Thursday, August 30, 2012

JUKUMU LETU KWA WATOTO WETU

Jukumu letu kwa watoto wetu

Ulimwengu ni makazi makubwa mno ya mitihani iliyopambwa kwa Baraka,vifungo, matarajio na raghba mbalimbali. Rasilimali za kidunia kama vile fedha, mali na watoto ni mitihani tuliyokabidhiwa ili tuwekeze kwa ajili ya Maisha ya baadaye. Kwa hivyo, ni muhimu kuzichukulia rasilimali za kidunia kama nyenzo za ustawi kwa ajili ya maisha ya Akhera. Qur’an Tukufu inatueleza:
“Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini.” (Kahf, 18: 46)
Wakati pesa, mali na watoto ni pambo zinapotumika katika njia ya Mwenyezi Mungu, pindi zinapotumika vibaya kwa ajili ya starehe na matamanio, baraka hizi zinaweza kumpeleka mtu kwenye njia ya taabu.
Walengwa wa karibu zaidi kwa Mwislamu ni watoto wake. Urithi pekee wa kweli ambao anaweza kukiachia kizazi chake ni neema za milele. Ni jukumu letu kuwaachia watoto wetu urithi wa daima, neema isiyonyauka wala kuisha, badala ya mali na furaha ya muda mfupi. Urithi wa milele ni Qur’an Tukufu na Sunnah tulizopewa na Mtume Muhammad (s.a.w). Kuhakikisha kuwa urithi huu mtakatifu unawafikia watoto wetu ni sababu kubwa ya wazazi kuendelea kupata thawabu, na kupuuza jambo hili ni sababu kubwa mno ya wazazi kupata adhabu na mateso katika maisha ya Akhera.
Mwenyzi Mungu Mtukufu anatuamrisha akisema; “Enyi mlio amini! Zilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe.” (Tahrim, 66: 6)
Mtukufu Mtume (s.a.w) naye anatuonya akisema; “Kila mmoja wenu ni mchunga na ataulizwa kwa alivyovichunga. Mwanaume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake na ataulizwa, na mwanamke ni mchunga wa nyumba ya mume wake naye ataulizwa”. Anasisitiza kuwa malezi na makuzi ya watoto ni jukumu shirikishi.
Katika hadith nyingine, Mtukufu Mtume (s.a.w) anasema; “Watendeeni wema watoto wenu na wafundisheni tabia njema.” (Ibn Majah, Adab 3)
Katika Hadith ifuatayo, Mtukufu Mtume (s.a.w) anaonyesha kuwa jukumu la malezi ya watoto ni bora zaidi kuliko hata Jihad, ambayo ni mojawapo ya amali zinazoheshimika sana katika dini ya Kiislamu. Mtume (s.a.w) alipojua kuwa hakuna mtu ambaye angewatunza wake na watoto, au wazee wa masahaba fulani waliotaka kushiriki katika vita vya Jihad, aliwaambia, “Rejeeni mkaziangalie familia zenu, kwani kufanya hivyo ni Jihad kubwa.”
Siku moja kijana mmoja mkakamavu, jasiri na mwenye afya njema, alikuja kumtembelea Mtume (s.a.w), na maswahaba walimstaajabia sana na kuvutiwa naye. Wakiwa wameshindwa kujizuia walisema;
“Ewe Mtume wa Allah! Kama kijana huyu jasiri angeshiriki katika vita kwa ajili ya Mwenyezi Mung (Jihad) ingekuwa jambo jema.”
Mtume (s.a.w) akawajibu, “Ikiwa kijana huyu anafanya juhudi kwa ajili ya mama na baba yake, anafanya juhudi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kama anafanya juhudi ya kulinda staha na heshima yake, anafanya juhudi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kama anafanya juhudi ya kutafuta riziki kwa ajili ya familia yake, anafanya juhudi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Lakini iwapo anafanya hivyo kwa ajili ya kutaka kusifiwa, basi yuko katika njia ya Shetani.” (Haythami, VIII, 144; Al –Mutaqqi, IV, 12/9252)
Katika Hadith ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w) anazungumzia thawabu, anahamasisha malezi ya watoto akisema:
“Zawadi bora ambayo mzazi anaweza kumpa mtoto wake ni tabia njema”. (Bayhaqi, Shuabul Iman, VI, 401 – 402)
Kila mzazi anatakiwa kuwa mfano kwa watoto wake katika ibada, tabia na maadili, na anatakiwa kuwalea tangu wakiwa wadogo, kama inavyosimuliwa katika kisa kifuatacho;
Tangu akiwa mtoto Abdullah bin Abbas alimuiga Mtume (s.a.w) baada ya kumuona akiswali swala ya usiku, na anaielezea kumbukumbu hii nzuri kama ifuatavyo:
“Usiku mmoja nilikuwa kwa shangazi yangu Maymuna, mmojawapo wa wake wa Mtume (s.a.w). Mtukufu Mtume (s.a.w) naye pia alikuwepo. Aliongoza swala ya ishaa, kisha akaja nyumbani na kuswali rakaa nne zaidi. Baada ya kulala kidogo alizinduka, nikamsikia akisema ‘mtoto mpendwa amelala,’ akinikusudia mimi. Kisha aliamka. Nami pia niliamka kuswali, nikasimama upande wake wa kushoto. Mtume (s.a.w) aliniweka upande wake wa kulia, akaswali rakaa tano, kisha akaswali rakaa nne zaidi…” (Bukhari, Ilm, 41)
Katika matukio mengine, akiwa bado mtoto mdogo, Ibn Abbas alishiriki swala ya jeneza na swala za Eid sambamba na Mtume (s.a.w), akipata bahati ya kuswali sana pamoja na Mtume (s.a.w) ( Bukhari, Janazah, 60, Idayn 16)
Mtume alikuwa akila na watoto, akiwaangalia, akizichangamsha akili na nyoyo zao, na akiwasahihisha katika makosa yao kwa njia nzuri.
‘Umar bin Abu Salama alielezea maneno ya hekima ya mtume:
“Nilikuwa miongoni mwa watoto waliolelewa chini ya malezi na uangalizi wa mtume (s.a.w).Wakati nilipokuwa nikila, mkono wangu ulikuwa ukizunguka sahani yote nikichukua, hivyo siku moja mtume akaniambia:
“Kijana, taja jina la M/mungu, kula kwa kutumia mkono wako wa kulia, na kula chakula kilichokuwa upande wako.” (Bukhari, Muslim)
Kwa mujibu wa riwaya nyingine, Mtume Muhammad (s.a.w) alisema “Sogea karibu yangu ule” akimfundisha taratibu za kula kirafiki na maneno mazuri ya upendo. (Ibn Majah)
Kwa hakika, mama na baba ambao wanataka watoto wao kuwa na tabia nzuri zenye kupendeza, ni lazima kwanza wafanye kila liwezekenalo wao wenyewe wawe ni mfano mzuri zaidi wa tabia hizo. Kama mtume alivyosema, “Heshimu wanawake wa wenzako, wanawake wako watakuheshimu, Kuwa mtii na mwenye huruma kwa wazazi wako, watoto wako watakuwa watii na wenye huruma kwako. Mtu ni lazima awe tayari kusamehe ndugu zake hata kama ni wakosa, kinyume na hayo, hatokuwa pamoja nami pembezoni mwa mto wa Kawthar huko peponi.” (Hakim IV, 170/7258)
Tunawajibika siku zote kukaa na watoto wetu kwa huruma, na tusiwapelekee katika fikira zisizofaa. Mfano ufuatao ni somo tosha kwetu sote:
Mtu mmoja alikuja kwa Abdullah bin Mubarak na kumlalamikia kuhusiana na ubaya wa tabia za mwanae. Abdullah bin Mubarak akamuuliza:
“Umeshawahi kumtolea maneno makali mwanao?” hivyo yule mtu akajibu:
“Ndio nimewahi kufanya hivyo” Ndipo Abdullah bin Mubarak aliposema:
“Wewe ndio sababu ya tabia hizo za mwanao”
Nukta nyingine muhimu ni kuwa mama au baba wasijaribu kuwalaghai watoto wao, na wawafundishe kuwa wakarimu. Abdullah bin Amir alielezea:
“Siku moja mama yangu aliniita wakati mtume yupo nyumbani kwetu, alisema:
-Njoo hapa, nataka nikupe kitu, hivyo mtume alipouliza:
-Unakusudia kumpa kitu gani? Mama yangu alijibu:
-Tende. Ndipo mtume akasema:
-Ikiwa hutampa kitu, itanukuliwa katika akili yako kuwa umemdanganya.” (Abu Dawud Adab, 80; \ahmad III, 447)
Katika hadithi nyingine, mtume alisema: Waleeni watoto wenu kwa huruma. Wote wanaohisiwanaweza kuondosha utovu wa nidhamu kwa watoto wao.” (Haythami)
Kwa kuongezea katika mapambano ya wazi ya kuelimisha watoto wetu. Tunawajibika pia kuswali kila siku, kwa kuwa elimu na swala vyote ni muhimu kwa wokovu wao.Ibn Abbas amesimulia, “Mtume alinikumbatia na kusema: “Ewe Allah Mpatie huyu hekima.” Na kwa baraka ya dua ya mtume, wakati alipokuwa mkubwa, alineemeshwa na sifa ya Mwanachuoni mkubwa wa waislamu na pia ni mfasiri wa Qur’an: Mfasiri alieleta changamoto katika maana ya Qur’an.”
Maneno haya yalizungumzwa na wachamungu wakubwa waliotangulia ni mifano mizuri zaidi ya ushauri unaohusu uangalizi wa watoto:
Abu Zakhariah Al-Anbar amesema: “Pasi na kuwa na mbinu mbadala, Taaluma ni sawa na kuni bila ya moto.”
Maneno ya ushauri toka kwa Ali kwenda kwa mwanawe ni mfano mkubwa kwetu sote, pale aliposema, “Ushauri wangu wa kwanza na wa kipaumbele zaidi kwako mwanangu ni kumkhofu Allah kwa kila jambo, kuwa mja wake mtiifu, na umkumbuke katika nafsi yako kila wakati.Kwa uangalifu chunga taratibu zinazokupeleka kwake (Qur’an na Uislamu).Kuna kifungo chochote kinachoweza kuwa kikubwa na muhimu kati yako na muumba? Ichunge nafsi yako kwa umakini kabisa ukitazama wakati wa umauti wako.Pandikiza uchamungu na uharibu matamanio ya nafsi yako, sikiliza kwa makini maneno yangu ya ushauri, tambua kuwa allah, amabe anamiliki kifo cha kila nafsi katika umiliki wake, pia ana miliki maisha yako.Yeye ndie anetoa uhai kwa vilivyopo, ndie ambae anachukua uhai huo, Yeye ndie ambae anamfanya tajiri kuwa masikini, na masikini kuwa tajiri.Yeye ndie ambae huleta kila aina ya taabu, matata, majonzi na maradhi na pia ndie ambae anatoa ulinzi na matibabu.Haijalishi umejihusisha kiasi gani katika elimu, bado utabakiwa na vitu vingi ambavyo ni lazima ukavisome, kwa hiyo kuna kweli nyingi nyuma ya mipaka ya fikira na nguvu za uono.Ikiwa utajaaliwa na lolote miongoni mwa kweli hizi, na allah akakufundisha hekima na busara, usije ukafikiri kwamba umeyapata hayo kwa nguvu zako binafsi.Kinyume chake, chukua kimbilio kwa aliye mtukufu zaidi na umpende, muabudu na umtii yeye pekee inavyotakikana, Uzuri wa ulimwengu huu ni mdogo na uhai wake ni mfupi, na mabadiliko yake ni ya haraka na yenye kuleta huzuni, furaha yake ni ya bandia na neema na ukarimu ni wake ni wakupita, dhambi na dhima yake ni ya milele, siku zote kumbuka chanzo kikuu cha maovu yote ni ni matamanio ya mali na hutakiwi kuruhusu tabia hizi za shetani kuingia ndani ya moyo wako! Kuwa mchamungu utaweza kujizuilia chukua uzoefun toka katika orodha ya waliobarikiwa inawezekana na katu usitume au kutegemea furaha hizi, zitumie katika njia ya Allah”
Imam Ghazali alitoa maneno haya ya usia kwa mwanae “Mwanangu elimu pasi na vitendo ni wazimu, na vitendo pasi na ujuzi ni upuuzi, tambua kwamba elimu hii leo haitakuweka mbali na uasi wala kukupeleka katika utii, hakutakuwa na umbali kati yako na moto wa kuzimu kesho”
Khalifa wa tano kutawala akiwafuatia makhalifa waongofu, Umar bin Abdul Aziz ambae alikifia kilele cha taaluma, hekima na uchamungu, na wakati wa mwaka wake wa pili na nusu kahalifa aliangazia moja ya utendaji wa kuheshimika zaidi, alibadilisha kivitendo kuelekea watoto wake kufuatia ushindi wake kama Khalifa katika siku aliyoigia madarakani, aliwaelekeza watu wakati abdul Malik, shati la mtoto wake lilipokuwa limechanika na wamejichanganya katikati ya kundi la watu walipoona pahala palipochanika, Umar alimwambia mwanawe akalishone shati hilo, “Mwanangu nenda kashone shati lako, unaweza ukawa huna tatizo la mavazi hivi sasa ila baadae ukalihitaji.”
Umar bin Abdul Aziz angeenda chumbani kwa binti yake kila usiku na kumjulia hali yake kabla ya kwenda kulala, usiku mmoja bintiye huyo alikuwa akifumba mdomo wakati wa kuzungumza na baba yake, wakati umar alipomuuliza mtumishi wao kwanini bintiye alifanya vile, alijibu
“Hakukuwa na chochote cha kula isipokuwa vitunguu na maharagwe, walifumba midomo yao ili usihisi harufu ya vitunguu.” Alivutika sana na tabia yao ya kichamungu na hisia ambapo macho yake yalijawa na machozi na akawaambia binti zake, “binti zangu wapendwa ikiwa mtapenda vyakula vizuri na furaha za ulimwengu, baba yenu atapata tabu huko akher”
Pia wakati; Umar alipokuwa katika kitanda chake cha mauti, mmoja aliyekaribu naye akasema “hujaacha mali yoyote kwa ajili ya familia na watoto wako” Ndipo akajibu, “Ikiwa watoto wangu ni watiifu kwa Allah atakuwa radhi nao, ikiwa watoto si watiifu kwa Allah kuwaachia utajiri hakutawasaidia”
Muadh bin Jabal alimuusia mwanawe, “Mwanangu wakti unaposwali, iswali swala hiyo kana kwamba ndiyo swala yako ya mwisho na katu usitarajie kuifika swala inayofuata, muumini anatakiwa kufa akiwa katikati ya mema mawili, wakati muumini anafanya jambo jema, anatakiwa kuwa na malengo ya kufanya jema linguine baada ya hilo, na hakuna jambo ovu litalokuja kati ya mambo haya mema mawili”
Maneno haya ya usia na maonyo ni muhimu sana kwa maisha katika kujichunga kuelekea katika furaha njema kwetu sote, na watoto wetu kutoka na utawala huo tunatakiwa kuzivunja tamaa mbovu na uovu, na kujiandaa wenyewe kwa ajili ya kukutana na muumba kabla hatujauacha ulimwengu huu wenye kukoma katika hali ya kuangalia kwa umakini ni vipi tunatumia uhai wetu, wapi tunapata utajiri wetu na tunautumiaje, ni nguvu kiasi gani tunatumia kuelimisha watoto wetu, watatuletea sifa au kutupunguzia siku ya hukumu na hatimaye matendo yetu yakiwa mazuri au mabaya Qur’an inatumbia: “Na jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni Fitna (mtihani), na kwamba kwa Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa.”(Anfal 8 28)
Mtume (s.a.w) alielezea katika hadithi kuwa mtoto anaefundishwa dini yake, anaandaliwa maisha ya milele huko akhera, na matokeo yake, hufunuliwa ubora wa tabia njema ni maana ya furaha na amani katika ulimwengu huu, na akhera kwa wote yeye mtoto na wazazi wake.Kutokana na habari iliyotolewa na mtume “Baada ya umauti, mja hupandishwa, kisha mja huyo huuliza:
Ewe mola, ni kipi nilichofanya kutunukiwa malipo haya? Ndipo Allah (s.w) atapomjibu
Mtoto wako wema (uliemuacha nyuma) amekuombea na kujitolea kwa ajili ya msamaha wako” (Ibn Majah Adab I Ahmad II, 509)
Kutokana na taarifa ya Ibn Abbas mtume s.a.w, “Mtu aliekufa ndani ya kaburi ni sawa na mfa maji anayetapatapa kutafuta msaada, akitumainia kufikiwa na msaada toka kwa baba mama au rafiki yake mpendwa na hilo ni jepesi zaidi kuliko ulimwengu na vyote vilivyopo ndani yake, Mwenyezi Mungu hushusha rehma kubwa zaidi ya milima humo kaburini kwa wote walio mara nyingi duniani wakijitolea na zawadi kubwa aliyehai kumuendea aliekufa ni kumuombea msamaha” (Daylami Musnad IV; Ali Al-Muttaqi XV)
Katika hali kama hiyo, maana pekee ya wokovu huko akhera ni kuendelea kwa mambo mema tuliyoyawacha na lililo muhimu kuliko mengine yote ni mtoto mchamungu, Asik pasa mtunzi wa Garibname, kitabu cha mashairi ya kisufi alielezea nasaba ya mja huendelea katika sehemu nne
1. Sulbi hii ni nasaba ya mtu binafsi anaemiliki mtoto, na muendelea kwa kizazi hiki kunategemea majaaliwa siku moja kizazi hiki kitakuja kukoma na inatupa mashaka kama nasaba hii itasitawi au la
2. Mali Huu ni usmbazaji wa utajiri na upendo wa mtu binafsi na malipo ya sadaka hii huendelea kwa kadiri mja yule alivyotoa zakat
3. Irshad Hawa ni watoto, na wanafunzi wanaojituma, na ukawaacha baada ya umauti nasaba hii itaendelea kwa kadiri watavyoendelea kufundisha wengine.
4. ‘Ilm ma Irfan hivi ni vitabu au makala zilizoandikwa kuvutia fikira na nafsi zote katika njia ya ukweli, hii ndio njia nzuri na yenye maskahi zaidi kuliko kazi zote kwa kuwa itaendelea kuwavutia kila wasomao makala hizo katika imani kamili, hadi kufikia siku ya hukumu.
Kufuatana na hayo, somo kuu ambalo kila mama na baba anatakiwa kuliangalia kufuatilia elimu za watoto wao na ni lazima tutende hivyo, na kuzuia wivu wa aina yoyote kati ya watoto wetu wakti utapofikia, tutawaingiza watoto wetu katika ndoa ndani ya mipaka ya uwezo wetu na wakati wa kutafuta mke au mume tunawajibika kuzingatia vigezo vya dini yetu na mwenendo mwema, ikiwa ndoa itafanyioka nje ya taratibu hizi huenda ikaishia katika talaka, au itakuwa ni sababu ya mateso na taabu hadi siku ya umauti, tunawajibika kuwachunga watoto wetu katika hali ya juu ya uwezo wetu kuwaepusha na uzembe, kuchelewa kurudi nyumbani, kwenda kuzurura pasi na sababu maalum, na kuepukana na marafiki wasiofaa, tuwaelekeze watoto wetu kuwa makini na majukumu yao, kuwa na heshima kwa familia zao, wakubwa, jirani, wanyonge, yatima, masikini, na kuwaombea kila mara.Tunatakiwa kuwafundisha watoto wetu kuwatembelea wagonjwa, kuwasaidia wenzao, na kujizoesha kutoa sadaka katika kuongeza hali njema ya kiroho kwao, pia tunatakiwa kuakisi uwajibikaji ulioelezwa katika Sunnah za mtume wetu na taarifa za wanachuoni na viongozi waliotazamia upendo, kujitolea, na kusimamia haki na uadilifu katika nyoyo zao
Ewe Mwenyezi mungu waongoze watoto wetu wawe wawajibikaji katika dini yetu hapa nchini na ulimwenguni kote, na uwalinde na kizinga cha uovu na vishawishi vinavyowazunguka na uwajaalie wawe ni sadaka yenye kuendelea kwa ajili yetu huko akhera
Amin!

SAFARI YA MAMA NA BINTI YAKE KUELEKEA UISLAM (SEHEMU YA KWANZA-MARY)

WANAWAKE WAWILI, NJIA MBILI,
MUNGU MMOJA
SAFARI YA MAMA NA BINTI YAKE KUELEKEA UISLAM (SEHEMU YA KWANZA-MARY)
WISDOM; Unaweza kutueleza historia yako kwa ufupi?
MARY; Salam jina langu NI Mary Al-Khaldi nina miaka 48, nafanyakazi kitengo cha huduma kwa wateja kujibu simu katika kampuni ya simu makao makuu vile vile najivunia kusema kuwa nafanya kazi katika taasisi ya Surayya Anne ambayo husaidia wanawake na watoto wenye kuhitaji. Ni mama wa watoto watatu; Eaman mwenye miaka 30, Maria 25 na Sarah mwenye miaka 24, vilevile nina wajukuu 3 wa kike na mmoja wa kiume, na mwengine mmoja wakike mtarajiwa inshallah.
WISDOM; Unamuda gani tangu uwe muislam?
MARY; Nimekuwa muislam moyoni mwangu kwa muda mrefu lakini nilibadilisha imani yangu na ushuhuda na kuanza kuufuata uislam kwa mapenzi yangu tangu miaka miwili iliyopita.
WISDOM; Upi ushiriki wako wa katika dini kabla ya uislam na unaweza kuelezea vipi ushirikiano wako na kanisa au na waumini wa imani yako.
MARY; Nilikuwa mkristo wa dhehebu ia Pentecoste ambalo babu yangu alikuwa ni “miongoni mwa mapadre”1 “Mhubiri”. 2 kwa namna nyengine sikuwa nafahamu ndani ya akili yangu au moyo wangu kwanini au kwa jinsi gani mtu anaweza kutengeneza lugha/sauti, au biblia, na baadae akasema mungu anaongea kupitia mtu mwengine. Zaidi ya hayo, ingawaje nilikuwa binti wa mtoto wa Muhubiri na wazee wa mama yangu walikuwa wamishonari wa kibaptist lakini nilishindwa kupata mantiki/uwelewa juu ya vitu vitatu ndani ya kimoja(mungu watatu ndani ya mmoja);Baba, Mwana na Roho mtakatifu.Nilivutiwa sana na uislam, kitu ambacho kilikaa sana kichwani mwangu;”ndio, Mtume…ndio, Allah ni Mungu na yeye ni mmoja na ndie aliyeumba vitu vyote”,Alhamdulillah. Kwa hiyo hakuna haja ya kuombewa; kwakuwa tuna njia ya wazi na ya moja kwa moja ya kuwasiliana na Allah kupitia swala,kwa wakati wote.Alhamdulillah.
Bado nahisi kuwa ninavyo vilivyo bora kwa ulimwengu wote kwa sababu nina mafundisho ya Biblia kabla ya uislam. Halafu mafundisho kuhusu uislam na Qur’an ni kifunguo cha macho kwakuwa vinelezea ni kwa namna ipi waisilamu pia wanasubiria kurudi kwa yesu na waislam vilevile wanaamini mitume wengine.
WISDOM; Kipi kilikuwa kitu cha kwanza kukuunganisha na uislam? Ulifikiria nini uliposikia kwa mara ya kwanza kuhusu uislam?
MARY; Mara ya kwanza kujifunza uislam ilikuwa mwaka 1978. Mume wangu wa kwanza alikuwa anatokea Iraq. Alhamdulillah,ndani ya miaka hiyo vilevile nilibahatika kukutana na marafiki wengi ambao walitokea Uarabuni na wote ni walikuwa waislam, Mashallah.
Nilikuwa mtoto wa kimasikini, nikimwangalia mama akifanya kazi mbili ili kupata kula ya kutuwezesha kuishi.Baada ya kuusoma uisilamu na kupata kuona ukarimu wa watu(waisilamu) ambao Allah amewaweka katika njia yangu, Hatimaye nikaona uisilam ndio mfumo sahihi kwangu. Hakukuwa na maswali kuhusu mali au elimu, au mazungumzo kama ”gari yangu ni nzuri au bora kuliko yako”.Mwaka 1979 nilikuwa na mtoto wangu wa kwanza.Nilianza kugundua unyoofu wa swala na imani kwa waislam wote ambao walituzunguka. Marafiki kutoka msikitini walihusika na mahitaji ya ndugu zao na waislam wenzao; swala, chakula, pesa, au kitu chochote ambacho mtu anahitaji, Alhamdulillah. Hata pale unapohitaji kuzungumza nao na kukaa nao wanakubali kwa kusema wapo kwa ajili yetu.
Hata, pale nilipopewa talaka na mume wangu wa kwanza, mwanangu alikuwa anaumwa na sikuwa na pesa wakati huo na nilikuwa nahitaji dawa. Nikapiga simu moja basi kila mtu aliniletea msaada. Hata mama yangu alipatwa na hofu/mshangao.
Nilisoma sana na mwenyewe nilifahamu moyoni kuwa mimi ni muislam;lakini kulikuwa na mapambano ndani ya akili yangu, kwahiyo sikuwa natekeleza moja kwa moja uislamu. Ingawaje nilikuwa nawafundisha wanangu kuhusu uislam na kuwaambia wenyewe wanaweza kuamua kuhusu imani zao lakini Allah ndio jina sahihi la Mungu, na ni Mungu wa wote. Mama yangu alikuwa akiwafundisha juu ya ukristo lakini sikugombana nae nilimuheshimu kwa kuwa ni mama yangu na ndie anayefanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha maisha yetu yanakuwa mazuri.
WISDOM; Ni tukio lipi hasa lililokupelekea kuwa muislam? Unakumbuka tarehe yake?
MARY; Baada ya muda mrefu ukawa mwanzo wa maisha yangu,Kaka zangu wote wawili wakawa walevi wa madawa na pombe na wakawa wenye kumtolea lugha chafu mama. Lakini mama alinikataza kuzuia ulevi wao na mama pamoja nao walihamia kwenye mji mwengine. Siku chache baadaye kaka yangu mdogo alimpiga na kumuua kaka mkubwa wakiwa kwenye harakati za kupigana.
Kutokana na hili nilihisi kuwa shetani yupo siku zote. Nikaanza kumlilia Allah ili kufanya haya yote yaondoke katika maisha yangu na moyoni mwangu.Siku moja nikiwa na huzuni nyingi nilikuwa nikiomba. Nilipiga magoti, nikswali wakati wa sijida nililia na kumuomba Allah Aondoe maumivu yote katika maisha yangu, au auchukue kabisa uhai wangu ili niwe na amani, kwa sababu nilifikia sehemu ambayo siwezi kujishughulisha na uhai wangu hata chembe.Alhamdulillah, Aliyafanya haya wiki mbili baadae, ilikuwa tarehe tano, ya mwezi wa tano, mwaka 2008.
Nilikuwa katika matembezi na rafiki yangu. Tulirudi nyumbani kwangu nikajimwagia maji na kuandaa chakula cha jioni.Baadaye nilianza kujisikia vibaya katika kifua changu. Nilitembea mwenyewe na rafiki yangu kuelekea hospitali ambako nililala juu ya meza ya daktari na nikazimia.nilizimia kwa dakika 30. Daktari alinihudumia kwa bidii,kiasi kwamba walitanua mbavu zangu zote wakifanya CPR, na nilikuwa na hali mbili katika moyo wangu. Rafiki yangu ambaye ni muislam wakati huo alikuwa akiniombea kwa Allah ili nizinduke.
Alhamdulillah, nilizinduka. Muujiza ulioje niliamka nikisoma Qur’an ambayo sikuwahi kuisoma kabla ya hapo. Kabla ya mshituko wa moyo wangu nilikuwa naweza kuzungumza vizuri kihispania na kingereza, lakini baada ya mshituko huo wa moyo kingereza chote kiliondoka katika kumbukumbu zangu na sehemu kubwa ya kihispania. Na katika nafasi ya lugha hizo ikaingia Qur’an kuchukua nafasi.3 Na familia yangu walipewa taarifa kuwa sitawezai kutembea wala kuongea tena, lakini Alhamdulillah, ndani ya miezi miwili ya tukio hilo nilirejea kazini. Sasa hivi kila siku naamka usiku na namshukuru Allah kwa maisha, miujiza, hewa ninayovuta, na kuwa muislam. Nashukuru Allah kwa mambo haya na kwa kunijibu maombiyangu,mashallah.4
WISDOM; Ni vipi mumeo, watoto wako na familia yako walipokea mabadiliko yako?
MARY; Mumewangu alifurahia hilo. Mtazamo wa mama yangu ”chochote kitakachonifurahisha” na baba yangu vile vile.Babu zangu wote hawakufurahia lakini waliendelea kunipenda na kunipa moyo. Bibi zangu walishakufa kabla ya hili, na ndugu zangu walijishughulisha na ugomvi tu, kwahiyo hawakusema chochote, Alhamdulillah.
WISDOM; Upi ulikuwa wakati mgumu zaidi na rahisi zaidi katika mihangaiko yako tangu ulipoanza kubadilika?
MARY; Kwa mara ya kwanza, Ilikuwa mwaka 1978, sikuwa nafurahia sana kuwa muislam kwa sababu ingawa nilikuwa navutiwa sana na kujifunza imani pamoja na swala, nilihisi kuwa kila kitu nalazimishwa. Kila mtu aliniambia ”fanya hivi na wengine fanya vile” kwahiyo haikuwa vizuri sana.Lakini Alhamdulillah, hayo yalipita. Nafikiri kila mtu anatakiwa kufundishwa akiwa mdogo na hapo anajifunza kupitia mifano, na sio kwa nguvu au hasira, kama tutatekeleza kile tunachofundisha watoto wetu watatusikiliza vizuri na kutuelewa.
Wakati mzuri au rahisi zaidi kwangu ulikuwa baada ya Mungu kunirudishia pumzi zangu baada ya kuzimia, macho yangu yaliona zaidi ukilinganisha na mwanzo.Niliamka nikisoma Qur’an ingawaje sikuwa najua kuongea kiarabu wala kusoma Qur’an na hadi hivi sasa bado siwezi kuisoma Qur’an.Nimajaaliwa tu ambayo nayapata kila siku, Alhamdulillah.
WISDOM; Kitu gani ambacho unakipenda zaidi katika uislam hivi sasa? Na usichopenda?
MARY: Napenda zaidi umoja(na uaminifu baina ya waislam).na nisichokipenda ni kile kitendo cha mtu kutokuwa na shukurani, unafiki na kuwafanyia wengine umbea au udaku.Pia sipendi pale watu wanapofikiria wanaweza kuwahukumu wengine. Hawana haki ya kuhukumu, chochote/lolote, hasa pale wanapohukumu matendo ya mtu yaliyokwishapita ambayo huwezi tena kuyabadili isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeweza kusamehe. Sisi binadamu hatuna haki ya kumhukumu mtu yeyote, awe mwanamke au mtoto kwa lolote lile. Tunahitaji kutekeleza mafundisho ya Qur’an na sunnah za Mtume na si mafunzo yoyote ya tamaduni za kibinadam. Mafunzo ya kibinadam ni kwa ajili ya heshima na si kwa matakwa ya Mwenyezi mungu.Kule mtu au wazazi wake na wazazi wa wazazi wake wanakotokea hakuwezi kumpa mtu nafasi ya kuamua yeye ni nani, kwahiyo haitoi nafasi ya kutoa hukumu kwake, ila kwa bahati mbaya nimeshuhudia hili likitokea.
WISDOM; Ni kitu gani muhimu zaidi ambacho mara nyingi unahitaji kukifahamu Maria5 kuhusu uislamu kama dini? MARY; Ninajivunia sana Maria kufanya maamuzi ya kuwa muislam na ninajivunia pia watoto wangu wote kufahamu kwa kiasi fulani kuswali na kuwa pamoja na Allah. Mungu ndiye pekee mwenye nguvu Alhamdulillah. Baadaye niliolewa tena na mwanaume kutoka Saud Arabia wakati watoto wangu wanakuwa na yeye alikuwa na mchango mkubwa sana katika maisha ya Maria. Alikuwa akiongea nae kuhusu uislam, Qur’an na Mtume Muhammad (s.a.w). Alikuwa anashindana na nafsi yake yeye mwenyewe kwa mda fulani. Na Mwenyezi Mungu shahidi yangu baadaye mwenyewe aliniambia ”mama nataka kuwa muislam”. Na nililifanikisha hilo na wala sikutoa nafasi kwa shetani/vumbi kumrudia, Alhamdulillah.
WISDOM; Je una aya zozote zile kutoka kwenye Qur’an ambazo hutumia kwa kujikinga au kujilinda au kukupa nguvu?
MARY; Ayat al-kursi na surat Baqarah, Maryam, Falaq na surat Nas. Kwa sasa hivi naweza kusoma vizuri hizi mbili za mwisho na Inshallah, Na soma zaidi kadri ya kumbukumbu yangu itavyojijenga.

ALOZIKWA BUTIAMA

1: NI MINGI SASA MIAKA, TANGU ALIPOONDOKA
    ONDOKA KAMA DHIHAKA, DUNIANI KAFUTIKA
    FUTIKA NA ZAKE TAKA, ZIMEBAKI TWATESEKA
    ALOZIKWA BUTIAMA..............................

2: ALICHOFANYA HAKUNA, TUBAKI KUJIVUNIA
    KUJIVUNIA LA MAANA, URITHI KWA TANZANIA
    TANZANIA TUJE NENA, BABO ALOTUCHIA
    ALOZIKWA BUTIAMA......................

3: AZIMIO ALIUNDA, MALI AKATAIFISHA
   TAIFISHA NA VIWANDA, NA NYUMBA JIMILIKISHA
   JIMILIKISHA NA UKANDA, WA PWANA AKAUFISHA
   ALOZIKWA BUTIAMA.................................

4: ALITUKUZA UDINI, AKAENZI UBAGUZI
   UBAGUZI KWETU PWANI, AKAHUJUMU MAKAZI
   MAKAZI YA VIJIJINI, UJAMAA UKAWINI
   ALOZIKWA BUTIAMA..........................

5: LEO MNAMWITA BABA, SEMENI KWA MKE GANI?
    MKE GANI WA HAIBA, AWE MAMA TAIFANI?
    TAIFANI TUJE SHIBA, ATUOPOE TOPENI?
    ALOZIKWA BUTIAMA.........................

6: LAU LAPIGWA KABURI, NINGELIPIGA LA KWAKE
   LA KWAKE KWA ZAKE SHARI, VIBAYA VITENDO VYAKE
   VYAKE VYA WAZI NA SIRI, ALOFANYA ASIFIKE
   ALOZIKWA BUTIAMA.................................

7: TWAMUOMBA SUBHANA, ATUEPUSHA NA DHAHAMA
    DHAHAMA ZA HUYU BWANA, ALOZIKWA BUTIAMA
    BUTIAMA NANONG'ONA SIJAONA WAKE WEMA
    ALOZIKWA BUTIAMA.......................

8: ALOZIKWA BUTIAMA, SIJAONA WAKE WEMA
    WEMA ULITUAMA, UBAYA UKAUZIMA
    UKAUZIMA DAIMA, USIPATE LA KUSEMA
    ALOZIKWA BUTIAMA............................

FAHAMU KUHUSU UISILAMU NA UKIRISTO

 KATI YA MIONGOZO YA DINI TOFAUTI NI MUONGOZO UPI UMEMTAJA YESU IPASAVYO, MAMA YAKE YESU NA FAMILIA YA YESU?
Uislamu kamwe haujawahi kuwa na uadui dhidi ya Ukristo. Bali, tangu mwanzo wa kudhihiri kwake ulifungua milango ya majadiliano: “Na utawaona walio karibu zaidi (kwa mapenzi) na waumini ni wale wanaosema:  Sisi ni Wakristo.  Hayo ni kwa sababu wako miongoni mwao wanachuoni na wamchao Mwenyezi-Enzi-Mungu, na kwamba wao hawatakabari” (5:82).

Heshima kubwa kwa Yesu Kristo na kwa mama yake Mariam Mtakatifu ni sehemu ya kanuni za mafundisho ya Uaislam: “Na (kumbukeni) malaika waliposema:  Ewe Mariam, Hakika Mwenyezi-Enzi-Mungu amekuchagua na amekutakasa, na amekuchagua kuliko wanawake wate ulimwenguni”.(3:43)

Kufungua  milango ya majadiliano ni kitu kinachopewa  umuhimu mkubwa katika Uislam, kwa sababu kwa upande mmoja mazungumzo na majadiliano haya hufanywa kwa ustahamilivu na utulivu na kwa upande mwingine ni kitu cha kimataifa “Sema: Enyi watu wa kitabu, njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, tusimwabudu ila Mwenye-Enzi-Mungu tu, wala tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yetu wasiwafanye baadhi kuwa ni waungu badala       ya Mwenye-Enzi-Mungu.  Basi wakikataa, waambieni:  Shuhudieni kwamba sisi ni wenye kunyenyekea (kwa Mwenye-Enzi-Mungu)(3:64)

Kama Wakristo wasingekuwa na chuki wangefanya juhudi makhsusi na ya makusudi ya kuichapisha Qur’an pembezoni mwa Injili zao. badala ya Torati ya Agano la Kale ambalo halikumtaja Kristo wala mama yake hata mara moja.  Theluthi nzima ya Qur’an inaelezea maisha ya Kristo na mamaye Mariam.  Hivyo wangelifahamu mengi ndani ya Qur’an kwani imejitosheleza kwa hilo.

Kuna sura nzima ya Qur’an iliyopewa jina la  familia ya Kristo:Al Imran (familia ya Imran). Neno “Al” hupewa familia maalumu zenye hadhi,utukufu na daraja ya juu.  

Aidha, katika Qur’an Tukufu kuna sura nyingi sana zinazoelezea masuala ya Yesu ‘Masih’.  Jinsi gani alivyokuwa akifikisha ujumbe aliotumwa na jinsi alivyoweza kudhihirisha miujiza aliyopewa na Mola wake ili awathibitishie wafuasi wake ‘Mayahudi.  Mfano wa sura hizo ni Suratul Maidah ‘meza’, ndani ya sura hii kuna miujiza mitatu, ambayo haikutajwa katika kitabu chochote cha Injili, isipokuwa Qur’an pekee.  Nayo ni kama ifuatayo.


1.       Uteremshwaji wa chakula kutoka mbinguni: “Akasema Isa bin Mariam: 
Ewe Mwenye-Enzi-Mungu, Mola wetu, tuteremshie chakula kutoka mbinguni ili kiwe sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe dalili itokayo kwako, na turuzuku, na wewe ni mbora wa wanaouruzuku.  Mwenye-Enzi-Mungu akasema:  Bila shaka mimi nitakiteremsha juu yenu, lakini miongoni mwenu atakayekataa mafundisho yangu baada ya haya, basi mimi nitamuadhibu adhabu ambayo sijamwadhibu yeyote katika walimwengu

2.       Kuwapa ndege uhai: “….. na ulipotengeneza udongo sura ya ndege
ukampulizia akawa ndege kwa idhini yangu, na ulipowaponyesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu

3.       Kuzungumza na watu katika utoto: “(kumbuka) Mwenye-Enzi-Mungu
atakaposema:  Ewe Isa bin Mariam; kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipokutia nguvu kwa roho mtakatifu, ukazungumza na watu katika utoto na katika utu uzima wako”.

Kuna sura ndani ya Qur’an iliyopewa jina la Mariam, mama wa Kristo:  Na mtaje Mariam kitabuni alipojitenga na jamaa zake, (akaenda) mahala upande wa mashariki.  Na akaweka pazia kujikinga nao, kisha tukampeleka malaika wetu aliyejimithithilisha kwake kama mtu kamili.  (Mariam) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa rehema aniepushe nawe, ikiwa unamuogopa Mwenye-Enzi-Mungu, (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mjumbe wa Mola wako, nimetumwa ili nikubashirie kupata mtoto mtakatifu.  Akasema: Ninawezaje kupata mtoto hali hajanigusa mwanaume yeyote wala mimi si asherati?  (Malaika) akasema:  Ni kama hivyo, Mola wako amesema; haya ni rahisi kwangu, na ili tuufanye muujiza kwa watu na rehma itokayo kwetu, na ni jambo ambalo limekwisha hukumiwa litokee

Vile vile kuna sura nyingine iliyopewa jina la watu wa pangoni: Alkahf: “Hakika wao ni vijana waliomwamini Mola wao, nasi tukawazidisha katika muongozo

Hizi sura tatu, Al-Maidah, Mariam na Alkahf, ni miongoni mwa sura ndefu katika Qur’an.

 Hata hivyo, pamoja na hayo yote, Mustashriqiina (orientists) na wamishionari wanaunyima Uislam na Mtume wake kila aina ya sifa bora na hawana imani nayo.  Wanataka kuwambia Wakristo kabla ya kuudurusu na kuustaajabia Uislam ambao ni dini na ustaarabu katika historia, kwamba Uislam ni mchanganyiko usio lingana wala kuafikiana na  Uyahudi, Ukristo na Upagani.  Tatizo walilo nalo ni ujinga mkubwa au ushabiki wa upofu uliopindukia, chuki na inda kubwa au yote kwa pamoja.  Ukosefu wa mtazamo sahihi umewapelekea kufika kwenye hitimisho potofu katika uhakiki na utafiti wao.

Huwezi kukosa kuona kitu hata kimoja kinachoaminiwa na dini zote tatu. Ni ajabu kutokuta itikadi moja iliyonadiwa na mitume wote, ijapokuwa dini zipo nyingi.  Nabii Mussa (A.S) alikuja baada ya Ibrahim (A.S) na Mussa (A.S) aliyaamini mafundisho aliyokuja nayo Ibrahim; Issa (A.S) ‘Yesu’ vilevile aliyekuja baada ya hao wote aliyaamini mafundisho yao kuwa ni ya kweli, na hatimaye  Muhammad (S.A.W) ambaye ndiye wa mwisho kabisa, naye amefuata njia hiyo hiyo ya kuyaamini mafundisho ya mitume waliofangulia. Rejea (Sura 2:285) (2:130) (2:285)

“Mtume (S.A.W) ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waislam wote wamemwamini Mwenye-Enzi-Mungu (S.W), na malaika wake na vitabu vyake, na mitume yake ‘yote’ wanasema “Hatutofautishi baina ya yeyote katika mitume yake.  Na husema tumesikia na tumetii …”

Uislam haujasomwa kikamilifu katika vyuo vikuu vingi vya Kimagharibi.  Nasikitika kusema kuwa huenda jambo hili lilifanywa kwa madhumuni maalum; hata hivyo kumekuwepo na baadhi ya waliokwenda kinyume na mtazamo na mwelekeo huo:  Wasomi kadhaa wa kimataifa hawakuwa na itikadi za upendeleo.  Wasomi hao ni kama vile Carlyle, Tolstory, Lord headley, Bernard Shaw, Edward Gibbon, Etienne Dinet, Count Henry de Castry, Renet Ginout, Dr. Griniet, na Roger Garody.  Ni jambo zuri mno kama Wamagharibi wataachana na chuki za kimapokeo dhidi ya Uislam ambazo zimekuwa zikiongezwa bila ya ukweli wowote na mabeberu wa kisiasa na viongozi wao wa kidini wenye ushabiki na inda nyoyoni mwao, na badala yake wausome na kuudurusu Uislam bila upendeleo wowote kama walivyofanya watu waliotajwa hapo juu.  Uongo na uzushi wa mustashriqiina na wamishionari hujirudia mwanzoni mwa kila kizazi.  Hawajapata mambo mapya kwa karne nyingi sasa.  Hung’ang’ania kuzusha mambo yafuatayo bila uthibitisho:-

-              Muhammad hakuwa Mtume kwa sababu alijifunza Qur’an au aliipokea kutoka kwa mtawa aliyeitwa Bahira au kutoka kwa Waraqah bin Nawfal.  {16:105}

“Wanaozua uwongo kwa kusema kuwa Muhammad amefundishwa Qur’an na huyo ‘Mrumi’ ni wale wasio ziamini aya za Mwenye-Enzi-Mungu na hao ndio waongo”

-              Uislam ulienezwa kwa nguvu ya upanga:  Watu walilazimishwa kuingia katika Uislam la sivyo wauawe, wakati ambapo Wahubiri wa Kikristo walipata wafuasi wengi kwa kutumia huruma na ukweli.

-              Uislam uliwakandamiza wanawake na kutangaza ndoa ya mitala.

Kashfa nyingi zilizotolewa na mustashriqiina na wamishionari ni upotoshaji mkubwa.  Ni vizuri wakafuata njia ya utafiti wa kisayansi unaowataka wasomi waadilifu na makini kuusoma Uislam katika namna ambayo Waislam huitumia kuusoma, yaani kuepukana na chuki za kupangwa, kuondokana na madhumuni yasiyokuwa ya kisayansi au mawazo ya ajabu ajabu yasiyotabirika ambayo hupotosha na kutoa mahitimisho yaliyoandaliwa na hivyo kuwa mbali na ukweli.

Mbali na hilo, uzushi huu unaowadhihaki Waislam, unaweza kukanushwa kirahisi kwa ushahidi na uthibitisho.  Wale wanaoushutumu Uislam tunawakumbusha aibu na mapungufu yao wenyewe kwamba, mkutano wa Nicea uliofanyika mwaka 325 A.D.  uliamuru kuchomwa moto kwa vitabu vyote visivyoafikiana na mafundisho ya Kanisa na kupiga marufuku kila kitu kilicho kinyume na imani za Kanisa.  Kwa njia hii Kanisa linajaribu kudhibiti nyoyo na kuzizuia roho za watu ambao zililazimishwa kuamini kile tu kilichoafikiwa katika mkutano huo.

Mkutano huo wa wakuu wa Kanisa ulifanya dhuluma kwa kuweka marufuku hiyo na ulifanya dhambi kwa uchomaji wa vitabu vya dini.  Vikao vilivyofuata baadaye vilirekebisha matendo hayo ya kijinga na kuondosha marufuku iliyowekwa juu ya vitabu vilivyo na elimu sawa ya dini.

Wanahistoria wa Kikristo wanasema kuwa kulikuwepo na Injili nyingi.  Lakini mwishoni mwa karne ya 2 na mwanzoni mwa karne ya tatu kanisa liliamua kubaki na Injili ambazo liliamini kuwa zilikuwa sahihi na hivyo likachagua Injili nne zilizopo leo hii na kuwalazimisha Wakristo kuzifuata sambamba na kuweka udhibiti na ukaguzi mkali na wa hali ya juu ili kuzifuta kabisa zile Injili nyingine.  Je watu wa Ulaya wamewahi kujali au kujiuliza kwamba Injili zilizofutwa zilikuwa na nini na kwa nini zilipigwa marufuku na nani aliyekuwa na haki ya kuzifuata?  Hata hivyo pamoja na kufanya marekebisho na kuvibakisha vitabu walivyoamini kuwa vilikuwa na mafundisho mazuri, Injili hizo sasa zimeingizwa mikono ya watu na kuufanya ukweli wa mafundisho yake kuwa wa kutia shaka kubwa, isipokuwa Injili aliyoiacha Yesu tu.

Wanaushaumbulia Usilam kwamba ulienea kwa nguvu ya upanga!  Kuna tofauti kubwa sana kati ya harakati ufunguzi iliyostaarabika ya kueneza mafundisho, na kulazimisha mafundisho na imani kwa njia ya upanga, kama Charlemagne alivyofanya katika zama za kati, na kama wamishionari waliosuhubiana na utafiti wa kijografia katika zama za leo, walivyofanya huko Afrika na Amerika. (wamishionari hao) waliwaangamiza watu wote, waliingia katika biashara ya utumwa na kuwachukua mamia kwa maelefu ya watu hao kama mateka na kupora maliasili za maeneo husika.  Yote hayo yakifanywa kwa jina la Yesu na kwa baraka za Papa.  Lakini Uislam ulitoa fursa huru kwa mwenye kuamua kuyafuata mafundisho yake ayafuate.

Qur’an Tukufu inasema:- 

          “Hakuna kulazimishwa katika dini (kuingia katika dini), hakika
uongofu umekwisha pambanuka na upotovu umedhihirishwa”

“Na sema huu ni ukweli uliotoka kwa Mola wenu, basi
anayependa akubali, na anayependa basi  akatae, kwa hakika
tumewaandalia madhalimu moto ambao kuta zake zitawazunguka”

“Lakini wakikataa, basi hakika juu yako ni kufikisha tu ujumbe uliowazi”

Injili ya Mathayo 10:34 inasema:-

          Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja
kuleta amani, basi upanga”

Bado wanadai kwamba Uislam ni dini ya upanga lakin Ukristo ni dini ya upendo, iwezekanaje? Kutokana na ushahidi wa {10:34} Mathayo?

Kanisa liliposhusha jina la mwanamke na kumdhalilisha kwa kumuona kuwa ndiye chanzo cha uovu na dhambi, Uislam ulikuja na kuinyanyua daraja ya mwanamke na kuiweka juu.  Muhammad (S.A.W) akasema:-
“Wanawake ni sawa na wanaume”. 

Uislam umemfanya mwanamke kuwa ‘Mnara’ wa wema na huruma; taji linalopamba kichwa cha kila mwanamke wa Kiislam ni mapendo na huruma.  Ndoa ya wake wingi ilienea sana na ikakubalika kwa watu wote hata watumishi wa Kanisa wenyewe.  Mtawala wa Kirumi Jastinian - mtunga sheria wa kipagani- ndiye aliyekuwa wa kwanza kufikiri juu ya kuweka sheria ya kuweka kikomo cha idadi ya wake na kuwa mmoja lakini Kanisa lilipinga fikra yake hiyo.

Uislam ulipokuja ulijaribu kuiwekea udhibiti ndoa ya wake wengi.  Ilikuwa ni kazi ngumu kuzuia mtazamo wao huu.  Bali Uislam ukaingiza utaratibu wa mwanaume mmoja kuruhusiwa kuoa wake hadi wanne.  Hii ilikuwa kama ponyo kwa watu wasiendeleze uchafu wa uzinzi.  Hakuna dhambi kwa asiyeweza kuitekeleza na wala haivunji sheria  za Uislam, ijapokuwa ni bora sana kwa wenye kuweza ‘kufanya uadilifu’ kuna faida nyingi sana katika hili kwa pande zote mbili ‘mke na mume’

          “Ndoa ya mitala ni tiba na sio matendo ya mazoea”

Nani anayesema kuwa Wamagharibi wamefungwa kuwa na mke mmoja tu?  Je siku hizi hakuna ndoa za mitala katika nchi za Kikristo?

Kwa  hakika ndoa ni mkataba unaowekwa baina ya mwanaume na mwanamke.  Lakini kwa kuwa yana husika kwa kiasi kikubwa na mustakbali wa vizazi na kwa kuwa yanaungana sana na uthabiti wa kweli wa nasaba za wahenga kupitia ndoa, Uislam unachukulia muungano huu kuwa ni kitu kitukufu.  Kama tukiiangalia ndoa kama ndoa tunakuta kuwa Wakristo huko Magharibi wana mahusiano ya kimapenzi  na wanawake wengi kuliko hata Waislam. Kwa kweli Wakristo huwa na wanawake wengi bila haya, kile anachokifanya Mwislam kwa kikomo kilichothibitishwa na madhumuni yaliyohalalishwa huchukuliwa kuwa ni aibu au kosa na kuitwa mitala, wakati ambapo Mkristo hufanya ufedhuli bila kuona haya na bila kizuizi haadhibiwi na sheria; ni uzinzi.

Maadui wa Uislam wanatambua vyema kuwa lau wangetumia sehemu ya juhudi zao katika kukashifu na kusingizia mafundisho yoyote kinyume na Uislam mafundisho hayo yangekanushwa.  Lakini ni jambo la kawaida kwamba Uislam husimama imara, kwa utukufu, hupanda milima na hatimaye kushinda  vita vyote vinavyoanzishwa na kupigana dhidi yake.  Kwamba Uislam ni dini ambayo siku zote inakwenda mbele na kukuendelea kwa rehma, ulinzi na msaada wa Allah:-

          Hakika sisi tumeiteremsha Qur’an, na hakika sisi ndio wenye
kuilinda”

Ndani ya kitabu hiki tujadili juu ya imani na mafundisho ya Uislam, si matendo yenye makosa ya baadhi ya wanaofuata dini hii kwa jina tu.  Maisha na matendo ya kweli ya baadhi ya Waislam wa siku hizi yanatofautiana na mtazamo wa Uislam wa kweli.  Uislam sio yale wayaonayo Wamagharibi katika matendo ya mtalii wa Kiarabu ambayo hukanyaga maadili yote wakati akikimbia kwa kutwetatweta kwenda kuridhisha matamanio yake, kwani sio kila Mwarabu ni Muislam na hivyo mitazamo wanayotumia kuhukumu Uislam wanakosea.

Katika kurasa zijazo tutaweka mahakama.  Katika kila kesi au kikao cha mahakama Uislam utaitwa kusimama kama mshitakiwa, mwendesha mashtaka ataleta mashtaka dhidi ya Uislam.  Huyu mwendesha mashtaka atakuwa ni mustashriqiina au mmishionari.  Tutataja jina la kitabu chake ambacho ndani yake tuhuma zimetokea.  Hakimu atauita Uislam kuja kujitetea.  Huyu hakimu ni akili yenye busara,
yenye umakini na hekima inayopenda kudhihirisha ukweli, ikaacha upendeleo na ambayo haina ushabiki.

Uislam utasimama kutii amri ya hakimu na hautahitaji mwanasheria kuutetea kwani kesi iko wazi na dhahiri na Uislam unajiamini utasoma na kutoa hoja zake kwa sauti kupinga mashtaka.  Utetezi wake utaandikwa na ushahidi wake utadokezewa kwa uwazi katika vitabu rejea ili wale wanaohudhuria mahakamani waweze kupata ushahidi huo kwa urahisi.  Kesi itahitimishwa na hakimu ambaye, hatatoa hukumu ya kuachiwa huru au kutiwa hatiani, kwani wasomaji au wasikilizaji wana tabia tofauti za akili na kufikiri.  Sitataja hukumu ya kila mshtaka kulazimisha mtazamo wangu ambao, nina hakika kwamba Uislam hauna dosari na hauna hatia ya mashtaka ya mustashriqiina na wamishionari.  Ni ukamilifu na hauna dosari yoyote, na hauna kasoro zozote, lakini nataka msomaji agundue jambo hili yeye mwenye.

Mwisho ninapenda kuwatanabahisha wale ambao wamejiamulia kashfa dhidi ya Uislam kama kazi yao na kujitolea kuuvunjia heshima, kwamba ukweli na nguvu na ni wenye kushinda na kwamba hisia za chuki katika maamuzi siku zote humpeleka mtu kwenye hitimisho lenye makosa.

Vile vile tunawakumbusha kuwa shutuma zao na mazungumzo yao ya bure yanafahamika vyema na hurudiwarudiwa mara kwa mara, na kwamba Uislam unapotoshwa katika akili zao si katika uhalisia wake.

“Hakika  Mwenye-Enzi-Mungu amewafanyia hisani kubwa Waislam alivyowaletea Mtume miongoni mwao, anayewasomesha aya zake.  Aya zake na anawatakasa na kuwafundisha kitabu na hekima na bila shaka kabla ya hapo walikuwa katika upofu mkubwa” {3:164}

Ninapenda kuwaambia wasomaji kuwa mazungumzo au majadiliano yapo wazi kwa watu wote, kwa utulivu, bila wasiwasi, kwa uadilifu, bila upendeleo, bila chuki, uongo na fujo ambazo kamwe hazipelekei kwenye matokeo yoyote mazuri.

Basi majadiliano baina ya ustaarabu masuala mbali mbali na yaanze katika ulimwengu huu ambapo masafa na na umbali umeondoshwa kuonyesha ukweli.  Mtu anaweza kuwa Damascus, muda wa asubuhi na jioni akawa London au New York, au jioni anaweza kutembelea Paris au Rome na asubuhi akazuru Karatch au Tokyo.  Majadiliano ni njia nzuri ya kudhihirisha ukweli.

Zama mpya au mwanzo wa historia mpya baada ya kufunga mlango wa karne ya ishirini zinapaswa kuanza kwa mtu kutafuta mambo mema popote yalipo hata kama yamo katika Uislam ambao ushabiki wa Kanisa umeiharibu sura yake kwa makusudi machoni mwa Wamagharibi ili kuwazuia wasiukaribie.

Ni wakati mwafaka kwa wapenda elimu na ukweli, kwa kutumia majadiliano ya busara na maarifa, waondokane na picha ya uongo ya Uislam iliyochorwa na ushabiki wenye chuki wa wabebaji wa msalaba.  Uzayuni una nafasi kubwa katika kutangaza propaganda hizo kwa kutumia uwezo wa kila aina ya vyombo vya habari inavyorimiliki.

Katika maisha ya kila siku mtu hufanya juhudi kujua iwapo habari alizosikia ni za kweli au sio za kweli.  Huwenda likawa tukio la kawaida linalorudiwarudiwa mahali popote ulimwenguni.  Katika kutafuta ukweli wa habari au ripoti aliyoisikia binadamu hujiheshimu yeye na huiheshimu akili yake, basi itakuwaje iwapo ukweli anaoutafuta unahusu dini yeye mabilioni ya wafuasi au waumini.  Je hapaswi kuiandaa akili yake katika kutaka kujua misingi na mafundisho ya kweli? Je wakati haujafika wa kuudurusu Uislam kwa busara na bila ya ushabiki na upendeleo katika namna ile ile inayofanywa na mtu mwenye akili kudurusu jambo lolote popote pale ulimwenguni katika maisha yake ya kila siku?  Ninatambua kuwa jibu sahihi la mtu makini ni ndiyo.