1. Usalama wa nafsi:-
Damu ya raia wasio Waislam ina thamani sawa na ya Waislam.
(a) Imesimuliwa na Omar bin Hassan kuwa Mwislam mmoja alimuua mwananchi asiye Mwislam. Taarifa hizi zilipomfikia Muhammad alisema ‘Mimi ndiye ninayewajibika kulinda haki yake’ kisha akaagiza kuwa Mwislam yule muuaji auawe.
(b) Wakati wa utawala wa Omar...
, mtu mmoja wa kabila la Bakr bin Wael alimuua raia asiye Mwislam kutoka Hira. Omar akaagiza kuwa muuaji apelekwe na kukabidhiwa kwa kabila la marehemu ambao waliamua kumuua.
(c) Wakati wa utaala wa Ali Khalifa wa nne Mwislam mmoja alikamatwa kwa mauaji ya raia asiye Mwislam na adhabu ya kifo ilihitajika. Ndugu wa marehemu alikubali kuchukua fidia na akamsamehe, kusikia hivyo Ali alitaka kujua kama ndugu huyo alikuwa ametishwa na familia ya muuaji na kushurutishwa kukubali fidia badala ya kutekeleza adhabu ya kifo. Lakini akamwambia Ali kuwa hapakuwepo vitisho vyovyote. Na hapo Ali akasema: “Damu ya yule aliyepewa dhamana ya ulinzi wetu ina thamani sawa na damu yetu na fidia yake ni sawa na fidia yetu.” (Rejea . Tabari – Uk. 2055, Tabari – Uk. 2050, The rights of the non-Muslim subjects cha Maududi – Uk. 13)
2. Sheria ya Uhalifu:-
Raia Waislam na wasio Waislam wote wana haki sawa mbele ya sheria. Huadhibiwa kwa kosa moja sawia, wizi, kuzusha uwongo na uzinzi. Lakini asiye Mwislam haadhibiwi kwa kunywa pombe.
3. Sheria ya Kiraia:-
Ali Khalifa wa nne anasema: mali zetu na mali zao wasio Waislam zina haki sawa mbele ya sheria. Wao wasio Waislam wanaruhusiwa kutengeneza pombe, kuziuza na kuzinywa. Wanaruhusiwa kufuga na kula Nguruwe kama Mwislam yeyote akiharibu pombe au Nguruwe yeyote anayemilikiwa na asiye Mwislam analazimika kumlipa fidia. Hii ni kwa sababu wao wameamua kufuata dini yao nasi tuna yetu hakuna kuwakera.
4. Utunzaji wa Heshima:-
Raia asiyekuwa Mwislam hatakiwi kudhuriwa kwa mkono au ulimi, hapaswi kupigwa, kutukanwa au kukashifiwa.
5. Kudumu kwa Agano:-
Makubaliano kati ya serikali ya Kiislam na raia wasio kuwa Waislam yanawashurutisha na kuwafunga waislam dhidi ya kuyavunja. Lakini raia wasio kuwa Waislam wana hiari ya kuyafuata au kuyavunja kwa utashi wao licha kosa au jinai yoyote kubwa inayotendwa na rais asiyekuwa Mwislam, bila kujali ukubwa wake, hili halivunji makubaliano hayo hata kama akimuua Mwislam au kutolipa kodi. Bali hapa ataadhibiwa kama mvunjaji wa sheria na hatazamwi kama mtu anayetakiwa kutengwa na taifa. Lakini vitu viwili pekee ndivyo vinavyoweza kuvunja agano hilo: Moja kuondoka katika taifa la Kiislam na kuungana na jingine katika kupigana vita dhidi ya na taifa jingine katika kupigana dhidi ya taifa hilo la Kiislam. Pili kuinua upanga hadharani dhidi ya taifa akikusudia kueneza uasi au mapinduzi.
6. Sheria binafsi:-
Raia wasiokuwa Waislam wana haki kamili ya kurejea kwenye sheria zao wenyewe wakati mmoja Khalifa wa Ki-bani Umayyah Omar bin Abdul Azizi, alimuandikia Imam Hassan Al Basri akitaka fatwa yake ya kwa nini Makhalifa wenye busara waliwaacha raia wasiokuwa Waislam kutumia sheria zao wenyewe za ndoa, Pombe na Nguruwe?
Hassan Al Basri akajibu akisema walitoa kodi ili waachwe wafuate imani zao wenyewe. Unatakiwa kufuata mfano wa wale waliokutangulia na hupaswi kuanzisha mambo yanayokwenda kinyume na mafundisho ya Uislam akaongeza akisema: wewe ni mfuasi sio mwanzilishi. Lakini ikiwa pande mbili, zisisokuwa za Kiislam, zitaiomba mahakama kutumia sheria ya Kiislam kusuluhisha tofauti zao basi mahakama lazima ifanye hivyo na kutumia sheria ya Kiislam. Lakini mmoja wao akiwa Mwislam na kesi yake inahusu sheria binafsi basi ni lazima kutumia sheria ya Kiislam.
7. Taratibu za kidini:-
Raia wasiokuwa Waislam wana uhuru kamili wa kutekeleza taratibu za dini yao katika majumba yao ya ibada. Serikali ya Kiislam haina haki ya kuingilia ibada hizo, vilevile wana haki ya kukarabati mahekalu yao.
8. Uvumilivu katika kuchukua kodi:-
Magavana wa Kiislam wanaamriwa kutowalazimisha raia wasio Waislam katika kuchukua kodi. Wanatakiwa kuichukua kwa upole na heshima hawatakiwi kushinikiza au kuuza mali zao ili kupata kodi hiyo. Khalifa wa nne Ali alimwandikia mmoja wa magavana wake akisema: katika kuchukua kodi usiuze Punda, Ng’ombe au Nguo yoyote ya mtu, si katika kipindi cha joto wakati wowote. Maulamaa wa Kiislam walitoa hukumu kwa wale waliokataa kulipa kodi ya kila mwaka kwa kuwaweka gerezani, lakini bila kuwapa kazi ngumu, na kwa kuwahudumia ipasavyo mpaka walipe. Yule aliye maskini sana sio tu kwamba anasamahewa kulipa kodi hii bali pia hupewa fungu lake kutoka katika hazina. Mtu akifa na deni la serikali kwa kutolipa kodi yake serikali haina haki ya kutaka kodi hiyo kutoka kwa warithi wala kutoka katika urithi wake Raia wasiokuwa Waislam wana uhuru wa kuelezea fikra zao, wana shule zao na wanaweza kufanya kazi za serikali isipokuwa kazi chache zilizo katika ngazi za juu, Waislam na wasiokuwa Waislam huamuliwa kwa sifa zao wana uhuru wa kujipatia pesa katika viwanda, biashara, kilimo au katika utaalam wao. Hivyo tunaona kuwa watu wasio Waislam waliishi chini ya mwavuli wa Uislam wakifurahia uhuru kamili, haki isiyokuwa na upendeleo na uhuru wa kuabudu, yote hayo yakitokana na mfumo wa Kiislam ambao msingi wake ni kumuogopa Mwenye-Enzi-Mungu katika shughuli zote na katika kutekeleza misingi thabiti ya Uislam.

No comments:
Post a Comment