: Kwanini wanawake zenu wanafunika mwili wote hadi nywele?

Sheikh alitabasamu, kisha akatoa pipi mbili, akaifungua ya kwanza kisha ingine akaicha haijafunguliwa. Akazitupa zote mbili chini katika vumbi kisha akamuuliza yule mwanaume wa kiingereza:  endapo utatakiwa kuchukua pipi moja wapo kati ya hizo mbili hapo chini, ipi utaichagua?
 
Yule mwanaume wa kiingereza akajibu: Hiyo ambayo haijafunguliwa.  Sheikh akasema; Hivyo ndivyo tunavowaweka uwaonevyo wanawake zetu

No comments:

Post a Comment