Monday, May 21, 2012
Naomba Kufahamu, Hii Nguo Ni Ipi?
1. Nguo inanishangaza, sio siri ndugu zangu
Tena inanitatiza, katika fikira zangu
Yafanya najiuliza,maswali kichwani mwangu
Hii nguo, nguo gani?
2. Nikiiona dukani,nguo hainivutii
Sioni yake thamani,na wala siiwanii
Wengi hawaitamani,tena hawaichahagui
Hii nguo, nguo gani?
3. Wale waliojaribu,hii nguo kununua
Wameonwa wa ajabu,wengi wamewashangaa
Wamekosa majawabu,maswali yalivyojaa
Nguo hii nguo gani?
4. Mwisho wa siku lakini,hii nguo tutavaa
Tuiwekapo mwilini,kamwe hatutoivua
Hatutojali thamani, wanadamu nawambia
Hii nguo, nguo gani?
5. Hii nguo,nguo ipi wanaukumbi nipeni jibu
Mwenye hoja uko wapi kwako nangoja jawabu
Michuzi nawe vipi swali langu unijibu
Malenga Nawauliza, Hii Nguo Nguo Gani?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment