Wednesday, March 21, 2012

KWANINI WATU WANA HASIRA



TATIZO LA HASIRA
“Mwanaume mmoja aliyeagiza swandwichi (vipande vya mkate jibini, nyama na vitu vingine katikati) katika mkahawa mmoja alipandwa ghadhabu alipoona kwamba chakula chake kimechukua muda mrefu kuandaliwa, akamtisha mhudumu mmoja wa mkahawa huo, akamsukuma kwenye meza, kumzabua kofi. Kisha mwanaume huyo mwenye hasira akachukua mkate wake na kuondoka.
Sisi sote tuna hukasirika mara kwa mara. Hasira ni sehemu ya hisia zetu kama zilivyo hisia zingine za upendo, tumaini, wasiwasi, huzuni, na woga. Hasira iliyodhibitiwa inaweza kuoneshwa kwa njia inayofaa, na inaweza kuwa na faida. Kwa mfano, hasira inaweza kuwa na faida ikiwa itamfanya mtu aazimie kushinda matatizo au vizuizi Fulani.
Kama kisa kilichopo hapo juu kinavyoonesha, hasira ina madhara pia. Watu Fulani hupandwa na hasira kali za haraka na tena ni mara nyingi zaidi kuliko wengine. Wanapochokozwa huenda wakafoka na kumshambulia mtu. Kwa kufanya hivyo, hasira zao zinawadhibiti badili yaw o kuzizidhibiti. Mtu ambaye hawezi kudhibiti hasira yake husemwa kuwa, anachemka kwa hasira, na kufanya hivyo ni hatari.
Watu wenye matatizo ya hasira hujiumiza wenyewe na kuwaumiza wengine pia. Mtu mwenye tatizo la hasira anaweza kulipuka kwa hasira kwa sababu ya mambo madogo sana na kutenda kwa jeuri, na hilo linaweza kuleta madhara makubwa. Fikiria mifano ifuatayo:
Mwanamume mmoja aliyekuwa akitembea pamoja na rafiki zake barabarani alipigwa risasi shingoni baada ya rafiki yake kumgonga kimakosa mtu waliyekuwa wakipishana nae kwa mkoba aliokuwa ameubeba.
Mwanamume mwenye umri wa miaka kumi na tisa alimpiga na kumuua motto wa miezi kumi na mmoja, wa mchumba wake. Mwanamume huyo alikuwa akicheza mchezo wa video (play station) wenye jeuri alipopandwa na hasira kwa sababu motto alishika kibonyezo Fulani na kumfanya mwanamume huyo ashindwe katika mchezo huo.
Ripoti kama hizo kutoka sehemu zote ulimwenguni zinaonesha kwamba idadi ya watu wenye matatizo ya hasira inaongezeka. Kwa nini idadi hiyo inaongezeka?

No comments:

Post a Comment