Nadharia ya
mabadiliko ya bahati nasibu yanaharibu uhai na hayawezi kuzalisha viungo
vinavyoendana.
Wafuasi wa Darwin
wanashikilia kuwa viumbe hai wanabadilika kutokana na mabadiliko ya bahati
nasibu na mabadiliko hayo yasiyo na utambuzi ndiyo yaliyozalisha viumbe mbalimbali
vizuri tunavyoviona hapa duniani hivi leo.
Dai hili linadhihirisha wazi
kutoendana na mantiki.
Mabadiliko haya ya
kimaumbile ni uvunjikaji, uharibifu na uhamishwaji unaotokea kwenye DNA iliyopo
ndani ya kiini cha seli hai kilichobeba taarifa yote ya jeni zake, mabadiliko
haya ni matokeo ya athari za mionzi na kemikali katika DNA. Asilimia tisini na
tisa ya mabadiliko yote huharibu kiumbe wakati asilimia moja iliyobaki haina
athari kabisa. Kamwe haijawahi kuonekana mabadiliko haya yakimnufaisha kiumbe
yeyote. Cha zaidi ni kwamba...
·
Kutokana na madai ya Darwin, mabadiliko haya
hayana budi kuzalisha mabadiliko ambayo yanalingana na kuendana na kila sehemu
ya mwili.
·
Kwa mfano, kutokana na madai ya
wanamabadiliko ya kimaumbile, kama sikio lilijitokeza upande wa kulia kwa
kupitia mabadiliko kwa namna walivyoelezea, hivyo pia mabadiliko yaliyofanyika
bila ya mpangilio maalum hayana budi kuzalisha sikio la pili lenye kufanya
kazi, huku likiwa na sifa zile zile. Fuawe, kikombe na kikuku cha kupandia
farasi vyote lazima vijitokeze katika sehemu mbili.
·
Mabadiliko ya bahati nasibu pia hayana budi
kuzalisha mishipa ya moyo katika pande zote. Kutokana na madai ya Darwin,
mabadiliko hayo yanatakiwa kuzalisha mishipa yote katika namna nzuri na katika
sehemu stahiki, katika muda sawa na katika mpangilio sawa.
·
Kinyume chake kutakosekana usawa mkubwa, na
matokeo yake yatakuwa ni viumbe vya ajabu ambavyo vitakuwa na sikio moja juu na
moja chini, jino lililo tofauti, au jicho moja puani na lingine kwenye bapa la
uso. Lakini kwa kuwa hakuna utofauti huo, Madai ya Darwin yana maanisha kuwa
mabadiliko hayo yatakuwa yamezalisha kila kitu katika usawa na muendano.
·
Lakini ukweli kwamba mabadiliko haya
yanasababisha madhara kwa asilimia 99 na ni dhaifu kwa asilimia 1 inapelekea
isiwezekane kuzalisha viungo sawa, vyenye mantiki na vinavyoendana kwa wakati
mmoja.
·
Madhara ya mabadiliko haya juu ya maumbile ya
kawaida ni sawa na kuyafyatulia risasi. Kukifyatulia risasi kitu kizima
kutakiharibu.Ukweli kuwa risasi moja haina madhara, au inaangamiza maambukizo
yaliyopo ndani ya mwili na hivyo kuyaponya, hakubadilishi chochote. Kiumbe
atakuwa ameangamizwa kwa risasi nyingine 99 zilizokishambulia.
Sayansi Inapingana
Na Wanadarwin, Na Wanaomkana Mungu
Mabadiliko ya kimaumbile ni
ulaghai wa kisayansi. Kwa miaka mingi sasa, Wanafuasi wa Darwin wamekuwa
wakitumia sayansi kupotosha watu juu ya mabadiliko ya kimaumbile. Lakini mpaka
sasa sayansi ni adui wa nadharia ya darwin.
- Sayansi inapingana na ukanaji Mungu. Sayansi inapingana na wakomunisti, na wafuasi wa maksi.
- Sayansi inaangamiza fikra za wafuasi wa maksi, wapinga mungu na wafuasi wa darwin. Sayansi ndiyo iliyoangamiza nadharia za Darwin.
- Sayansi ndiyo iliyopambana na propaganda za Darwin kwa nguvu zaidi.
- Sayansi imeshinda ulaghai wa wana mabadiliko ya kimaumbile ambao wamekuwa wakiwafundisha watu kwa miaka mingi.
- Sayansi imeangamiza misingi ya falsafa ya wapinga Mungu.
- Sayansi inateketeza na kuangamiza nadharia ya Darwin popote inapoenda, popote inapokuwa ni mada ngeni, na popote inapojitokeza. Kwa hiyo, Sayansi inawakilisha moja ya kero kubwa kwa wafuasi wa Darwin.
Sayansi ndiyo iliyoweza
kuonyesha kuwa protini kamwe haiwezi kuzalishwa kwa bahati nasibu.
Sayansi ndiyo
iliyodhihirisha ulimwengu wa seli usio wa kawaida, na imeonyesha kuwa kamwe
jambo lisingeliweza kuibuka kwa bahati nasibu tu.
Sayansi ndiyo iliyoonyesha
ukweli kuwa mabaki ya viumbe hai zaidi ya 350 yaliyogundulika kamwe hayakuibuka
kwa bahati nasibu.
Sayansi ndiyo iliyoonyesha
ugumu katika viumbe hai na kuonyesha kuwa viumbe hivi visingeliweza kujitokeza
kwa bahati nasibu.
Sayansi ndiyo iliyoonyesha
kuwa haiwezekani kwa aina moja ya kiumbe kubadilika kwenda kwenye aina nyingine
ya kiumbe.
Sayansi ndiyo
iliyodhihirisha mabaki ya viumbe hai katika kipindi cha kambrian. Kwa hiyo,
sayansi yenyewe imetoa ushahidi wa kutosha wa kuweza kufuta hii nadharia ya
mabadiliko ya kimaumbile, na bado inaendelea kufanya hivyo. Madai yote ya
Darwin yameporomoka mbele ya sayansi.
Sayansi inatoa hitimisho la
kustaajabisha ambalo linawakana moja kwa moja wafuasi wa Darwin ambao
wanajitahidi kuficha uongo wao kwa kusema “mabadiliko ya kimaumbile ni
sayansi”. Si kwamba sayansi inaihudumia dini; bali pia inatoa ushahidi wa
kuwepo kwa Allah Mtukufu. Sayansi ni kwa ajili ya wale wanaomuamini Allah.
Sayansi haina budi kutumiwa na waumini wa kweli. Ukweli huu umekuwa jinamizi
kubwa kwa wafuasi wa Darwin katika karne ya 21.
Mankind!
An example has been made, so listen to it carefully. Those whom you call upon
besides Allah are not even able to create a single fly, even if they were to
join together to do it. And if a fly steals something from them, they cannot
get it back. How feeble are both the seeker and the sought! (Surat al-Hajj, 73)
Nadharia
za Darwin ziliwezaje kuja na kutawala ulimwengu?
Itikadi ya wafuasi wa Darwin
ni uongo uliojiegemeza moja kwa moja kwenye ulaghai, kwa kushikilia kuwa maisha
yametokea kwa bahati nasibu. Lakini licha ya kuwa kinyume kabisa na mantiki,
uongo huu umetawala katika nchi zote za ulimwengu, serikali zake, mashule,
vyuo, mikutano ya kisayansi, sehemu za kazi, magazeti, majarida, idhaa za redio
na vituo vya luninga. Huu ni udikteta wa itikadi ya Darwin, mfumo wa hila ambao
umesababisha ulaghai wa Darwin kutawala ulimwengu. Udikteta huu wa hila ambao
umekuwa ukifanya kazi kwa miaka 150 iliyopita, kwa sasa upo katika machungu ya
kifo, ingawa bado ushawishi wake upo.
Kutawala kwa udikteta wa
itikadi za Darwin kunategemea vitisho, udhalimu, kukamia na kukandamiza.
HAIWEZEKANI KWA PROFESA ANAYEPINGA NADHARIA YA DARWIN KUFUNDISHA katika chuo
chochote duniani. Hakuna waziri mkuu katika nchi yoyote anayeweza
kutangaza kuwa anapinga nadharia ya darwin. Hakuna mwalimu anayeweza kuwaambia
wanafunzi wake kuwa mabadiliko ya kimaumbile ni uongo, na wanafunzi nao
hawawezi kuwaambia walimu wao kuwa hawaamini mabadiliko ya kimaumbile. Profesa au mwalimu yeyote atakayefanya hivi
ataondolewa katika wadhifa wake mara moja. Mwanafunzi atafeli somo husika. Haiwezekani Kwa Waziri Anayepinga Mabadiliko
Ya Kimaumbile Kubakia Katika Serikali.
Kwa hakika karibia juhudi zote zilizofanywa duniani kote kuwezesha ukweli
kuhusu uumbaji ufundishwe sambamba na nadharia ya mabadiliko ya kimaumbile katika
mashule hazikufanikiwa kusonga mbele.
Mashirika ya habari yanayofahamika yametakiwa kutoa taarifa kuhusu
mabaki ya uongo ya viumbe hai kana kwamba ndio ushahidi wa mabadiliko ya
kimaumbile. Hawana budi kuwajibika katika ulaghai huu kinyume chake kazi yao
uchapishaji itafikia kikomo. Haiwezekani kwa mwanasayansi au profesa ambaye
maisha yake ya kazi yamefikia kikomo kutokana na kutetea uumbaji, au kurejea
karatasi inayohusu uumbaji, kupata kazi nyingine. Pia kuna uwezekano mkubwa mtu
huyo akapoteza marafiki. Na bila shaka, hakuna hata haja ya kuuliza ikiwa mtu
huyo atapata tena nafasi katika fani ya sayansi.
Njia iliyotumika ni vitisho, udhalimu na ukamiaji. Kutokana na
vitisho na sera za udhalimu zilizotumiwa katika udikteta wa wafuasi wa Darwin,
watu wameshindwa kupinga nadharia ya Darwin kwa uwazi, na wameweza hata
kuwajibika mpaka leo. Kila njia inayowezekana inatumika kuzuia watu wasipinge
nadharia ya Darwin. Kinyume chake waungaji mkono wa imani ya kichawi yani
nadharia ya Darwin wasingelikuwa na namna yoyote ya kuendeleza nadharia hii
isiyo na mashiko. Uongo unasemwa kwa sauti ya juu, na inachukuliwa kuwa ni
uhalifu kuchukulia huu kuwa ni uongo. Nadharia iliyodaiwa kuwa ni ya kisayansi
pindi ilipozinduliwa, imegeuka na kuwa mfumo wa imani ya kichawi ambao
hauhusiani na sayansi, mfumo ambao umezuiwa wazi wazi kwa mtu yeyote kuupinga.
Ukweli ni kwamba jambo la kuzingatia ni kwamba ni kwa namna gani jambo hili
linafanywa kwa wazi bila hata aibu yoyote.
Nadharia
ya mabadiliko ya kimaumbile, ambayo inameleta maafa makubwa katika dunia, pia
inatafuta kuzuia maendeleo ya sayansi.
Leo hii
mamilioni ya dola yanatolewa kwa ajili ya masomo ya mabadiliko ya kimaumbile.
Kujifunza mabadiliko ya kimaumbile inamaanisha kutumia fedha kwa
ajili ya kuzalisha ulaghai mpya na kuutawanya kwenye vyombo vya habari. Fedha
hii ambayo ingeliweza kutumika katika maendeleo ya tafiti za kisayansi na
maendeleo ya fani ya udaktari, kwa mfano katika kutibu kansa, ugonjwa wa ukali,
au ingelitumika kuokoa mamilioni ya watu kutokana na kufa kwa ajili ya njaa
katika bara la Afrika, kinyume chake inachukuliwa kutoka kwa watu wasio na
hatia na kupotezwa kwenye ulaghai.
Mabadiliko ya kimaumbile, ambayo ni ulaghai wa hali ya juu wa
miaka 150 iliyopita, imesambaa duniani kote na kiini macho cha hali kimeingizwa
kwa watu kwa kutumia mbinu za udikteta wa nadharia ya Darwin. Kama ambavyo
tumeona, nadharia ya Darwin imepata uungaji mkono wa dunia, si kwa sababu ya
kuwa ya kisayans, bali kwa sababu watu wamelazimishwa na kushurutishwa
kuiamini, na inalindwa na udikteta wa nadharia ya Darwin. Watu wasidanganyike
na ukweli kuwa watu wengi wanaonekana kuinga mkono nadharia hii kwani baadhi ya
watu hawa hawafahamu kuwa nadharia ya Darwin ni ulaghai mkubwa mno, wakati
wengine wanaonekana kuunga mkono nadharia ya Darwin kutokana na hofu yao juu ya
kupoteza ajira yao au kukosolewa kwa uadui. Utawala wa nadharia hii ya uongo
ulimwenguni na katika taasisi zote mbovu ulioletwa na udikteta wa nadharia ya
darwin, ambayo ni ya kishetani, vyote vimeanza kuangamia kimoja baada ya
kingine. Na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, maangamizi ya moja kwa moja ya
nadharia hii ya mabadiliko ya kimaumbile yamefika, ni kiasi cha kusubiri
kidogo.
Atlasi Ya Uumbaji Na Wafuasi Wa Darwin Ambao Wamepoteza Imani Yao
Juu Ya Itikadi Yao
Pindi mtu aliyefungiwa katika chumba atakapoambiwa kuwa 'nje kuna
giza' kuna uwezekano wa asilimia hamsini akaamini. Lakini pindi atakapoona jua
nje kwa kupitia kwenye nyufa hakutakuwa na njia yoyote ya kumshawishi kuwa nje
kuna giza.
Wafuasi wa Darwin nao wapo katika utata huu huu. Wafuasi wa Darwin
wamekuwa wakisambaza aina zote za uongo na kuonyesha kuwa ni sayansi. Kamwe
hawakuhisi aibu hata kidogo kwa sababu wamejishawishi wenyewe kuwa wanaweza
kuwadanganya watu kwa taarifa hizi za uongo. Uongo ulirudiwa kwa mafundisho
mazito, maonyesho na kiini macho, na hivyo imesababisha uungwaji mkono mkubwa.
Hata hivyo wakati kila kitu kilipokuwa kinaenda kulingana na mipango ya wafuasi wa Darwin, na
wakati ambapo watu walianza kupagawishwa na kiini macho hiki, na wakati ambapo
ilikuwa inakaribia kuwa ni uhalifu kupinga mabadiliko ya kimaumbile, mara watu
wakapata mwangaza wa jua. Jua hilo lilikuwa ni Atlasi ya uumbaji.
Kutokana na kusambaa kwa haraka kwa Atlasi ya uumbaji duniani, haikuwezekana tena
kuwashawishi watu kuwa kulikuwa na mabadiliko ya kimaumbile. Hakukuwa na hata
mfuasi wa Darwin mmoja aliyeweza kukana maelfu ya mabaki ya viumbe hai
yaliyoonyeshwa kwenye Atlasi
ya uumbaji. Kwa kuongezea ni kwamba, moja wapo ya mabaki haya
yaliyoonyeshwa ndani ya kitabu hiki bora yalikuwa yanatosha kuangamiza
mabadiliko ya kimaumbile.
Kutokana na sababu hiyo, vyombo vya habari vya Ufaransa, ambavyo
ni moja wapo ya ngome za nadharia ya Darwin, zilipata hofu mbele ya Atlasi ya uumbaji, huku
vikisema maneno kama vile; “Janga kubwa kwenye historia ya Ufaransa”, “Janga
limeshuka kutoka angani” na “Miaka yetu mia moja ya ustaarabu imeanguka”.
Bunge la Ulaya lenye kukubaliana na nadharia ya Darwin
lilikichukulia kitabu hiki kuwa kikwazo kikubwa katika ufundishaji wa
mabadiliko ya kimaumbile, na ilifanya jambo hili kuwa la mtafaruku mkubwa;
mamia ya mashirika ya habari yaliyokuwa wafuasi wa Darwin walilazimika
kukubaliana na athari ya atlasi hii duniani.
Atlasi Ya Uumbaji Ilisaidia Kuwapa Nguvu Waumini Wote
Kusambaa duniani kwa ukweli kutoka kwa bwana Oktar kuwa hakuna
hata protini moja inayoweza kuzalishwa kwa bahati nasibu na kuthibitisha kwake
kwa kutumia atlasi ya uumbaji,
kuwa mamilioni ya maumbile ya viumbe hayajabadilika imekuwa ni juhudi yake
muhimu katika kumaliza nadharia ya mabadiliko ya kimaumbile hivi leo. Ni jambo
la kushukuru kwamba kutokana na mafanikio haya, waislamu waaminifu, wakristo na
wayahudi wameweza kujitokeza na kupinga kwa uwazi na kwa ujasiri. Baadhi ya
waumini waaminifu, ambao mwanzoni hawakuweza kujiingiza kwenye juhudi yoyote
ile, walianza kupata nguvu kutokana na muamsho wa kazi hii muhimu.
Baada ya juhudi kubwa na nzuri ya bwana Oktar iliyolenga kufuta
kabisa nadharia ya mabadiliko ya kimaumbile, imewezekana kufanya mikutano ya
kuonyesha uongo wa nadharia ya mabadiliko ya kimaumbile na kuwahamasisha watu
waamini upweke wa mwenyezi mungu ndani ya vituo vya kijeshi vya marekani, na
kuutangaza ukweli huo katika mabasi yaliyoandikwa “Mungu yupo” ubavuni mwake
huku yakitembea katika mitaa ya london kwa uhuru.
Kutokana na kuamshwa na
juhudi hizi muhimu, MIKUTANO JUU YA UUMBAJI iliyohudhuriwa na maelfu ya watu
imefanyika ndani ya Canada, Marekani, Uswizi, Ubelgiji, Ujerumani, Australia na New Zealand, Ufaransa,
Denmark, Sweden, Indonesia na Malaysia, Singapore, Dubai na nchi nyingine
nyingi, wakati vituo vya luninga na magazeti ya duniani kote yameelezea
mafanikio haya makubwa.
Mara tu baada ya mafanikio haya makubwa, baadhi ya wafuasi wa
Darwin walipoteza imani yao juu ya dini hii ya kichawi. Hawana tena nguvu ya
kutetea uongo huu walioueneza kwa miaka mingi, au kuleta tena uongo mwingine.
Majarida
Ya Wafuasi Wa Darwin Yamekuwa Yakisitishwa Moja Baada Ya Jingine, Na Si Kwa
Sababu Ya Kifedha, Bali Ni Kwa Sababu Yamepoteza Imani
na machapisho yake yamekuwa yakipungua.
Machapisho ya wafuasi wa Darwin yaliyokuwa maarufu duniani ambayo yalikuwa
yakitoa taarifa juu ya madai ya ulaghai mpya au mwingine karibia kila wiki KWA
SASA YAMESHINDWA KUTOA HATA MOJA. Propaganda ya Darwin, ambayo ndiyo chanzo cha
nguvu za nadharia ya Darwin, imefikia mwisho. Wafuasi wa Darwin ambao walikuwa wakiibua nadharia hii ya
mabadiliko ya kimaumbile katika sehemu mbalimbali kwa kutumia mbinu mbalimbali
za propaganda kwa sasa wamekuwa kimya na hawataki kuaibika zaidi.
Mlango Wa Kuelekea Kwenye Ukombozi Kutoka Kwenye Pigo La Nadharia
Ya Darwin Uko Wazi Daima
Dini zote za uongo na kishirikina zinaugulia maumivu ya kuanguka
katika saa za mwisho ambazo tunaishi, na ambazo Hazrat Mahdi (amani iwe juu yake) na
nabii Issa (amani iwe juu yake) watarudi. Hakuna mtu atakayeweza kuzuia
uangukaji huo. Hii ni kanuni ya Mwenyezi Mungu. Katika zama hizi, Mwenyezi
Mungu analeta maangamizi haya ya wazi kwa kupitia kazi za bwana Oktar. Wale
wote waliomuamini Darwin bila ya kufahamu mapema watakuja kufahamu namna
walivyokuwa wamedanganywa, wakati huo wafuasi wa Darwin watajuta kutokana na
kujikuta kwao ndani ya nafasi ya uongo. Lakini bado hawajachelewa, bila shaka,
hawana budi kujitokeza na kutetea ukweli huu, kwani kukubali kwao makosa na
kushindwa ni wema mkubwa. Kwa hiyo, wafuasi wote wa Darwin ambao wametambua
uongo wa nadharia ya Darwin, bila shaka wana nafasi ya kusahihisha kosa hilo baya walililolifanya katika maisha
yao hali ya kuwa bado wanaishi hapa duniani.
No comments:
Post a Comment