Hakika mwanamke mwema anatakiwa amlaki mumewe
mlangoni wakati arejeapo jioni toka katika mishughuliko yake ya kila
siku hali ya kuwa ni mwenye tabasamu tele usoni, na asubuhi yuatakiwa
kumsindikiza mumewe hadi mlangoni aendapo kazini na amwache akiondoka
kwa tabasamu huku akimpatia maneno mazuri yenye kuvutia.
Anatakiwa kuandaa mazingira ya kumfanya mumewe apende kurudi mapema nyumbani
mara amalizapo kazi. Awapo nyumbani anatakiwa awe msafi na mwenye
kupendeza hata ikiwa ana watoto kede, ili asimkirihishe mumewe endapo
atarudi ghafla nyumbani. Mke anatakiwa kujiepusha na kila kile
kisichopendwa na mumewe,,,kwakuwa endapo mwanaume atakosa kuona kile
akipendacho kwa mkewe, moyo wake unaweza ukashawishika kirahisi kutafuta
yaliyokatazwa, ambayo yanaweza yakatia doa furaha na utulivu wa
familia. Mwanamke mwenye busara hujitoa mwenyewe kwa mumewe mpendwa kama
ua zuri la waridi lichanuapo.
Inshallah Kwa Hayo Na Mengine Mengi...
Kaa Tayari Kusoma Kitabu Changu Cha Nyumba Yenye
Amani, Pepo Duniani. (kitatolewa
bure
No comments:
Post a Comment