Wednesday, March 21, 2012

HIVI KWA MUUNDO HUU TUTAFIKA BAADA YA MIONGO MINGAPI?


Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani la Tanzania(NECTA) haya ndiyo matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2011 

 JUMLA YA WATAHINIWA 3671 SAWA NA ASILIMIA 1.09 WAMEPATA DARAJA LA KWANZA 
 JUMLA YA WATAHINIWA 8,112 SAWA ASILIMIA 2.41 WAMEPATA DARAJA LA PILI
 JUMLA YA WATAHINIWA 21,794  SAWA ASILIMIA 6.48  WAMEPATA DARAJ A LA TATU
 JUMLA YA WATAHINIWA 146,639 SAWA  ASILIMIA 43.60  WAMEPATA DARAJA LA NNE 
 JUMLA YA WATANIHIWA 156,085 SAWA ASILIMIA 46.41 WAMEPATA  DARAJA SIFURI

Kulingana na taarifa hizi kati ya daraja la 1- 111 ufaulu ni asilimia 9.98 ,Ukilinganisha na wale waliopata kati ya daraja la
IV - 0 ambao wamepata asilimia 90.01 

Baraza la Mitihani (NECTA) wamekaririwa wakisema kuwa kiwango cha ufaulu kimeongezeka sasa ni wakati wetu wanaharakati wapenda maendeleo ya taifa letu  kuyachambua na kuyafanyia tathimini  matokeo haya, kisha tuambiane je kiwango cha ufaulu kwa hali hii kinaongezeka au kinapungua. Je hii ndiyo elimu bora nchini Tanzania? 

No comments:

Post a Comment