Qur’an Tukufu inasema:-
“Hakuna
kulazimishwa katika dini (kuingia katika dini), hakika
uongofu
umekwisha pambanuka na upotovu umedhihirishwa”
(10)
“Na
sema huu ni ukweli uliotoka kwa Mola wenu, basi
anayependa
akubali, na anayependa basi akatae, kwa
hakika
tumewaandalia
madhalimu moto ambao kuta zake zitawazunguka” (11)
“Lakini
wakikataa, basi hakika juu yako ni kufikisha tu ujumbe uliowazi”
Injili ya Mathayo 10:34 inasema:-
“Msidhani
ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja
kuleta
amani, basi upanga”
Bado wanadai kwamba Uislam ni dini ya
upanga lakin Ukristo ni dini ya upendo, iwezekanaje? Kutokana na ushahidi wa
{10:34} Mathayo?
Kanisa liliposhusha jina la mwanamke na
kumdhalilisha kwa kumuona kuwa ndiye chanzo cha uovu na dhambi, Uislam ulikuja
na kuinyanyua daraja ya mwanamke na kuiweka juu. Muhammad (S.A.W) akasema:-
“Wanawake ni sawa na wanaume”.
Uislam umemfanya mwanamke kuwa ‘Mnara’
wa wema na huruma; taji linalopamba kichwa cha kila mwanamke wa Kiislam ni mapendo
na huruma. Ndoa ya wake wingi ilienea
sana na ikakubalika kwa watu wote hata watumishi wa Kanisa wenyewe. Mtawala wa Kirumi Jastinian - mtunga sheria
wa kipagani- ndiye aliyekuwa wa kwanza kufikiri juu ya kuweka sheria ya kuweka
kikomo cha idadi ya wake na kuwa mmoja lakini Kanisa lilipinga fikra yake hiyo.
Uislam ulipokuja ulijaribu kuiwekea
udhibiti ndoa ya wake wengi. Ilikuwa ni
kazi ngumu kuzuia mtazamo wao huu. Bali
Uislam ukaingiza utaratibu wa mwanaume mmoja kuruhusiwa kuoa wake hadi wanne. Hii ilikuwa kama ponyo kwa watu wasiendeleze
uchafu wa uzinzi. Hakuna dhambi kwa
asiyeweza kuitekeleza na wala haivunji sheria
za Uislam, ijapokuwa ni bora sana kwa wenye kuweza ‘kufanya uadilifu’
kuna faida nyingi sana katika hili kwa pande zote mbili ‘mke na mume’
“Ndoa
ya mitala ni tiba na sio matendo ya mazoea”
Nani anayesema kuwa Wamagharibi
wamefungwa kuwa na mke mmoja tu? Je siku
hizi hakuna ndoa za mitala katika nchi za Kikristo?
Kwa
hakika ndoa ni mkataba unaowekwa baina ya mwanaume na mwanamke. Lakini kwa kuwa yana husika kwa kiasi kikubwa
na mustakbali wa vizazi na kwa kuwa yanaungana sana na uthabiti wa kweli wa
nasaba za wahenga kupitia ndoa, Uislam unachukulia muungano huu kuwa ni kitu
kitukufu. Kama tukiiangalia ndoa kama
ndoa tunakuta kuwa Wakristo huko Magharibi wana mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengi kuliko hata Waislam. Kwa
kweli Wakristo huwa na wanawake wengi bila haya, kile anachokifanya Mwislam kwa
kikomo kilichothibitishwa na madhumuni yaliyohalalishwa huchukuliwa kuwa ni
aibu au kosa na kuitwa mitala, wakati ambapo Mkristo hufanya ufedhuli bila
kuona haya na bila kizuizi haadhibiwi na sheria; ni uzinzi.
Maadui wa Uislam wanatambua vyema kuwa
lau wangetumia sehemu ya juhudi zao katika kukashifu na kusingizia mafundisho
yoyote kinyume na Uislam mafundisho hayo yangekanushwa. Lakini ni jambo la kawaida kwamba Uislam
husimama imara, kwa utukufu, hupanda milima na hatimaye kushinda vita vyote vinavyoanzishwa na kupigana dhidi
yake. Kwamba Uislam ni dini ambayo siku zote
inakwenda mbele na kukuendelea kwa rehma, ulinzi na msaada wa Allah:-
“Hakika
sisi tumeiteremsha Qur’an, na hakika sisi ndio wenye
kuilinda”
Ndani ya makala hii tumejadili juu ya
imani na mafundisho ya Uislam, si matendo yenye makosa ya baadhi ya wanaofuata
dini hii kwa jina tu. Maisha na matendo
ya kweli ya baadhi ya Waislam wa siku hizi yanatofautiana na mtazamo wa Uislam
wa kweli. Uislam sio yale wayaonayo
Wamagharibi katika matendo ya mtalii wa Kiarabu ambayo hukanyaga maadili yote
wakati akikimbia kwa kutwetatweta kwenda kuridhisha matamanio yake, kwani sio
kila Mwarabu ni Muislam na hivyo mitazamo wanayotumia kuhukumu Uislam
wanakosea.
Mwisho ninapenda kuwatanabahisha wale
ambao wamejiamulia kashfa dhidi ya Uislam kama kazi yao na kujitolea kuuvunjia
heshima, kwamba ukweli na nguvu na ni wenye kushinda na kwamba hisia za chuki
katika maamuzi siku zote humpeleka mtu kwenye hitimisho lenye makosa.
Vile vile tunawakumbusha kuwa shutuma
zao na mazungumzo yao ya bure yanafahamika vyema na hurudiwarudiwa mara kwa
mara, na kwamba Uislam unapotoshwa
katika akili zao si katika uhalisia wake.
“Hakika
Mwenye-Enzi-Mungu amewafanyia hisani kubwa Waislam alivyowaletea Mtume
miongoni mwao, anayewasomesha aya zake.
Aya zake na anawatakasa na kuwafundisha kitabu na hekima na bila shaka
kabla ya hapo walikuwa katika upofu mkubwa”
{3:164}
Ninapenda kuwaambia wasomaji kuwa
mazungumzo au majadiliano yapo wazi kwa watu wote, kwa utulivu, bila wasiwasi,
kwa uadilifu, bila upendeleo, bila chuki, uongo na fujo ambazo kamwe
hazipelekei kwenye matokeo yoyote mazuri.
Basi majadiliano baina ya ustaarabu
masuala mbali mbali na yaanze katika ulimwengu huu ambapo masafa na na umbali
umeondoshwa kuonyesha ukweli. Mtu
anaweza kuwa Damascus, muda wa asubuhi na jioni akawa London au New York, au
jioni anaweza kutembelea Paris au Rome na asubuhi akazuru Karatch au
Tokyo. Majadiliano ni njia nzuri ya
kudhihirisha ukweli.
Zama mpya au mwanzo wa historia mpya
baada ya kufunga mlango wa karne ya ishirini zinapaswa kuanza kwa mtu kutafuta
mambo mema popote yalipo hata kama yamo katika Uislam ambao ushabiki wa Kanisa
umeiharibu sura yake kwa makusudi machoni mwa Wamagharibi ili kuwazuia
wasiukaribie.
Ni wakati mwafaka kwa wapenda elimu na
ukweli, kwa kutumia majadiliano ya busara na maarifa, waondokane na picha ya
uongo ya Uislam iliyochorwa na ushabiki wenye chuki wa wabebaji wa
msalaba. Uzayuni una nafasi kubwa katika
kutangaza propaganda hizo kwa kutumia uwezo wa kila aina ya vyombo vya habari inavyorimiliki.
Katika maisha ya kila siku mtu hufanya
juhudi kujua iwapo habari alizosikia ni za kweli au sio za kweli. Huwenda likawa tukio la kawaida
linalorudiwarudiwa mahali popote ulimwenguni.
Katika kutafuta ukweli wa habari au ripoti aliyoisikia binadamu
hujiheshimu yeye na huiheshimu akili yake, basi itakuwaje iwapo ukweli
anaoutafuta unahusu dini yeye mabilioni ya wafuasi au waumini. Je hapaswi kuiandaa akili yake katika kutaka
kujua misingi na mafundisho ya kweli? Je wakati haujafika wa kuudurusu Uislam
kwa busara na bila ya ushabiki na upendeleo katika namna ile ile inayofanywa na
mtu mwenye akili kudurusu jambo lolote popote pale ulimwenguni katika maisha
yake ya kila siku? Ninatambua kuwa jibu
sahihi la mtu makini ni ndiyo.
No comments:
Post a Comment