Friday, November 9, 2012

HATUA 101 KATIKA ELIMU


Kutoka katika maneno mazuri zaidi
Kutoka katika QUR’AN TUKUFU

“…….…Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe………” (28:77)

“Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema” (Umiliki wa maisha, uwezo na njia zote za maisha).
(102:8)

















1.
Elimu huanza kutolewa ndani ya tumbo la mama.
                Kwahiyo Mwalimu wa kwanza wa mwanadamu ni mama yake mzazi.

2.
Watoto ni Baraka toka kwa Mwenyezimungu walizokabidhiwa wazazi  na walimu ili wawapatie tabia njema na mwenendo wa hali ya juu.

3.
Mwenendo mwema, tabia za kupendeza na utu ndio urithi bora zaidi ambao wazazi wanaweza kuwaachia watoto wao.  Na njia ya kufikia haya hupitia katika elimu yenye ubora wa hali ya juu.

4.
Miongoni mwa viumbe, ni wanaadamu ambao huhitajia zaidi elimu. Sanaa nzuri zaidi katika maisha ni kuongeza wanadamu wema. Mwenyezi mungu Mtukufu alimtuma Mtume kuwa Mwalimu bora zaidi wa wanadamu. Kwa maneno mengine, Kazi ya Ualimu ni taaluma ya utume.

5.
Mwalimu sio tu mtu yeyote mwenye kutoa taarifa kuhusiana na somo Fulani, bali pia ndiye mwenye kupanda mbegu ya usafi wa moyo, mwenye kufungua upeo mpya wa macho, hualika katika akili ya kawaida, na hufundisha mwenendo mwema na kufanya yaliyo sahihi. Kwa maneno mengine, mwalimu hutengeneza sauti yenye dhamira kwa mwanafunzi.


6.
Katika hali ya kumkuza mototo, haitoshi kumpatia pahala pa kulala na chakula cha kukila. Kitu kitakiwacho hasa ni madoido ya akili na ulimwengu wake wa kiroho kwa kumpatia taaluma na kujifunza.

7.
Mwalimu analazimika kuwaelimisha wanafunzi wake kuhusiana na masuala ya kiroho. Pia atatakiwa kuelekeza malengo ya wanafunzi wake, yasiwe ni yenye kuelekea katika ulimwengu wa kisayansi pekee, bali pia yaelekee katika mafundisho ya kidini, kiroho na hekima.

8.
Endapo yeyote atapatiwa elimu ya upande mmoja (mazingira) pasi na kupewa elimu ya kiroho ni sawa na bure. Ni muhimu kuweka mlingano kati ya elimu ya ulimwengu wa kimaada na ulimwengu wa kiroho. Vinginevyo, ni itakuwa ni kama ndege arukaye kwa bawa moja, mwanafunzi atakuja kuwa chakula cha paka mwenye njaa.

9.
Kwa kila kiumbe ambacho hakiwezi kwenda sambamba na mwenendo wa maisha, itakuwa si rahisi kwa kiumbe hicho kuzuia kupotea kwa wakati. Hii ndiyo sababu Ali (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe pamoja nae) ametupatia ushauri ufuatao:
“Usimlee mtoto wako kulingana na zama au kipindi ama namna ulivyolelewa wewe, lakini unatakiwa kumlea kulingana na zama atakazoishi mtoto huyo”
                                                                                               
10.
Endapo taifa litafanikiwa kuwa na vijana waliofundishwa vizuri na kuwa na moyo wenye upendo, taifa hilo litakuwa na nguvu kubwa kulinganisha na mataifa mengine; vinginevyo, itakuwa ni kinyume chake.


11.
Si jambo la kustaajabisha au la muujiza kuweza kufahamu mustakabali wa taifa Fulani. Ili kufanikiwa hilo, inatosha kuangalia mwenendo wa vijana na watoto wa taifa hilo. Ikiwa wanatumia nguvu na vipawa vyao katika mambo mema na mazuri, maswala ya kiroho, na uchajimungu, fahamu kuwa mustakabali mzuri wenye kung’ara unalisubiri taifa hilo. Kwa upande mwengine, endapo watatumia nguvu bila ya mpangilio na kuyafurahia matamanio yao binafsi, mustakabali wao utakuwa ni wa kuhuzunisha.

12.
Wale walio na mitaji na wakawa wanatafuta sehemu nzuri zaidi kwa ajili ya kuwekeza. Elimu, pamoja na kuwa, ndio sehemu nzuri zaidi kiuwekezaji. Maandalizi yaliyo sahihi zaidi kwa ajili ya mustakabali wa baadae ni kukuza watu wenye uhitimu na ubora katika tunu za kibinadamu.

13.
Jambo la kwanza ambalo mwalimu anapaswa kuliweka kwa mwanafunzi ni tabia itayomfanya mwanafunzi apongezwe awapo mbele ya wanafunzi wenzake; na atatakiwa kusambaza nuru ya taaluma, roho iliyosafika, na vipawa chanya toka ndani ya moyo wake, na hatimaye atatakiwa kububujisha mafuriko ya huruma na upendo kwa wanafunzi wake.

14.
Ni jambo gumu mno kwa mwalimu kumshawishi mwanafunzi wake kumsikiliza endapo vitendo vyake vinapingana na maneno yake. Kama anavyosema Mturuki maarufu mwenye hekima Bwana Ziya Pasha:
“Kazi za mtu ni kama kioo kinachoonesha mwenendo wake; hivyo asije yeyote akadanganyika na utamu wa maneno.”

15.
Mwalimu kabla ya yote anatakiwa apambe maisha yake yote na wema ambao anaushauri na kuunasihi kwa wengine na atapaswa kujitahidi yeye mwenyewe awe ni mfano ulio hai.

16.
Ni muhimu kwa mwalimu kuenezo vipawa chanya vinavyowazunguka. Katika kuliendea hili hata baadhi ya mifano toka katika maisha ya wanyama yanaweza kupigiwa mfano: Kuku huwalinda vifaranga wake kwa kuwahifadhi chini ya mbawa zake wakati anawalea. Nyoka huwalea vijana wake kwa mtazamo wake. Nge humbeba mtoto wake mgongoni. Wakati wanyama hulea watoto wao kwa uangalifu wa hali ya juu, vipi mwanadamu anatakiwa kuwa?

17.
Katu haiwezi kupatikana elimu yenye ubora wa hali ya juu ikawa hakukupatikana imani ya kutosha kati ya mwalimu na mwanafunzi. Mwalimu, juu ya yote, anatakiwa awe na uwezo wa kuonesha tabia za hali ya juu wa ubora kwa watu wanaomzunguka kwa sababu watu hupambika na tabia njema na huheshimika kwakuwa na utu. Hufuata nyayo za watu wa aina hiyo.

18.
Raia huwa kulingana na walivyo watu wanaowaongoza. Zama za furaha na neema (Asr Sa’adah) ziliundwa na roho njema ya Mtume (s.a.w).
Maswahaba wa Suffa ni mfano bora katika hili. Abdullah b. Mas’ud, Mmoja miongoni mwa maswahaba wa Suffa, alisema akionesha kiwango cha utimilifu alichofikia kutokana na mafundisho ya Mtume:
 “Tuliweza kusikia ukumbusho (Dhikr) wa kitoweo kilipokuwa kikienda chini kooni.” 

19.
Mikusanyiko ya kiroho (Suhba) kupeana mashauri ya kidini ilikuwa ndio njia muhimu zaidi ya elimu katika zama za Mtume, Kulikuwa kunapatikana muunganiko mkubwa zaidi wa kiroho kupitia mikusanyiko hii. Aina hiyo ya mikusanyiko hunyunyiza rutuba inayohitajika ndani ya nyoyo za waliohudhuria. Kuwa na aina hii ya mazungumzo na mikusanyiko ni sawa na kuandika dawa kwa maradhi yao.

20.
Mwalimu anapaswa kuangalia uwezekano ambao mwanafunzi kautegemeza kwake anaweza kuwa ni kiungo maarufu na muhimu baadae; na pia hatakiwi kusahau kuwa baadhi ya watu muhimu wanaoweza kuja kuubadilisha ulimwengu huenda wakawa ni miongoni mwa anaowalea hivi sasa.

21.
Ili uweze kutoa huduma yenye ubora wa hali ya juu, mwalimu pia anapaswa kuwa makini zaidi na maendeleo yake binafsi. Nguvu ya muendelezo wa mafanikio inapendeza itokane na tabia yake. Vinginevyo, zawadi na vipaji vingi vinaweza vikapotea kutokana na uzembe wake.

22.
Kizazi kilichohitimu ni zao la walimu waliohitimu ambao wanao uwezo wa kutoa taaluma na mwenendo mwema. Wote wanaofundishwa na wazembe na walimu wasiohitimu wataangukia katika uzembe na watu dhaifu.

23.
Endapo tunatamani kukuza wanafunzi waliokamilika, tunatakiwa kwanza tuwe ni walimu tuliokamilika.

24.
Kitu kilichokarabatiwa ni kadi ya biashara ya mwenye kukarabati. Vivyohivyo, ubora wa mwalimu unaweza kuthaminishwa kutokana na ubora wa mwanafunzi aliyefundishwa na mwalimu huyo.

25.
Ni jambo la muhimu zaidi kwa mwalimu kujifundisha yeye mwenyewe kwanza, kwa mwalimu masikini itakuwa ni kupoteza muda wa wanafunzi waliojitegemeza kwake.

26.
Mchungaji huwajibika kwa ng’ombe wake. Mchungaji atatakiwa kumbeba ndama ambaye mguu wake umevunjika. Vivyohivyo, wanafunzi ni deni la mwalimu wao.

27.
Kila mmoja anaamini kwamba maneno yao ni muhimu na yenye nuru na yanawataka kuyachukua. Hii ndio sababu mwalimu anatakiwa kuwa makini kumsikilza mwanafunzi anayeulizia msaada kuhusiana na tatizo linalomkabili.

28.
Mwalimu anatakiwa amchukulie mwanafunzi wake kwa umakini, amuoneshe heshima, na anapaswa kumfanya mwanafunzi ayahisi haya yote kupitia matendo yake.

29.
Mwalimu anayewageuzia wanafunzi wake katika kijimsitu kidogo ambaye anauwezo wa kuwa mti mkubwa kwa hakika atakuja kuwajibishwa mbele ya Allah.

30.
Mwalimu anatakiwa kuwafahamu wanafunzi wake wana tabia zipi ndipo ataweza kuukamata mshipa utakaomfikisha katika nyoyo zao.

31.
Kwakuwa tabia na utu hutofautiana, mbinu au sehemu ya ushauri inaweza kumnufaisha mwanafunzi mmoja, ilhali aina hiyo hiyo ya mbinu au ushauri unaweza ukamdhuru mwanafunzi mwengine. Hii ndiyo sababu mwalimu anapaswa kufahamu hali ya kiroho ya mwanafunzi wake.


32.
Mwalimu anatakiwa kufahamu tunu na kipaji alichonacho mwanafunzi wake kama anavyoweza kuzifahamu vipande vya Tasbihi yake, kuwa na uwezo wa kuwaongoza wanafunzi wake kuelekea katika vipaji vyao.

33.
Zama hizi tunaishi katika kipindi ambacho watu wameparaganyika kama vipande vya mbao katika maji yanayitiririka kwa kasi. Cha kuhuzunisha zaidi, Mto unaoweza kuleta uhai katika ardhi unapita ukitiririsha maji yake katika mfereji wa maji machafu kwa wale wasioongozwa katika muelekeo ulio sahihi.

34.
Mwalimu anapaswa kuwa na huruma, na kuwahurumia wanafunzi wake. Hata kuwawajibishwa kwa mambo ambayo hawana uwezo wa kuyabeba. Atatakiwa kumhukumu kila aliye chini ya uwezo wake.

35.
Mwalimu bora ni Yule mwalimu wa darasa zima. Hakuwezekani kupatikana amani katika darasa pasi na uadilifu; katika darasa lilikosa amani, hakuna somo linaloweza kufundishwa; katika maeneo ambayo hakuna somo lifundishwalo, katu hakutapatikana aina yoyote ya elimu.

36.
Mwalimu anatakiwa kufahamu vizuri kabisa kuwa uadilifu haumaanishi kuwafanya na kuwatendea wote sawa sawa bali ni kuwapatia vile wanavyostahiki kuvipata. Mwalimu pia anatakiwa kujiepusha na tabia zote ambazo zitadhuru hisia za uadilifu wa wanafunzi.



37.
Mwalimu anatakiwa kuwa mtenda haki, si katika kutoa hukumu tu, bali pia katika kusahihisha mitihani. Kwa kifupi, anatakiwa kutenda haki kila wakati katika kila jambo.

38.
Mwalimu anatakiwa kuweka mipango kulinga na muuondo wa darasa na zana za kufundishia za somo alizonazo hivyo ataweza kufundisha kwa ufanisi.

39.
Mwalimu aliyejipanga vizuri na kuandaa mikakati yake ipasavyo anaweza kuona pale alipoishia kabla, kile alichofundisha, na amepata mafanikio kwa kiwango gani.

40.
Pindi anapopanga na kuandaa mipango na mikakati, mwalimu lazima afikirie juu ya wakati gani, wapi, na vipi atatumia mbinu za kufundishia anazoziandaa.

41.
Mwalimu ni lazima afahamu kuwa wajibu wake hauishii tu katika kuhamisha taaluma toka kwake kwenda kwa mwanafunzi wake. Wakati anapanga masomo yake,  mwalimu atatakiwa kuandaa sehemu ambazo zitamvutia na kuvuta umakini wa mwanafunzi wake. Awasilishe somo kwa kutoa mifano inayoakisi uhalisia wa maisha na kutoa mbinu na njia ya S na J (Swali na jibu) vitamfanya mwanafunzi kuwa makini na mfanisi.

42.
Subira, uvumilivu, na kujinyima ni funguo bora zaidi kufikia mafanikio ya kielimu.



43.
Mwalimu hatakiwi kukata tama anapokabiliana na mambo magumu na chamoto; kinyume chake uvumilivu utakomaa na utafikia kiwango cha juu zaidi katika kipindi cha hali ngumu.

44.
Kwasababu ya madhaifu na upungufu wa maana, mwalimu hawezi kupoteza matumaini au kuonesha kukosa uangalifu na kukosa nguvu au kupungukiwa uwezo.

45.
Ni muhimu kutokusahau maji ya uhai kwa kawaida hufichwa katika zama ngumu na maeneo yenye tabu; kwa vile vinavyoyapa thamani na mafanikio maisha ni nguvu na kujitoa katika njia ya kukubali malengo matukufu.

46.
Elimu sio mapenzi ya muda mfupi. Ni swala la kujivunia katika uwajibikaji ambapo utajazwa na upendo na ukarimu hadi pumzi yako ya mwisho. Katika hali hii ya huruma kutakuwa na kunyweshwelezwa na mwalimu na Mwenyezi Mungu atamuwezesha.

47.
Mwalimu ni mtu anayeweza kuilinda na kuichunga imani yake katika aina yoyote ya jamii aliyopo; ambaye atauweka mbali moyo wake kuepukana na mali na maslahi yake; ambaye anaweza kusikia sauti zilizonyamaza za wenye mahitaji ya elimu.

48.
Ni kana kwamba makosa kutekeleza watoto wa mto, wazazi wa mtu, utaalamu wa mtu kwa ajili ya kupata riziki yake kwa msamaha wa kuokoa wengine, ni makosa pia kuyafanya hayo kuwa ndio sababu ya kukwepa kuwasaidia wengine.

49.
Mwalimu hatakiwi kujisikia huzuni  kwa kukosa nafasi ya kupata mali, pia asiwe na furaha kwa kuharibikiwa na wingi wa umiliki wake wa ulimwengu.

50.
Mwalimu atatakiwa kutenga muda kwa ajili ya wanafunzi wake nje ya muda wa kawaida wa masomo darasani. Hatakiwi kuwa kama mfanyakazi anayeangalia saa kila wakati na baadhi ya nyakati akiisogeza mbele ili afike muda wake wa kutoka kazini.

51.
Mwalimu hatakuwa kuwa mtengenezaji wa matatizo bali anatakiwa awe ni mtatuzi wa matatizo. Badala ya kuangalia makosa na mapungufu kwa kuyakosoa, anatakiwa awe na uwezo wa kutatua matatuzi kwa roho na mtazamo ulio mwema.

52.
Mwalimu hatakiwi kuwalaumu wengine kwa kufanya makosa wakati yeye akiendelea kufundisha; anatakiwa ajiangalie yeye mwenyewe kama ndio chanzo cha makosa hayo.

53.
Kwa mwalimu, kuangazia sasabu kwa kusema “Nitafanya nini sasa? Sina kipaji. Hizi ni nyakati zilizopotea. Hakuna yeyote anayekuja katika madarasa yangu,” Mwenyezi Mungu hujibu sababu kama hizo kwa kuumba Mitini nje ya kuta za miamba na kuzalisha matunda kwa ajili yao.

54.
Elimu ni sanaa ya kusahau sababu kabla ya kukutana na aina zote za sababu. Elimu haiwezi kufikiwa pale ambapo kutokuvumilia na sababu zinakuja.


55.
Mwalimu mzuri hasubiri nafasi na uwezekano umfuate alipo. Kila siku anatakiwa kutafuta njia za kusaidia wengine.

56.
Elimu si taaluma ya kukaa na kusubiri. Inahitaji kiwango kikubwa cha nguvu. Kwahiyo mwalimu ni lazima aujaze moyo wake kwa nguvu chanya.

57.
Mbegu za taaluma iliyopandwa kwa upendo na shauku itakuja kuwa Mti Mkuyu mkubwa hapo baadae.

58.
Mwalimu anatakiwa kufahamu vyema mwenendo mwema unaokubalika na kuheshimiwa na jamii na hatakiwi kuwadharau.

59.
Mwalimu mwenye moyo mwema, wenye heshima na fahari atawasaidia wengine kwa furaha ya unyenyekevu; katu hawezi kuumiza hisia za wengine na katu hawezi kusababisha hisia zake zikaumizwa kirahisi. Haitakiwi kusahaulika kwamba nyoyo ndio eneo la uoni wa uungu.

60.
Mwalimu anatakiwa kuwa makini na mwangalifu mno katika kila tendon a tabia yake. Anatakiwa kuwa mpole mwenye heshima hata wakati anapofanya utani.



61.
Mwalimu mzuri ni lazima afahamu mipaka sahihi iliyopo kati ya majivuno na heshima, udhalilishaji na soni. Hatakiwi kuchanganya kati ya mambo yanayofanana.

62.
Mwalimu anatakiwa kujitahidi na kuendea kila hatua ya maisha yake katika njia iliyo nzuri ya maadili ya uisilamu. Hatakiwi kusahau kuwa kila moja miongoni mwa matendo yake na kila moja mipongoni mwa maneno yake ni sawa na matofali yanayowekwa na kujengwa katika mwenendo wa wanafunzi wake.

63.
Mwalimu anapaswa kufahamu kuwa elimu si kuhamisha maalumati toka kwa mmoja kwenda kwa mwengine, bali pia ni kusafirisha tabia. Atatakiwa pia kufikiria juu ya makosa na madhaifu ambayo yanaweza kunakiliwa wakati anahamisha  maalumati kwenda katika fikira ya mwanafunzi wake na anatakiwa siku zote auhisi wajibu wake wa uhamishaji katika matendo na tabia zilizokuwa zakupendeza.

64.
Mwalimu anapaswa kuwa ni mtu wan yoyo ambae anajitahidi kupata msamaha wa muumba kwa kusamehe wengine.

65.
Kila mmoja anahitaji la upendo na huruma. Kuonesha huruma na upendo kwa wanadamu kunapunguza maadui na hasama na kunaongeza upendo na rundo la marafiki wema.
66.
Elimu iliyo sahihi haiwezi kujazwa na kiburi, kuvunja mioyo, na njia za ukatili.


67.
Katu haiwezi kukubalika kwa mwalimu kuwafanyia jeuri wale wote waliokuwa chini ya amri yake kwa ajili ya kuwaadabisha.

68.
Ukatili uliopindukia hutengeneza hali ya kinyongo na chuki.
Uvumilivu uliopindukia hudhoofisha mamlaka.
Mafanikio yanaweza kupatikana tu kwa kuweka mzani sawa baina ya vitu hivyo.

69.
Mwalimu anatakiwa kusema maneno yake kwa uzuri na upole na siku zote azungumze kuhusiana na wema. Kwakuwa hakuna anayependa maneno makali nay a ujeuri. Upole, uzuri, na utamu wa mazungumzo ni njia nzuri ya kuziingia nyoyo.

70.
Ni kama ilivyo kwa rubani ambaye hayuko sawa hawezi kuruhusiwa lkurusha ndege, vivyo hivyo, mwalimu mwenye hasira au ambaye hayupo katika hali nzuri asiruhusiwe kuingia darasani.

71.
Mwalimu atatakiwa kuweka maonyo yake na kutoa ushauri na nasaha zake katika njia ya amani na hatakiwi kusahau kuwa matendo na tabia yanayoumiza ni madhaifu na mapungufu makubwa mno ya kibinadamu yanayopaswa kuepukwa muda wote.l

72.
Wanadamu siku zote huwa chini ya miongozo ya hisia zao. Wanafikiria na kufanya chini ya miongozo yao. Kwahiyo, Mwalimu bora siku zote hufanya maamuzi baada ya kushauriana na wenzake. Hilo humsaidia mwalimu huyo kutoa huduma sahihi.

73.
Athari ya mwalimu ambae moyo wake umejazwa na upendo na usafi war oho ni sawa na athari za upepo upepeao katika bustani iliyojaa maua yenye harufu nzuri na kuchukua uturi wao mzuri na kuupeleka maeneo ya mbali.

74.
Ulimwengu huu utaweza kubadilika na kuwa kama peponi kwa mambo matatu: Kwa kububujishwa huruma kupitia mikono yako, ulimi wako, na moyo wako …

75.
Ili kufikia wokovu, waumini waliokomaa huwatafuta wenzao katika jamii zao na kuwapatia elimu, huduma, na huruma ili kuwaokoa.

76.
Ushindi wa kweli ni ushindi wan yoyo. Na hili litaweza kufikiwa tu kwa wale wanaogeuza nyoyo zao katika upendo.

77.
Mwalimu wa kuigwa ni mtaalamu wa nyoyo. Yeye ni daktari anaetibu nyoyo kwa chanjo ya maisha ya milele.

78.
Moyo wa mwalimu utaelekea katika kituo cha kiroho kwa kujipa muda wa kupata uwezo wa kuangalia viumbe kwa uoni wa muumba.



79.
Upendo na Uchapaji kazi hutatua matatizo yote.
Tunawapata watu ambao matatizo yao tumeyatatua. Tunapata malipo ya kiroho kwa kila tuliyefanikiwa kumpata na kuchukua jukumu kubwa la kila ambaye tumempoteza.

80.
Mhanga ni kipimo cha upendo.  Kuzungumza tu hakuna maana yoyote. Mawlana Jalaludin Rumi anasema:
“Usiwe mpumbavu wa maneno.” Kilele cha upendo kinatakiwa kuthibitishwa kwa mhanga.

81.
Mwalimu anatakiwa kuyahisi maumivu ya wanafunzi wake na afurahi pamoja na furaha zao. Anapaswa kuwachukulia kama marafiki, kaka zake ama dada zake. Pia anatakiwa awe muangalifu katika suala la lugha ya urafiki na udugu.
82.
Mwalimu hatakiwi kuwa ni mtu mwenye kuangalia makosa na mapungufu ya wanafunzi wake pekee; hasa anatakiwa kuwa mtu anaye jaribu kusahihisha makosa yao pasi na kuwaamsha.

83.
Mapenzi ni kama njia ya umeme kati ya nyoyo mbili. SAuti ya elimu hutegemea na nguvu ya njia hii.

84.
Mwalimu analazimika kufungua milango ya moyo wake kwa wanafunzi kwa upana kiasi kwamba wanaweza kuanzisha njia madhubuti ya ushawishi.

85.
Upendo kwa mwalimu huongeza hamu kwa kila anachokifundisha. Kumfikia mwanafunzi kwa upendo na huruma humsaidia mwalimu kufikisha ujumbe wake, sio kupitia njia za sababu, bali ni kupitia njia za moyo.

86.
Mwalimu anatakiwa aende darasani kwake kwa unyenyekevu na heshima kana kwamba anakwenda katika nyumba ya ibada. Anapaswa kukumbuka kuwa zana muhimu zaidi ya kazi yake ni upendo na wema.

87.
Elimu ambayo haujafikia moyo katu haiwezi kuja kuwa busara wala hekima.

88.
Walimu hujenga taswira ya ulimwengu kupitia kwa watoto kama kiungo cha thamani zaidi, hii ni kwamba. Nyoyo na fikira zao. Kwahiyo, inawezekana kuwaita walimu “Watengenezaji wa baadae."

89.
Elimu na busara vinaweza kufundishwa vizuri na kuleta athari nzuri zaidi kupitia kuishi na wachamungu na wenye nyoyo safi. Zama mtu anapofikia hatua hii, huwaona wanafunzi wake kupitia jicho la upendo na huruma. Mbegu zilizopandwa kwa upendo na huruma huwa ni za daima.

90.
Ili kuja kuwa mwalimu mzuri, ni lazima mwalimu awe na hisia zilizokomaa kwa upendo na huruma.

91.
Wanafunzi wanastahiki kuangaliwa Kama ndege waliojeruhiwa na kulelewa kwa huruma na upendo. Kwa huruma na upole ni dawa zilizo na athari na nguvu kubwa zaidi kwa kukuza sauti ya nyoyo na akili.

92.
Huruma ni kanakwamba moto usiozimika katika moyo wa mwalimu.

93.
Ni ukandamizaji kwa wanadamu kuwafanya kama waalimu wale wote wenye kutafuta maslahi binafsi na kuwanyima huruma na upendo.

94.
Ni kama mandhari ya mawaridi na maua mengine ambayo huwafanya watu wakatili na wenye nyuso za kutisha kutabasamu, watu wanaowaongoza wenzao wanapaswa kuwa kama mawaridi na maua mengine. Wanatakiwa kuwa na uwezo wa kulainisha nyoyo zilizo yabisi na kuzifanya sura za kutisha kutabasamu.

95.
Jambo la muhimu zaidi ambalo mwalimu anatakiwa kulipa umakini mkubwa mno ni kufahamu kuwa makosa yanatokana nay eye mwenyewe na mafanikio yanatoka na muumba.

96.
Juu ya yote haya, mwalimu analazimika kuchukulia utaalamu wake kama neema na zawadi kwake. Ili kuonesha shukurani zake kwa neema hii aliyoneemeshwa, anatakiwa kuhisi jukumu la kujipa mwenyewe zana za kiroho na kimaada.



97.
“Ubinafsi” na “Umimi” wanatakiwa kuutoa na kuweka “Upendo” na “Huruma” kwa mwalimu.

98.
Maisha ya Mwalimu yanatakiwa kujikita katika usafi wa moyo, juhudi, na huduma pasi na majivuno.

99.
Kila siku ni mpya na kurasa safi katika kalenda ya maisha.  Ni juu ya mikono yako kujaza kurasa hii safi katika namna iliyo bora.

100.
Mwalimu anatakiwa kuchukulia kila hatua pamoja na wanafunzi wake kana kwamba ndio pumzi yake ya mwisho katika ulimwengu huu hivyo anatakiwa kutumia nafasi hiyo katika namna nzuri kadiri iwezekanavyo. Ni lazima ajihisi mwennye kushukuru na kuonesha shukurani zake katika matendo yake.

101.
Watoto wanahitajia mafunzo kutoka kwa wazazi wao na walimu wao na ilhali wazazi na walimu wanahitajia maombi toka kwa watoto na wanafunzi wao kama sadaka yenye kuendelea kuwepo (Sadaqa jariya) katika maisha ya akhera.






Kutoka katika muongoza bora zaidi wa elimu
QUR’AN TUKUFU na UTAMADUNI WA MTUME WA ALLAH
Maneno yaliyo bora zaidi nay a kheri kuliko yote ni kitabu cha Allah.
Hakika muongozo na njia iliyo bora zaidi ni njia ya Mtume wa Allah.
Uchamungu ndio makazi yaliyo na sauti nzuri.
Mazungumzo matakatifu ni kumkumbuka Allah.
Hadithi na habari za kuvutia zaidi zipo ndani ya Qur’an tukufu.
Njia yenye nuru zaidi ni njia ya miongozo ya mitume.
Elimu nzuri na yenye manufaa zaidi ni ile inayomfanya mtu kuwa na hekima na busara.
Mali ndogo ambayo inakufanya uweze kushukuru ni bora kuliko kuwa inayokunyima shukurani.
Maombia mabaya zaidi ya msamaha ni yale yanayoletwa wakati wa kufa.
Majuto mabaya zaidi ni yale yanayooneshwa siku ya hukumu.
Uongo ni dhambi kubwa zaidi.
Utajiri ulio bora zaidi ni utajiri wa moyo na kupata utajiri kupitia kuridhika.
Imani yenye thamani ni ile iliyohifadhiwa moyoni.
Ukwasi pasi na kutoa zaka na sadaka utakuwa ni aibu siku ya hesabu.
Madeni na riba ni vitu vibaya zaidi kuvipata.
Dhuluma na kiza kikubwa zaidi cha upofu ni kupotea njia wakati ulishakuwa katika njia iliyo nyooka.
Upofu mbaya zaidi ni upofu wa moyo.
Kumuongoza asiye muumini katika njia iliyonyooka (Uisilamu) ni bora zaidi kuliko kila kitu kichomozewacho na jua juu yake. Haya ndio matunda ya kuuelimisha moyo.
Ingawa kila aina ya ubaya ni ubaya wa kuzidiana mmoja kwa mwengine; ubaya zaidi ya wote ni “Ubaya wa mwanadamu.”


No comments:

Post a Comment