Monday, April 16, 2012

Maisha Katika Familia Ya Kambo

Baba, Mama, Mtoto Wa Kambo

Namna Familia Za Kambo Zinavyoweza KufanikiwaMatatizo Ya Pekee Ya Familia Za Kambo

Hakika haitafaa kutatua matatizo ya familia za kambo kwa kutumia mashauri yaleyale yanayopewa familia za kawaida. Kwani kufanya hivyo ni kama kujaribu kutafuta njia katika barabara ya jiji moja kwa kutumia ramani ya jiji lingine.

Ukweli ni kwamba zaidi ya kuwa na matatizo ya pekee, familia za kambo zina matatizo mengi kuliko yale ya familia za kawaida. Mwanasaikolojia mmoja, anasema kuwa familia yak ambo ndio “Uhusiano tata, usio wa asili, na mgumu zaidi kati ya mahusiano yote ya wanadamu.”

Ikiwa hali ni ngumu hivyo, familia wadhani familia yak ambo itawezaje kuwa na mafanikio? Mahusiano katika familia za kambo yanaweza kufananishwa na kitambaa kikubwa kilichoshonwa kwa kutumia vitambaa vidogo vidogo tofauti tofauti. Vinapoanzwa kushonwa kwa pamoja, huenda mshono huo ukawa dhaifu, lakini unapokamilika, unakuwa na nguvu-ikiwa vitambaa hivyo vilishonwa kwa uangalifu.

Acheni tuchunguze baadhi ya matatizo ya kawaida ambayo hukumba familia za kambo na hata ambazo zimesaidia wengi kuunganishaidia maisha yao. Kisha tutasoma kuhusu baadhi ya familia za kambo ambazo zimefanikiwa.

TATIZO LA KWANZA

MATARAJIO YASIYOTIMIZWA

Nilitarajia ya kwamba nikiwapend watoto wangu wa kambo na kuwajali sana watanikubali na kunipenda penda pia, lakini bado hadi sasa halijawa, Huenda kuwa na familia yak ambo iliyo na umoja ikaonekana kuwa ni ndoto, tena ya mchana kweupe.

Familia nyingi za kambo huanza zikiwa na matarajio makubwa. Wazazi hutarajia kwamba wataepuka na kurekebisha makosa yaliyofanywa katika ndoa zao za kwanza na watapata upendo na usalama ambao ulikosekana katika ndoa hizo. Ingawa huenda matarajio mengine yasiwe halisi, bado yanaweza kumfanya mtu afadhaike yasipotimia. Waswahili wanasema “Tarajio lililocheleweshwa linafanya moyo uwe mgonjwa.” Ufanye nini ikiwa matarajio uliyokuwa nayo hayajatimia na moyo wako wazidi kuumwa?

UNACHOWEZA KUFANYA


Usiupuuze hisia zako kwa kudhania kwamba ipo siku utaacha kukata tama. Badala yake, chunguza ni matarajio gani yasiyotimia yanayokufanya utamauke. Kisha chunguza ni kwa nini ulitarajia jambo hilo ili uelewe ni kwanini unashikamana nalo. Mwishowe, jaribu kutafuta jambo linaloweza kutimizwa kwa sasa. Ona mifano ifuatayo:


1. Tangu Mwanzo, nitawapenda watoto wangu wa kambo nao watanipenda. Kwa kuwa siku zote nimekuwa nikitamani kuwa na familia changamfu na yenye uhusiano mzuri wa karibu. Baada ya muda upendo wetu unaweza kukua. Jambo muhimu kwa sasa ni kwamba tujihisi tukiwa salama na tuheshimiane katika familia.

2. Kila mtu katika familia atazoea hali haraka. Kwakuwa yupo tayari kuanza maisha mapya. Ambapo familia za kambo huchukua kati ya miaka mine hadi saba kuimarika. Matatizo yao ni ya kawaida.

3. Hatutazozana kuhusu pesa, Upendo utasaidia wanafamilia wa kambo wasibishane kuhusu mambo madogo madogo. Masuala ya kifedha yanayohusiana na ndoa zetu za awali ni mazito. Huenda isiwe rahisi kushirikiana katika matumizi ya pesa.

TATIZO LA PILI

KUELEWA HISIA ZA WENGINE

Huenda watu katika familia za kambo wasielewe kabisa maoni ya wengine katika familia zao. Kwanini hilo ni muhimu? Matatizo yanapotokea, huenda ukataka kuyatatua kwa haraka. Lakini ili ufanikiwe kuyatatua lazima kwanza uwaelewe watu wa familia yako.
Ni muhimu kufikiria jinsi unavyozungumza, kwakuwa maneno yanaweza kujenga au kubomoa. Kifo na uzima vipo katika nguvu za ulimi. Unawezaje kuutumia ulimi wako ili kuwasaidia wote waweze kuelewana.

UNACHOWEZA KUFANYA

Pendezwa na wengine na uwe na hisia mwenzi au mbadala badala ya kuhukumu. Mfano:
Mwanao akisema “Ninamkosa baba yangu,” kubaliana naye. Badala ya kusema “Lakini baba yako wa kambo anakupenda na kukujali kuliko baba yako mzazi. Unaweza ukamwambia, Lazima upitie hali ngumu, hebu nieleze, ni nini hasa kinachokufanya umkose baba yako?
Badala ya kumlaumu mwenzi wako mpya wa ndoa kwa kusema, “Ikiwa ungekuwa mzazi mzuri motto wako angekuwa na adabu zaidi,” mweleze hisia zako. Unaweza kumwambia: “Tafadhali mkumbushe mtoto awe akinisalimu na kuniamkua anapkuja nyumbani, hilo litanifanya nijihisi vizuri?”

Jaribuni kufahamiana zaidi wakati mnapokula, wakati wa tafrija na wakati wa ibada kwa mujibu wa imani zenu

itaendelea,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment